Baada ya video kusambaa mtuhumiwa mwenye pingu akipigwa, askari aliyehusika awekwa mahabusu

Jamal Akbar

JF-Expert Member
Oct 9, 2014
413
471
Imetolewa na Jeshi la Polisi:

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI:

Ndugu wanahabari,

Imeonekana kipande cha video kwenye mitandao ya kijamii inayoonyesha kijana mmoja akiwa na pingu huku akipigwa na askari, kitendo ambacho ni kinyume cha sheria.

Ndugu wanahabari,

Kitendo hicho si tu ni kinyume cha sheria, bali pia ni kinyume na maadili ya Jeshi la Polisi.Tukio hilo limeshachukuliwa hatua kuanzia jana na kamanda wa Polisi Kinondoni na askari aliyehusika yupo mahabusu na hatua stahiki zinaendelea kuchukuliwa dhidi yake.

Kijana anayeonekana katika kipande cha video hiyo akipigwa, alituhumiwa kuiba simu aina ya Samsung Galaxy Note 10 ambayo alikiri kuiba na kwenda kuonyesha kwa mtu aliyemuuzia ambaye naye alikutwa na simu hiyo.
Jeshi la Polisi chini ya Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, litaendelea kusimamia Nidhamu, Haki, Weledi a Uadilifu kwa kuchukua hatua stahiki dhidi ya askari Polisi anayekiuka sheria na maadili ya Jeshi la Polisi.


PRESS.jpg
 
Imetolewa na Jeshi la Polisi:

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI:

Ndugu wanahabari,

Imeonekana kipande cha video kwenye mitandao ya kijamii inayoonyesha kijana mmoja akiwa na pingu huku akipigwa na askari, kitendo ambacho ni kinyume cha sheria.
...
Afande Misime, this is a tip of an ice berg, This is the order of the day!!
 
Viko vingi tu zaidi ya hivyo.

Napendekeza askari wenu mue mnawapiga msasa matumizi sahihi ya PGO.

Wengi wao Yale mafunzo ya CCP washayasahau Wana act kwa hisia
Wanajikosha tu kwa vile wamerekodiwa unyama wa Polisi unazidi hata wa shetani eti tunasimamia maadili ya kazi wakati kila leo mahabusu wanafia vituo vya Polisi shame
 
Tuendelee kuwarecord na wao wataendelea kuchukua hatua.
 
Tatizo hawa police wameshatuona sisi ni mazuzu, jibu hili linalingana na la tiss kuhusu issue ya yule raia aliyekwaruzana na tiss officer's barabara na watendaji hawa wa tiss wakaamua to do arrest (kisheria hawaruhusiwi, ni jeshi la police pekee wenye uwezo to arrest),Ile case imeshakua ni cold 🥶 one
 
Hilo li form 4 failures wanapiga raia hadi kituoni unakuta wamemfunga mtu wanamgonga virungu.....isiwe taabu niliisha apa kuua limoja
Kuua haitasaidia tatizo ni mfumo..naamini siku serikali ya CCM Itaondoka madarakani na kupisha akili mpya, tutaexperience mabadiliko chanya mengi.
 
Baada ya video inayomuonesha askari akimpiga mtuhumiwa aliyekaa chini akiwa na pingu, Jeshi la Polisi limemchukulia hatua askari huyo kwa kumuweka mahabusu.

Msemaji wa Polisi, SACP David Misime amesema: “Kitendo alichofanya askati huyo si tu ni kinyume cha sheria bali pia ni kinyume cha maadili ya Polisi, tayari hatua zimechukuliwa na Kamanda wa Polisi Kinondoni.

“Kijana anayeonekana akipigwa alituhumiwa kuiba simu aina ya Samsung Galaxy Note 10 ambayo alikiri kuiba na kwenda kuonesha mtu aliyemuuzia."
Fa2PG-LX0AAyjVy.jpg
 
Back
Top Bottom