samsun
JF-Expert Member
- Feb 9, 2014
- 7,386
- 5,962
Wakuu nadhani mko poa kama nilivyoamka mimi.
Kama kichwa cha habari kinavyosema,baada ya wafanyakazi "hewa" hebu tuangalie na "hewa" zingine. Kama ilivyo kwa nchi yetu jinsi watu "wanavyojiongeza" basi hata kwenye sehemu nyingine za kiutekelezaji wa mambo ya kijamii lazima watakuwa "wanajiongeza" pia. Sasa namuomba mh Rais wetu Dr.John Joseph Pombe Magufuli aangazie na upande mwingine wa hiki kitu "hewa" kwenye, MIRADI hewa, ZABUNI hewa, WAFUNGWA hewa, VIFAA hewa,WANAFUNZI hewa, MIKOPO hewa,PEMBEJEO ZA KILIMO hewa.n.k
MIRADI HEWA : Hapa utakuta serikali imekusudia kutekeleza miradi kadhaa,mfano ya maji sasa kuna mojawapo linaweza kufanywa kama si mradi usiwepo kabisa basi upo robo ya kusudio lakini serikalini unajulikana kama mradi umekamilika na unafanya kazi.
ZABUNI HEWA: Hapa inatangazwa zabuni kwaajili tu ya kutekeleza wajibu wa kutangaza lakini tayari mtu keshapatikana na keshapewa malipo ya awali ili aanze kazi.
WAFUNGWA HEWA: Hapa utakuta magereza yetu yanatoa taarifa ya wafungwa wapo wengi sana kwenye magereza yetu lakini kumbe karibia nusu ya idadi iliyotolewa si ya kweli.Lakini huku ndio unapokuta hesabu ya milo inayojulikana eidha haipo au haipo kwa kiwango kinachoelezwa.
VIFAA HEWA: Hapa ndipo kwenye "uvundo" wenyewe,spea za magari,pikipiki,mitambo na mashine mbalimbali kuna moja kati ya haya yanaweza kufanyika,kutoa taarifa ya kifaa fulani kimeharibika (wanakiharibu makusudi au wanakitoa hiko kifaa) na ikitolewa pesa ya kwenda kukinunua watu pesa wanapiga kisha kesho mashine/mtambo/gari/ pikipiki inafanyakazi watu wameshachukua chao
WANAFUNZI HEWA: Hapa hasa kwenye hizi shule za bweni za serikali inatolewa idadi kuuuuuuuuuuubwa lakini wanafunzi waliopo hata robo ya hiyo idadi haipo sasa najua unajua nini kinacholengwa hapo, wanapata bajeti kubwa sana kuliko hali hlisi.
MIKOPO HEWA: Hapa ni kule vyuoni ambapo inaelezwa idadi kuuuubwa ya waliopatiwa mikopo lakini sio kweli na mara nyingi wanajikopesha wenyewe na hawalipi ila serikalini inaelezwa kuwa wamepewa wanafunzi.
PEMBEJEO ZA KILIMO HEWA: Huku kuna balaa si kitoto mabwana na mabibi shamba na wenzao wanazichezea pesa za serikali si kitoto. kuna kuwapa pembejeo za kilimo wakulima "hewa" na wanaopewa ni wachache mno kuliko idadi iliopo kwenye makaratasi ya serikali.
Wakuu ongezeeni sehemu nyingine ambazo "hewa" ni balaa ili kama kuna mtumishi anayesoma uzi huu ajue anatumia mbinu gani au anaanzia wapi kuwakamata.
Ni hayo tu.