Baada ya uteuzi wa Philip Mpango kuwa Makamu wa Rais wa JMT, sasa naamini watu kama Makonda, Chalamila, Ole Sabaya hawana nafasi katika Serikali

The Palm Tree

JF-Expert Member
Apr 13, 2013
7,032
2,000
Kwa kumteua Dkt. Philip Isdor Mpango kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ni ishara muhimu ya kuonesha kuwa Madam President Samia Suluhu Hassani, atakuwa Rais wa namna gani.

Kumbukumbu zinaonesha kuwa Dkt. Philip I. Mpango ni mtu safi na mwadilifu.

Hana makando kando yanayoweza kuwa mjadala. Kama kuna makosa fulani fulani aliyatenda ktk kipindi chote cha uwaziri wa fedha, itakuwa ni kwa sababu ya nature ya uongozi wa boss wake aliyekuwa anafanya nae kazi yaani Mwendazake John Pombe Magufuli..

Binafsi sioni kama ni Rais atakayefuata nyayo za Mwendazake Hayati Pombe ambaye kila mtu anajua sifa zake, kuwa, alikuwa Rais asiyeambilika wala kushaurika , mwoneaji, katili na hakuona shida kumwaga damu ya wakosoaji wake.

Ni wazi kabisa kuwa, Rais Samia Suluhu Hassan hawezi kuchukuliana na viongozi wenye tabia na hulka za mwendazake.

Viongozi kama DC wa Hai Ole Sabaya; DC wa Arumeru Jerry Muro; aliyekuwa RC wa DSM Paul Makonda a.k.a Daudi Albert Bashite; RC wa Mbeya Chalamila, RC Iringa Ally Hapi na wengine kibao wanaofanana na hawa, hawana chao tena.

Wanaodhani kuwa hawa wanaweza kupata nafasi ya uongozi ktk utawala wake, wafikiri mara mbili mbili.

Hata hizi nafasi za uongozi wanazoshikilia kwa sasa, ni suala la muda tu kuwa wataziacha na kurudi walikotoka..

Tukumbuke kuwa, siku zote mpanda ngazi huwa ni lazima ashuke.
 
mukaruka mzee

JF-Expert Member
Jan 22, 2020
970
500
Kinachofuata mama avunje Baraza la mawaziri na alisuke upya.
Huu nao pia ni ushauri kwa kiongozi wetu mpya, Rais Samia Suluhu Hassan, basi tusubiri kwani yote, kuvunja na kuunda Baraza jipya la Mawaziri au kuendelea na hili au kulifanyia marekebisho kidogo kadri apendavyo, YOTE YAKO NDANI YA UWEZO WAKE au siyo! Tusubiri tuone.
 
LIMBOMAMBOMA

JF-Expert Member
Oct 3, 2017
8,791
2,000
Huu nao pia ni ushauri kwa kiongozi wetu mpya, Rais Samia Suluhu Hassan, basi tusubiri kwani yote, kuvunja na kuunda Baraza jipya la Mawaziri au kuendelea na hili au kulifanyia marekebisho kidogo kadri apendavyo, YOTE YAKO NDANI YA UWEZO WAKE au siyo! Tusubiri tuone.
Lengo ni Jema Sana la kutoa ushauri huu, kuendeleza na Baraza la zamani haitakuwa njema, kwa maoni yangu pm, kmk, dpp na Ag waondolewe haraka, mama ateue wa kwake.
 
The Palm Tree

JF-Expert Member
Apr 13, 2013
7,032
2,000
Nimeyasoma mawazo yako NAYAHESHIMU ila kwa kweli ni vizuri tusubiri tuone yajayo bila kuwa na jaziba au chuki za wazi wazi kwa yoyote. Huu ni ushauri tu, halafu, nilikuwa napita tu!
Asante kwa kusimama na kusema neno badala ya kupita tu.

Kusubiri na kuona atafanya nini, ni jambo zuri.

Lakini hili halizuii watu kusema neno kwa kila hatua anayopiga kwenda mbele. Hii itamsaidia asije akajikwaa ktk hatua zake.

Na binafsi sina chuki na yeyote hata ktk wale niliowataja.

