Baadaya ya JK na Banda kutoa kauli zao leo Kamati kukutana kuhusu mpaka kwenye ziwa Malawi

Unaposema nisome international bilateral treaty nicompare na riparian rights kwa dhumuni gani?

Treaty ni makubaliano. Makubaliano ya nguvu ya kwanza kabla ya lolote. Riparian right unazosema zimekuja baada ya makubaliano ya 1890.
 
Maelezo yako mkuu ni mazuri na marejeo ya bunge la tanganyika pia,Fikiri pamaoja nami
hivi kabla ya mkataba wa heligland ziwa lote lilikuwa la Nyasaland? kwa mantiki kwamba wananchi wa kyera kule matema beach na kwingineko walikuwa hawachoti maji wala kuvua samaki ziwa nyasa? kama walikuwa wanachota, baada ya mkataba huo kufungwa utaratibu uliofuata anayeujua atueleze kuhusu ziwa hilo ili urejewe baada ya Mama Banda kudai ziwa lote ni lao.
Mimi naona matamshi ya kawawa hayakuwa na mantiki kwani raia wake wa kyera wangepata wapi maji baada ya kusema Tz hahina hata asilimia moja ya ziwa hilo inamaanisha wananchi wangechota maji ya ziwa wale tu wanaomiliki passport zinazowaruhusu kuvuka mipaka ya nchi.
Naona maamuzi ya UN ndo sahihi yanayoruhusu nchi zinazopakana kwa mpaka wa maziwa wagawane katikati kwani wananchi wa pande zote mbili walikuwa wanatumia maji ya maziwa hayo bila kujua hata kama upande wa pili wa ziwa kuna watu wengine.Mjadiliano juu ya suala hili inabidi yafanyike kwa makini na siyo tu mtu kukurupuka.
 
Maelezo yako mkuu ni mazuri na marejeo ya bunge la tanganyika pia,Fikiri pamaoja nami
hivi kabla ya mkataba wa heligoland ziwa lote lilikuwa la Nyasaland?

Kabla ya Heligoland achilia mbali Nyasaland kumiliki ziwa bali hata wilaya za Kyela, Tukuyu na sehemu kadhaa za Mbeya zilikuwa za watemi wa Nyasaland. Hili ni jibu la Banda lililomnyamazisha Nyerere alipoanza kuleta mdaia kwa ziwa hilo. Banda alisema kuwa kuwadai ziwa Nyasa ni kuongeza chumvi kwenye kidonda kwa kunyang'anywa na wakoloni sehemu hizo ambazo hata lugha utasikia ni zile za Malawi. Banda alisema anazitaja tu sehemu hizi kumkumbusha Nyerere historia lakini wao kama Malawi hawana mpago kuzidai kwani wanaheshimu makubaliano ya OAU ya mwaka 1963 kwamba mipaka iliyowekwa na wakoloni na tuliyorithi ibaki hivyohivyo.



kwa mantiki kwamba wananchi wa kyera kule matema beach na kwingineko walikuwa hawachoti maji wala kuvua samaki ziwa nyasa? kama walikuwa wanachota, baada ya mkataba huo kufungwa utaratibu uliofuata anayeujua atueleze kuhusu ziwa hilo ili urejewe baada ya Mama Banda kudai ziwa lote ni lao.

Hotuba hiyo ya Banda inasema wazi kwamba Malawi haijawahi kukataza mtanzania kuvua, kuogelea au kutumia ziwa hilo. Alisema hivi: lets all fish and swim in the beautiful lake Malawi...
 
Treaty ni makubaliano. Makubaliano ya nguvu ya kwanza kabla ya lolote. Riparian right unazosema zimekuja baada ya makubaliano ya 1890.

Ndo maana nimesema riparian rights zina nafasi yake katika hili suala la ziwa kuwa mpakani mwa nchi.

Hiyo Heligoland treaty ni kiini macho tu cha Wamalawi. Tungepata mjanja naye angeneutralize hiyo Heligoland treaty na ile British order in council ya mwaka 1902 wakati Waingereza wanapeana jukumu/ lindo la himaya yao ya Nyasaland "lindo"/ himaya inaishia upande wa magharibi wa ziwa Nyasa. Waingereza hawakulijumuisha ziwa Nyasa kwenye himaya yao
 
Laana ya kikwete hiyo mbona utawala wa wenzake wamalawi hawakuja kudai ziwa nyasa! Avue gamba lake kwanza amvishe paka aone itakuwaje.
 
