Baadhi nchi Ughaibuni zamgombea Lissu, zadai ziara zake ni maslahi binafsi na kuharibu mahusiano

TataMadiba

JF-Expert Member
Feb 7, 2014
9,866
5,742
Ziara za Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu nje ya nchi zimegonga mwamba baada ya baadhi ya nchi hizo kubaini kuwa ziara hizo zinaweza kuathiri mahusiano mazuri ya kidiplomasia ambayo Tanzania imekuwa nayo kwa muda mrefu na nchi hizo.

Nchi hizo zimebainisha pia kuwa Lissu anatumia ziara hizo kwa ajili ya maslahi binafsi ya kujipatia fedha na umaarufu wa kisiasa.

Aidha Watanzania waishio katika baadhi ya nchi hizo wametahadharishana kutotumiwa na Wanasiasa kutoka Tanzania ili kuepukana kufutiwa vibali vya kuishi katika nchi hizo kutokana na kwenda kinyume na sheria za nchi hizo.

Baadhi ya nchi ambazo tayari zipo taarifa kuwa zimeyakataa maombi ya Lissu kwenda kufanya mahojiano na vyombo vya habari vya nchi hizo na kuomba misaada ya kifedha ni pamoja na

Ufaransa
Sweden
Denmark
Urusi

Kufuatia hatua hiyo ya baadhi ya nchi hizo kupiga marufuku shughuli zozote za kisiasa za Lissu katika nchi zao, uongozi wa hospitali anayotibiwa Lissu ya chuo kikuu cha Leuven nchini Ubelgiji kwa kuhofia kutiliwa shaka na sheria za uuguzi nchini humo inasemekana unaweza kuamua kumshauri Lissu aamue aidha kutulia hospitalini ili aendelee na matibabu au arejee nyumbani Tanzania.

Tafakuri: Ingeshangaza sana kama Lissu angeendelea kufanya siasa katika nchi za wazungu. Wenzetu wana akili sana,wanajua kupima atahari ya jambo lolote na hawasiti kuchukua hatua za haraka pale wanapoona mataifa yao yanaweza kuingizwa kwenye matatizo yasiyo ya lazima. Kimsingi hata kule ambako Lissu alibahatika kuongea na vyombo vya habari walikuwa wanamsanifu tu.

Tukio hili la Lissu na lile la maandamano ya Mange Kimambi yanapaswa kuwa mfano mzuri kwa watanzania tujitambue. Ni rahisi ukatumiwa na mataifa haya kama kibaraka wo ukiwa tanzania lakini siyo ukiwa katika mataifa yao. Hili wanalizingatia sana kwa maslahi mapana ya mataifa yao.


 
Baadhi ya Nchi ambazo tayari zipo taarifa kuwa zimeyakataa Maombi ya Lissu kwenda kufanya mahojiano na Vyombo vya habari vya nchi hizo na kuomba misaada ya Kifedha ni pamoja na
  1. Ufaransa
  2. Sweden
  3. Denmark
  4. Urusi.
Hivi Lissu aende Urusi kufanya nini kwenye nchi ambayo wasiokubaliana na Kremlin wanashambuliwa ama kuua kwa sumu? Ufaransa ina ushawishi kiasi gani kwenye siasa za nchi yetu?

Sweden na Denmark sidhani kama ziko kwenye orodha ya ziara ya Lissu iliyotolewa awali!!
 
Kumbe ndiyo maana Mnyiramba hasikiki tena? Arudi tu akalime alizeti maana hata Ubunge sasa ni hatihati kuendelea nao
 
Back
Top Bottom