Baada ya vitisho NATO, Putin aomba kuzungumza na Biden

Mrengwa wa kulia

JF-Expert Member
Mar 21, 2022
975
3,459
MAJI sasa HAYA NYWEKI
tunasema samaki katema Ndoano.
Beki hazikabi tena.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Sergei Lavrov amefanya mahojiano na kituo cha televisheni cha serikali Rossiya 1,
ambapo alisisitiza kwamba Marekani imekuwa ikihusika kwa muda mrefu katika vita vya Ukraine.

"Inaonekana kwangu kwamba Wamarekani wamekuwa wakishiriki kwa kweli katika vita hivi vya muda mrefu, "Lavrov alisema.

Akizungumzia uwezekano kwamba Uturuki inaweza kuandaa mazungumzo kati ya Urusi na nchi za Magharibi, Lavrov alisema Moscow itakuwa tayari kusikiliza mapendekezo yoyote na kwamba Rais wa Uturuki Erdogan na Rais Putin wanaweza kujadili hili wakati wa mkutano huko Kazakhstan baadaye wiki hii.

Lavrov pia alisema kwamba wale wanaoendelea kukisia kuhusu vita vya nyuklia vinavyodaiwa vitasababishwa na Moscow wanapaswa kutambua wajibu wao kwa kile wanachosema, na kwamba Putin "amesema mara kwa mara kwamba katika mafundisho yetu ya nyuklia tunachukulia hii kama hatua ya kulipiza kisasi pekee".

Lavrov aliongeza kuwa Urusi haitakataa mkutano kati ya Rais Putin na Rais wa Marekani Biden katika mkutano ujao wa G20 na itazingatia pendekezo hilo iwapo itaupokea.

wakati huo huo

. Katibu mkuu wa NATO aionya Urusi dhidi ya kushambulia miundombinu yake

Shambulio lolote dhidi ya miundombinu muhimu ya muungano wa kijeshi wa NATO litasababisha "mwitikio wa umoja na mkali", Katibu Mkuu wa NATO Jens Stoltenberg ameonya.

Stoltenberg aliuambia mkutano wa waandishi wa habari kwamba washirika wa NATO walikuwa wakiongeza usalama karibu na mitambo muhimu baada ya mashambulizi kwenye mabomba ya gesi yanayopita chini ya Bahari ya Baltic.

Bado haijafahamika ni nani alikuwa nyuma ya kulipuliwa kwa mabomba hayo.

Akizungumzia vitisho vya siri vya matumizi ya silaha za nyuklia na Rais wa Urusi Vladimir Putin, Stoltenberg alisema kuwa NATO inafuatilia kwa karibu vikosi vya nyuklia vya Urusi na haijaona mabadiliko yoyote katika mkao wao.
SOURCE

AFP
ROSSIYA. (shirika la habar la russia).
BBC.


NAONA HATIMAE ANDUNJE ANATAFUTA TUNDU LA KUTOKEA.
 
Mtoa mada wapi Mrusi kasema kataka akutane na Biden au viongozi wa Nato, alicho sema Russian haikatai kuongea na hao viongozi kama Rais wa Turkey atataka kuwapatanisha, Russian toka mwanzo hajakataa kuongea hata na Ukraine sa usiwe unaongea vitu havipo kwenye habari. Eti maji yamemfika shingoni 😂

Al Arabiya wanasema Mrusi bado hajatumia silaha zake za kisasa bado yani hizo silaha anazo tumia ni za zamani, kijana Mrusi we msikie tu ndio mana US anapigana naye yeye kakaa nyuma anawasogeza wengine mbele
 
Putin au Mwingine? Putin anataka hiyo vita iishe 2030. Ana chukua Jimbo moja baada ya jingine afu ana lima ngano huku ana pigana. Yeye aki vuta zake Kiko.

Leo amekutana kiongozi wa UAE jaribu kapuku kuruka kama NATO na USA haija kukamata. Yeye akitaka hata kujisaidia Germany ana tua hapo
 
Bomba zimelipuliwa na NATO hakuna ubishi kwa uchochezi wa US.

Mmarekani anacheza karata zake taratiiiiiiibu huku anakunywa Gahawa.
 
9720f514-50b1-46e7-bd2a-c7f3458097fa.jpg
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom