Uchaguzi 2020 Baada ya watanzania kumchagua Magufuli kwenye Uchaguzi Mkuu hakika huo ndio utakuwa mwanzo wa mwisho wa Upinzani

Hizi ni njozi za alinacha tu, tunaingia ktk nguvu ya soko la kunadi sera za vyama kama "supply" na pia tunasikilizia muitikio wa wapigakura kama "demand". Hicho unachotaka kutuaminisha ktk mada yako mbona ni kama ndoto za alinacha pia.
 
IMG-20200826-WA0087.jpg
 
Kama upinzani kufa, basi ilikuwa ni kipindi hiki cha hii miaka mitano ya mwanzo. Kama hilo limeshindikana ndio ataweza kwenye awamu yake ya mwisho kama atashinda? Kwa ujumla, udhaifu na uimara wake kila mtu ameujua, hatakuwa na lolote jipya zaidi ya haya aliyoyafanya sasa zaidi ya kukamilisha miradi aliyoianza, iwapo ataweza kabla ya kutoka madarakani. Hao waliofanikiwa kuwa washabiki wake ndio hao hao, lakini hana uwezo wowote wa kuwabadilisha wasiomkubali, na hawatabadilika. Upinzani sio vyama bali ni fikra, na hilo halitakufa kamwe.
 
Mwaka huu CCM wataacha kovu lisilopona kwa upinzani. Amini hili
 
Umesema kaka, baada ya uchaguzi mitandao ya kijamii itabaki safi na kazi kwa TCRA zitapungua sana.

Tuko huku mitandaoni kabla Magufuli hajawaza kuwa rais wa nchi hii, na ameingia madarakani bado tuko na mitazamo yetu hii hii. Tuko kwenye upinzani kwa mitazamo, na hatuko kwenye upinzani kwa kufuata mkumbo.
 
Kama upinzani kufa, basi ilikuwa ni kipindi hiki cha hii miaka mitano ya mwanzo. Kama hilo limeshindikana ndio ataweza kwenye awamu yake ya mwisho kama atashinda? Kwa ujumla, udhaifu na uimara wake kila mtu ameujua, hatakuwa na lolote jipya zaidi ya haya aliyoyafanya sasa zaidi ya kukamilisha miradi aliyoianza, iwapo ataweza kabla ya kutoka madarakani. Hao waliofanikiwa kuwa washabiki wake ndio hao hao, lakini hana uwezo wowote wa kuwabadilisha wasiomkubali, na hawatabadilika. Upinzani sio vyama bali ni fikra, na hilo halitakufa kamwe.
Ni fikra zinazobadilika baada ya wenye fikra za kuwa wapinzani kupata wanachokitaka, nacho ni maendeleo ya kweli.
 
Mwaka huu CCM wataacha kovu lisilopona kwa upinzani. Amini hili

Sio kwa kura, bali kwa matumizi mabaya ya madaraka. Na kwa taarifa yako hakuna ccm, bali kuna madaraka ya rais yanayotumika vibaya kuibeba ccm.
 
Tuko huku mitandaoni kabla Magufuli hajawaza kuwa rais wa nchi hii, na ameingia madarakani bado tuko na mitazamo yetu hii hii. Tuko kwenye upinzani kwa mitazamo, na hatuko kwenye upinzani kwa kufuata mkumbo.
Watu kama wewe wenye mawazo kama yako uwa wanapotea baada ya kuona wapo pekee yao kwenye mapambano ya wasichoamini kama ni sahihi
 
Ni fikra zinazobadilika baada ya wenye fikra za kuwa wapinzani kupata wanachokitaka, nacho ni maendeleo ya kweli.

Maendeleo ni wajibu wa serikali yoyote, hata iliyoingia madarakani kwa kupindua nchi. Upinzani ni mitazamo mbadala ya chama kilichoko madarakani. Kama maendeleo ndio yanaondoa upinzani, basi nchi zote zenye maendeleo zisingekuwa na vyama vya upinzani. Kwa uwezo huu mdogo wa uelewa, unadhani upinzani upo kwa sababu hakukuwa na bwawa la umeme huko Ruvu, hii inaonyesha ulivyo na uwezo mdogo.
 