Lakini unasahau jambo moja kuwa, matendo ya mtu huambatana naye na kiukweli ndiyo yanampa sifa mtu huyo.

Niliowataja matendo ya uongozi wao ni ya hovyo na haya comply na maadili ya Utumishi wa umma.

Mama Samia Suluhu akiwabeba hawa, sooner or later watamnyea mikononi mwake.

Ni onyo tu kwake.
 
FUSO

JF-Expert Member
Nov 19, 2010
23,297
2,000
Mama yetu Samia, watanzania baadhi wameumizwa sana - hata kufurahia hayo madaraja sijui reli mpya inakuwa ngumu kwao kwa maumivu waliyonayo - yaani kuwa kwenye siasa za upinzani imekuwa kama ni kukata tiketi ya mashitaka ya uhaini ama mauti.

Ni muda sasa wa kuwapunzisha hawa watanzania wenzetu - wameumizwa sana, sana !! Mtoa hoja amekupa list ambayo ilikuwa ni ya hatari... list ukicheza nayo hauonekani mitaani. Anza na hiyo list kwa kuanzia - si watu wazuri kabisa!

Tuna imani kwa pamoja tutaijenga Tanzania yetu mpya irudie kwenye msingi yake ya Umoja na Udugu ambapo vyama vya siasa ilikuwa ulingo wa kujibizana kwa hoja na utani hasa hasa wakati wa kampeni.

Turejeshee utamaduni wetu wa awali mama yetu mpendwa.
 
misasa

JF-Expert Member
Feb 5, 2014
11,344
2,000
Tunasema timu ile ile ila kiwanja tofauti, wale walifikiria kwenda kunywa juisi ikulu wasahau.

Nina imani president n VP
 
This is...

JF-Expert Member
Dec 28, 2014
2,335
2,000
Huu nao pia ni ushauri kwa kiongozi wetu mpya, Rais Samia Suluhu Hassan, basi tusubiri kwani yote, kuvunja na kuunda Baraza jipya la Mawaziri au kuendelea na hili au kulifanyia marekebisho kidogo kadri apendavyo, YOTE YAKO NDANI YA UWEZO WAKE au siyo! Tusubiri tuone.
Katiba hairuhusu yote uliyoorodhesha.

Lazima Rais mpya avunje baraza la mawaziri.Ateuwe upya na awaapishe yeye km mteuaji.

Lazima Rais mpya ateuwe Waziri Mkuu mpya na Waziri Mkuu huyo ale kiapo mbele ya Rais.

Kikatiba hakuna kwamba nitaendelea na Hawa hawa. Lazima Waziri mkuu na baraza la mawaziri aliteuwe na liape mbele yake km Rais.
 
mukaruka mzee

JF-Expert Member
Jan 22, 2020
970
500
Katiba hairuhusu yote uliyoorodhesha.

Lazima Rais mpya avunje baraza la mawaziri.Ateuwe upya na awaapishe yeye km mteuaji.

Lazima Rais mpya ateuwe Waziri Mkuu mpya na Waziri Mkuu huyo ale kiapo mbele ya Rais.

Kikatiba hakuna kwamba nitaendelea na Hawa hawa. Lazima Waziri mkuu na baraza la mawaziri aliteuwe na liape mbele yake km Rais.
Well nisingependa kuingia kwenye malumbano ya kisheria ambako siko kwangu, ila uzoefu unaonesha kuwa SIYO LAZIMA every incoming new president aanze au ateue baraza la mawaziri lake. It is rightly assumed kuwa kwenye uteuzi wa haya mabaraza ya mawaziri, Rais mara nyingi, kama sio zote, huwa akishauriana na Makamu wake , so it is assumed! Tusubiri tuone hiki mnachosema na kutafsiri nyie wasomi wa sheria.
 
Natena wiza

JF-Expert Member
Mar 13, 2021
322
500
Lengo ni Jema Sana la kutoa ushauri huu, kuendeleza na Baraza la zamani haitakuwa njema, kwa maoni yangu pm, kmk, dpp na Ag waondolewe haraka, mama ateue wa kwake.
Watu mnatafuta sana PM, na kwa bahati mbaya Sioni hilo likitokea. