Pdidy
JF-Expert Member
- Nov 22, 2007
- 50,956
- 22,148
MKUU wa mkoa wa Mwanza, Abbas Kandoro ametangaza nia yake ya kugombe ubunge jimbo la Kalenga wilaya ya Iringa Vijijini katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu.
Kandoro alitangaza nia yake hiyo kwenye kikao cha Shirikisho la Wenye Viwanda nchini (CTI), kilichokuwa kikifanyika katika hoteli ya New Mwanza.
Alisema ameamua kutangaza rasmi kuwa anatarajia kuwania ubunge katika jimbo la Kalenga ambalo kwa sasa linashikiliwa na Steven Galinoma baada ya kuona kuwa anaweza kuwatumikia wananchi wa jimbo hilo.
"Ubunge si lelemama mimi mwenyewe nilikaa kwa muda
nikajiuliza je? Ninaweza kuwatumikia wananchi nikaona nina weza hivyo ninayosababu ya kutangaza nia yangu ya kuwania ubunge ili niwatumikie wananchi,"
alisema Kandoro
Alisema kutokana na hali hiyo ndiyo maana huko nyuma baadhi
ya vyombo vya habari vilikuwa vikiandika hata alipofika Mwanza wanahabari walimuuliza lakini hakuweza kusema chochote kwa kuwa bado alikuwa akitafakari.
Alisema kuwa pamoja na kuwa yeye ameamua kutangaza nia
yake hiyo, lakini watu wanaotarajia kujitokeza kwa nia ya kuwania ubunge wakae na kujiuliza kuwa kweli wana nia ya dhati ya kuwatumikia wananchi na siyo vinginevyo