Baada ya viongozi wa kijiji kutupotezea miaka 8 wakicheza political games, naiona miaka 5 mingne iki

Mar 17, 2016
193
188
Kijiji chetu tangu miaka ile alipojiuzuru mjumbe mkuu wa serikali ya kijiji ya awamu ya 4, kilianza kuwashuhudia viongozi kutoka milengwa yote ya kulia na kushoto wakitumia mda mwingi wakicheza michezo ya siasa.

Muchuano mkali alikuwa ndani ya wale wa mlengwa wa kulia huku wale wa mlengwa wa kushoto wakifanya hasa kazi ya kutia chumvi ktk mchezo kwa kuwasema sema wale walioonekana kuwa wachezaji maarufu kuwa sio waaminifu kwa kijiji chetu.
Kadiri tulipokaribia kwenda kumtafta Mwenyekiti mpya, ndivyo muchuano ulivozidi kuwa mukali, wajumbe wa mwenyekiti, wawakilishi kutoka mashinani, waumini wa mlengwa, watumishi wa kijiji, wachuuzi maarufu wa kijiji hadi wachunga kondoo, wote walijikuta ktk mchezo, kwa ufupi shughuli za kuleta maendeleo ya kijiji zilipewa nafasi ya mwisho kabisa.

Wajumbe wa Mwenyekiti wakiwa wanabadilishwa hapa na pale, kulingana na taarifa za upande wao ktk mchezo, watumishi waandamizi nao hvo hvo.Nasikia hadi vijiji vingine vikaanza kuingia ktk mchezo hasa kile kijiji kikubwa kinachojumuisha vijiji vidogo vidogo 52, kile chenye watu wengi zaidi na wafupi wafupi na kile kijiji maarufu kwa kuanzisha vita kubwa kubwa.

Mchezo ukafikia hatua ngumu hasa pale mjumbe mkuu yule mstafu mwenye rangi nyeupe juu alipohamia mlengwa wa kushoto na kupata uungwaji mkono toka kwa baadhi ya waliowahi kuwa wajumbe wa kijiji akiwemo yule Mzee maarufu wa kijiji.

Kijiji kimefanikiwa kupata Mwenyekiti mpya na wajumbe wapya, lkn wasiwasi wangu ni kuwa dalili za michezo ile naanza kuziona zikirudi. Safari hii zinamhusisha Mwenyekiti na wajumbe wake kwa upande mmoja, japo baadhi ya wajumbe wanaonekana pia kutokuwa upande wa Mwenyekiti hasa yule mjumbe wa vt vituzungukavyo, yule mwenye lami dhidi ya wachuuzi maarufu wa kijiji chetu kwa upande mmoja, na dhidi ya mlengwa wa kushoto kwa upande wa pili, ambao sasa wanaye mcheza michezo hii maarufu wa kijiji chetu japo hajawahi shida game hata moja ya high profile.

Ukiacha hzo pande maarufu ktk mchezo huu, wapo pia wenyeviti wastafu wa kijiji chetu wa miaka ya karibuni, wawakilishi wa mashina ambao pia ni wachuuzi maarufu, waliokuwa wajumbe wa serikali ya kijiji iliyopita, viongozi na watumishi hasa wanaosemekana wamejinufaisha sana kupitia jasho la wanakijij.

Ni hali hii inanifanya nipatwe na wasi wasi kuwa endapo viongoz wetu hawa, hawatakaa chini na kuweka uzalendo mbele na kuiacha michezo hii hadi pale mda wake utakapofika, huenda sisi wakazu wa kijiji hiki tukaendelea kukumbwa na matatizo ambayo tumekuwa nayo Siku zote, japo kila Siku tunaambiwa kijiji chetu sio maskini kama tunavyodhani.
 
Back
Top Bottom