Ndo maana nimesema riparian rights zina nafasi yake katika hili suala la ziwa kuwa mpakani mwa nchi.

Hiyo Heligoland treaty ni kiini macho tu cha Wamalawi. Tungepata mjanja naye angeneutralize hiyo Heligoland treaty na ile British order in council ya mwaka 1902 wakati Waingereza wanapeana jukumu/ lindo la himaya yao ya Nyasaland "lindo"/ himaya inaishia upande wa magharibi wa ziwa Nyasa. Waingereza hawakulijumuisha ziwa Nyasa kwenye himaya yao

Order in Council ya 1902 isingeweza kufanya lolote maana hiyo ni Sheria ya British Monarch ambayo isingekuwa na nguvu kwenye Germany territory ambapo Germany ndiyo ilikuwa inatawala hapa mwaka huo 1902!
 
Order in Council ya 1902 isingeweza kufanya lolote maana hiyo ni Sheria ya British Monarch ambayo isingekuwa na nguvu kwenye Germany territory ambapo Germany ndiyo ilikuwa inatawala hapa mwaka huo 1902!
Mkuu nimetumia neno lindo hapo kusudi ili kila mtu anielewe. Hapo Muingereza alikuwa anawaonesha watumishi wake mipaka ya eneo/himaya yao. Hilo eneo halikuijumuisha ziwa Nyasa hata hivyo.

Kwa maneno mengine baada ya Heligoland treaty Waingereza sasa wanatuma wenzao waje kufanya shughuli za utawala huko Malawi mwaka 1902. Wanawaelekeza watumishi wao kwamba mtaenda Nyasaland himaya yetu(Waingereza) itaanzia magharibi mwa ziwa Nyasa
 
hansard za bunge ni kukmbukumbu za kila siku (kumbukumbu za ukweli na za utata na za uongo uliokawia kubainika). ndio maana
1: kauli ya liwalo na limo imo ktk hansard
2: ripoti ya kamati ya mwakyembe ambayo leo kundi la lowasa linadai si ya kweli nayo ipo ktk hansard
3: uongo wa mwigulu nchemba kuhusu vurugu za ndago nazo zipo hansard.
Therefore hata kauli ya kawawa sitashangaa kuwapo hansard na japo ni uongo.
ndio maana wamalawi wanatucheka kuwa elimu yetu finyu! Hansard ni kumbukumbu ya kinachosemwa bungeni. Ikumbukwe nyerere alipinga madai ya malawi ina maana hakuisoma hiyo hansard?

N
 
Mkuu nimetumia neno lindo hapo kusudi ili kila mtu anielewe. Hapo Muingereza alikuwa anawaonesha watumishi wake mipaka ya eneo/himaya yao. Hilo eneo halikuijumuisha ziwa Nyasa hata hivyo.

Kwa maneno mengine baada ya Heligoland treaty Waingereza sasa wanatuma wenzao waje kufanya shughuli za utawala huko Malawi mwaka 1902. Wanawaelekeza watumishi wao kwamba mtaenda Nyasaland himaya yetu(Waingereza) itaanzia magharibi mwa ziwa Nyasa

Heligoland treaty is bilateral isingeweza kubadilishwa na mtu mwingine bali Germany na Britain kukutana. Maadam hawakukutana na kutia saini hadi huo mwaka 1902 basi Heligoland treaty haijawahi kuwa overrulled.

Kama ni suala la kuelekeza settlers kuwa mpaka wenu ni katikati hayo maelekezo hayafuti makubaliano yaliyopo. Monarch wa UK hakuwa na mamlaka ya kubadi hata nukta kwenye mkataba ule na hakuwa na mamlaka ya kubadili hata sentimeta moja ya ardhi bila kutiliana saini na mwenzake wa Ujerumani.
 
ndio maana wamalawi wanatucheka kuwa elimu yetu finyu! Hansard ni kumbukumbu ya kinachosemwa bungeni. Ikumbukwe nyerere alipinga madai ya malawi ina maana hakuisoma hiyo hansard?

N

Wewe ndiye mbumbumbu unayeropoka toka kitandani mwako bila kufanya research. Katika uhai wake, Julius Nyerere hakuwahi kupinga madai ya Malawi kwamba Ziwa lote ni la Malawi!
 
Wewe ndiye mbumbumbu unayeropoka toka kitandani mwako bila kufanya research. Katika uhai wake, Julius Nyerere hakuwahi kupinga madai ya Malawi kwamba Ziwa lote ni la Malawi!
google (nyerere on lake nyasa issue) article ya kwanza. Isome halafu rudi niambie kama kweli hajawahi
Kupinga., ndg ucwe mtukanaji
M
 
Hilo ziwa bora walichikue wamalawi.
Agreement iwe kuwaruhusu watanzania pembezoni mwa ziwa waendelee kuoga, kunywa maji ya Nyasa. Pamoja na kuvua samaki.
Kama ni mafuta yabaki malawi.
Tanzania tuna mengi na hatuyathamini
Dhahabu imejaa nchi nzima.
Almasi, Uranium, copper, chuma,
Tanzanite siisemi.
Gesi bwerere Ntwara.
Waachie wamalawi Wese lao.
 
Hizo stori tuu ila wajeda na zana zao wamepelekwa wakumwaga huko ziwani, na mimi nisahfika kule kuna vituo vya jeshi letu ndani ya ziwa pamoja na boti za kijeshi, malawi hawajaziona tangu kale leo waseme ziwa lote ni lao? Kimsingi lazima tuna miliki sehemu fulani ya ziwa watake wasitake, nakumbuka tushapigan vita ya masaa kadhaa na hao jamaa wakasalimu amri miaka ya sabini sasa watakoma. Ila liwalo na liwe. Kmwalimu aliwaambia kama ziwa lote ni lao basi waondoe maji yao yasiguse ardhi yetu wakashindwa. Naomba kwenda vitani kama itatokea. Heri kufa ukipigania haki yako kuliko kufa ukinyanyaswa na kilico chako nawe umekaa kimya
 
google (nyerere on lake nyasa issue) article ya kwanza. Isome halafu rudi niambie kama kweli hajawahi
Kupinga., ndg ucwe mtukanaji
M

Wala sina haja ya kuzisoma maana zote hizo nilishazisoma siku nyingi zilizopita. Wewe ndiye uliyesoma hapo lakini hukuelewa.

Mwalimu Nyerere hakuwahi kutamka kwamba tuna umiliki wowote wa ziwa lile. Mimi naomba huko unaposoma hebu copy na ku-paste hapa statetement yake inayokufanya udhani kwamba aliwahi kutamka unavyodai.

Nimekutega hivyo nikijua wengi mnakurupuka na kudhani Nyerere naye alikuwa mkurupukaji kama mnavyofanya nyinyi. Ukisoma documents zote utagundua Nyerere alitamka nini na mimi sitaki nikutafunie maana unajua kusoma.

Kwa kukusaidia soma hansard ya Rashid Kawawa akiwaleleza msimamo wa Tanganyika June 1962 huku Nyerere akiwa mbunge kama backbench na hakupinga hoja ya Kawawa mle bungeni!
 
Hilo ziwa bora walichikue wamalawi.
Agreement iwe kuwaruhusu watanzania pembezoni mwa ziwa waendelee kuoga, kunywa maji ya Nyasa. Pamoja na kuvua samaki.
Kama ni mafuta yabaki malawi.
Tanzania tuna mengi na hatuyathamini
Dhahabu imejaa nchi nzima.
Almasi, Uranium, copper, chuma,
Tanzanite siisemi.
Gesi bwerere Ntwara.
Waachie wamalawi Wese lao.

Hapo kwenye RED ndivyo ilivyo siku zote, na kwa aliyewahi kufuatilia history ya mzozo huu anafahamu wazi kwamba hiyo ndiyo busara ya Rais kamuzu Banda aliyoitamka mwaka 1967 kwamba kila mtu alitumie hilo ziwa.

Lakini kwa propoganda zikafanya akili zifundishwe kuhasamiana na Malawi na Tanzania kuliko kuangalia walau busara za maraisi wote wawili yaani Nyerere na Kamuzu Banda.

Hivi wewe na akili zako unaweza kuamini kwamba Kamuzu Banda alikuwa lunatic kiasi hicho!!!
 
Hakuna UN convention inayokupa haki kwa Ziwa Malawi. UN convetion imeset hiyo ruling kama hakuna any recognised agreement wakati hapa recognised agreement ni Anglo-Germany treaty inayotambuliwa na kumbukumbu za Serikali ya Tanzania.

Washabiki wa hili mliolikurupukia inabidi tuanze kujadili matokeo ya kukurupuka. Na kwa Membe na Lowasa hili halitaacha kuwa doa kwao kwa safari zao za kisiasa. Wameidanganya nchi lakini wameshidnwa kuidanganya dunia.