Watu kama wewe wenye mawazo kama yako uwa wanapotea baada ya kuona wapo pekee yao kwenye mapambano ya wasichoamini kama ni sahihi

Ukiwa mpinzani unayejua maana ya upinzani huhitaji kuwa na watu wengi wafuata mkumbo, kwa sababu hujui maana ya upinzani ndio maana unadhani upinzani uko maana hakukuwa na ndege. Kwa hili mwenye tatizo ni ww usiyejua upinzani ni nini. Subiri Magufuli atangazwe mshindi kwa hiyo idadi ya wapiga kura ya kupika ya watu 29m+, kisha uone kama upinzani utakufa.
 
Imani tuliyonayo watanzania kwa jemedari wetu wa mapambano dhidi ya ufisadi, rushwa, uhujumu uchumi na uzembe ni wa kiwango kisichotiliwa shaka yoyote hususani kwa tukio lilipo mbele yetu la uchaguzi. Binafsi , mimi ni mmoja wa waumini safi wa kazi na misimamo ya Rais Magufuli kwa rasilimali zetu , sina shaka na maoni haya hata kwa walio wengi.

Tulianza naye safari pamoja na kwa hakika safari ya kuelekea nchi ya ahadi mwaka 2020- 2025 tutakuwa naye pamoja. Ahadi ya elimu bila malipo, kudhibiti upotevu wa mapato, matumizi bora na sahihi ya kodi za watanzania, miundombinu rafiki ya kuchochea uchumi na maendeleo ndio sababu ya imani kubwa tuliyonayo watanzania kwa Rais Magufuli. Si rahisi hata kidogo kufanya anayofanya Rais Magufuli bila kuwa na uthubutu

Ni mengi sana mazuri aliyofanya kwa nchi yetu na yale ambaye hajafanikiwa kuyafanya ni changamoto zinazohitaji muda zaidi na ndio maana tunasema miaka 5 ijayo Tanzania itaonesha maajabu makubwa sana kimataifa na wengi kustaajabishwa na uthubutu wa kiongozi huyu. Ni mitano tena kwa Magufuli

Awamu ya pili ya Rais Magufuli kwa waliojaliwa kuangalia mambo kwa jicho la tatu watakubaliana nami kwamba ndio utakuwa mwanzo wa mwisho wa upinzani kwa sababu kuu mbili: mosi, upinzani utakuwa umeshuhudia nguvu na uwezo halisi wa CCM na kwa kuwa watakuwa wametumia nguvu na uwezo wao wote kuitoa CCM madarakani na wakashindwa basi mwisho wa upinzani ni dhahiri. Pili, katika awamu ya pili ya Rais Magufuli yatafanyika makubwa sana katika taifa hili ambayo watanzania wataachana na fikra zote na mawazo yote ya upinzani kushika dola na kukubali CCM itawale milele.

Nawashauri wapinzani na upinzani kwa ujumla wajiandae kwa mwisho huu wenye maumivu makali lakini hakuna namna wa kurudisha wakati nyuma kuwashawishi watanzania kuikataa CCM.
mlishawishi sana wabunge waunge juhudi kwa kudhani upinzani 2020 hautakuwepo, sasa mnayoshuhudia hadi mnalewa vibe la upinzani hahaha
 
Kama mmeshindwa kuumaliza miaka hii mitano ambayo, mmefanya siasa wenyewe, kuwateka na kuwatesa, kuwabambikia kesi nk, kwa sasa sahauni kabisa hiyo habari
Huwezi jua kuwa upinzani umeisha mpaka baada ya uchaguzi.
 
Nadhani unamanisha kuwa upinzani utaongezeka mara dufu, maana rais wangu ni rais wa visasi...anasema waziwazi hatapeleka maendeleo mahali watachaguliwa wapinzani...
Ingawa alikuwa anakuwa rais ambae angefuta kweli upinzani kama tu serikali yake isingekuwa ya chuki na visa.
Ila akirudi nakuhakikishia upinzani utakuwa mkubwa mno maana sio nje ya chama chetu hata ndani kuna watu wengi wameumizwa na wataumizwa sana
 
Kumbe upinzani bado upo! Nilidhani yale mapambio ya upinzani kufa ni ya kweli kumbe maneno tu yakumfurahisha malaika mkuu ili wapambe washibishe matumbo yao
 
Back
Top Bottom