Baada ya wamachinga/omba omba kumshinda Dar; Abbas Kandoro aomba ubunge Kalenga

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,720
21,779
MKUU wa mkoa wa Mwanza, Abbas Kandoro ametangaza nia yake ya kugombe ubunge jimbo la Kalenga wilaya ya Iringa Vijijini katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu.

Kandoro alitangaza nia yake hiyo kwenye kikao cha Shirikisho la Wenye Viwanda nchini (CTI), kilichokuwa kikifanyika katika hoteli ya New Mwanza.

Alisema ameamua kutangaza rasmi kuwa anatarajia kuwania ubunge katika jimbo la Kalenga ambalo kwa sasa linashikiliwa na Steven Galinoma baada ya kuona kuwa anaweza kuwatumikia wananchi wa jimbo hilo.

"Ubunge si lelemama mimi mwenyewe nilikaa kwa muda

nikajiuliza je? Ninaweza kuwatumikia wananchi nikaona nina weza hivyo ninayosababu ya kutangaza nia yangu ya kuwania ubunge ili niwatumikie wananchi,"

alisema Kandoro

Alisema kutokana na hali hiyo ndiyo maana huko nyuma baadhi

ya vyombo vya habari vilikuwa vikiandika hata alipofika Mwanza wanahabari walimuuliza lakini hakuweza kusema chochote kwa kuwa bado alikuwa akitafakari.

Alisema kuwa pamoja na kuwa yeye ameamua kutangaza nia

yake hiyo, lakini watu wanaotarajia kujitokeza kwa nia ya kuwania ubunge wakae na kujiuliza kuwa kweli wana nia ya dhati ya kuwatumikia wananchi na siyo vinginevyo
 
Atamshinda kirahisi yule babu ambaye alikuwa anataka kufia bungeni, Galinoma.
 
Huyu kandoro nae vipi? Kwani huko Mwanza anamtumikia nani? Bungeni sio mahala pa kwenda kupumzika!
 
mbona mnamkosea heshima na haki ya msingi kandoro?.....
nani ambae wamachinga amewamudu?
 
Nyie acheni kumshambulia Kandoro. Kandoro alifanya kazi nzuri Dar. Na sasa Mwanza yuko fit. Huyo ninawaambieni anafaa kuwa mbunge kwa sababu he is effective and he will definitely deliver. Nikiongea kinabii huyu anakuja kuwa Waziri wa TAMISEMI next government ya Kikwete. Kwa vile CV yake inaruhusu
 
Nyie acheni kumshambulia Kandoro. Kandoro alifanya kazi nzuri Dar. Na sasa Mwanza yuko fit. Huyo ninawaambieni anafaa kuwa mbunge kwa sababu he is effective and he will definitely deliver. Nikiongea kinabii huyu anakuja kuwa Waziri wa TAMISEMI next government ya Kikwete. Kwa vile CV yake inaruhusu
Kandoro Dar es Salaam aliweza nini tuambie? Uchafu uliisha? Foleni barabarani ziliisha? Machangudoa waliondoka? Kelele za muziki na promosheni je? Wanasiasa wote siku hizi slogan zao ni "kuwatumikia wananchi", "nimeombwa na wazee", n.k. Ukweli ni kwamba wanasukumwa na maslahi yao binafsi hasa yatokanayo na kuwa na madaraka. Kandoro hana tofauti yoyote.
 
Zipo taarifa kwamba alitumia hela za michango ya ujenzi wa madarasa kununua wajumbe wa ccm , hata hivyo alipigwa chini .
 
Back
Top Bottom