Mimi sina wasiwasi kabisa na matokeo ya mkutano wa leo huko Malawi kwamba watanzania tutapewa ukweli waziwazi kwamba hatuna hata tone moja.

Niko radhi Moderator anipige life ban kama haitakuw hivyo kwani nimesimamia ukweli na wanaosema tofauti wamesimami uongo ambao karibu wataumbuka ila wasimpomoshee kejeli Membe ambao baadhi wameshaanza kama huyu gulio hapa chini:
Haya mambo tuliyazungumza sana hapa, tukaambiwa sisi si Wazalendo tukaitwa kila aina ya majina, anyway kikao kinaendelea ila kwa sasa nadhani kinachotakiwa sasa, delegate yetu huko kwenye kikao ibadili agenga, na ajenda iwe "ni vipi Malawi wataanza kulipa gharama za maji yao kugusa aridhi yetu".

Haya mambo ni ya ajabu sana, hivi ikitokea (tsunami)mafuriko (siombei itokee na ninamuomba Mungu isiwe hivyo kabisa)na sehemu ya aridhi yetu (livingstone mountain) inamezwa na maji ya ziwa Nyasa na eneo la ziwa linaongezeka upande wa Tanzania, je itakuwaje hapo - ardhi yetu si itakuwa imekwenda Malawi pia?
 
Nadhani kinachotakiwa sasa, delegate yetu huko kwenye kikao ibadili agenda, ili tuwadai Wamalawi gharama za maji yao kugusa aridhi yetu, but haya mambo ni ya ajabu sana, hivi ikitokea (tsunami)mafuriko (siombei itokee na ninamuomba Mungu isiwe hivyo kabisa)na sehemu ya aridhi yetu inamezwa na maji na ziwa Nyasa na ukubwa unaongezeka, so inakuwaje aridhi itakuwa imekwenda Malawi pia?

Hapo kwenye RED, watu kama nyinyi ndiyo walau mna hoja zinatushawishi na kamati iliyoko huko ikitegemea ulichokiandika basi walau tutakuwa na ahueni kwamba hizi ni sababu za walau tukalipata ziwa hili.

Kuliko porojo nyingi zilizotamba humu wakati hata mimi tu ninaweza kuzipinga, sembuse wataalamu waliobobea wa Malawi na ambao Malawi imewateau kwenye hiyo technical comitee!

I salute you bana.
 
Kwa mimi mzaliwa na niishie matema naipa serikali option mbili kwaza ni kuclaim na kuweka clear nusu ya ziwa ni mali ya TZ au kutuacha tuwe wananchi wa malawi lakini vinginevyo hakuna solution hata wakiwapa wamalawi hilo ziwa sisi hatutakubali.
 
I salute you Nikupateje kwani ulichoandika ni kweli kabisa. Binafsi mwanzo niliamini mengi yaliyosemwa na mawaziri wetu lakini niliishiwa nguvu mara baada ya kusoma kwa umakini makala yakisomi ya James Mayall yenye kichwa cha habari 'The Malawi-Tanzania Boundary Dispute' ya December 1973. Ukweli ni kwamba hata Nyerere hakuwahi kufanikiwa kumshawishi Banda kuwa sehemu ya ziwa lile lipo Tanzania mbali na kuishia kumtishia Banda kuwa basi utanilipa kwa kila wimbi la ziwa hilo linalogusa ardhi yangu. Haraka za viongozi wetu kuitangaza Tanzania kuwa iko tayari kuingia vitani kama Malawi wangeendelea na utafutaji mafuta kumetuaibisha kama taifa na hili lazima tulikubari. Kwa wamalawi wanaolewa wanatuona sisi ni wababe na wapenda vita na watu wanaoweza kung'ang'ania kisicho chetu.

Hapo ndipo ninapoona busara za JK kwani naye angeweza kufuata mkumbo na kuendeleza ubishi wenye nia ya kuwafurahisha wanaotaka kulifanya suala hili liwe mtaji wakisiasa, basi ingekuwa aibu kubwa kwa taifa. Wakati tunao wasomi wengi kuliko Malawi na vyuo vikuu vingi kuliko Malawi, suala hili lingetushushia hadhi na tukaonekana ni watu wanaofanya maamuzi magumu bila kufanya research. Inafaa sana katika suala hili watanzania tuka-negotiate kwa namna ya kupata haki ya matumuzi ya maji na rasilimali zake hata kama mpaka upo upande wetu.
 
Back
Top Bottom