Synthesizer
JF-Expert Member
- Feb 15, 2010
- 11,143
- 18,774
Wengi walidhani kwamba Chadema walichelewa kuingia uwanjani kwenye msiba wa Mkapa na ndio maana walizuiwa kuingia. Hata account ya Sugu ilidafuliwa kupandikiza wazo hilo. Yote haya yalikuwa mpango maalum. Njama.
NIlieleza wazi kwamba habari kutoka jikoni zilieleza wazi kwamba kwa makusudi kabisa Chadema walipewa muda wa kuwasili uwanjani ambao wangekuta Raisi Magufuli ameisha ingia uwanjani, na hivyo wazuiwe kuingia kwa kisingizio cha kufuata protokali, kwamba wasingeingia baada ya Raisi Magufuli kuwa ameshaingia.
Lakini ukweli ni kwamba tukio hili la msiba lililofanyika siku moja tu baada ya Lissu kurejea nchini, lilihofiwa kwamba lingempaisha Lissu kwa free publicity. Hata kuna watu walihisi kwamba Lissu angeshangiliwa pale ambapo angekuwa akiishuka garini, na hili lilionekana kwamba ni jambo lisilokubalika kabisa, kwa kuzingatia uwepo wa vyombo vingi vya habari na watu waliokuwa wakiangalia luninga na kusikiliza redio juu ya tukio hili.
Hata ilihofiwa kwamba kesho yake Lissu angekuwa habari kuu kwa baadhi ya magazeti badala ya tukio la msiba, kwa vichwa kama "Umati wa waobolezaji waziziam kumshangilia Lissu akiingia uwanjani kwenye msiba wa Mkapa".
Hiki ndicho kilisababisha kwa makusudi kabisa viongozi wa Chadema wachezewe kwa kupewa muda ambao wangeambiwa wamechelewa na Raisi Magufuli ameshaingia uwanjani hivyo wasingeruhusiwa kuingia kama ujumbe.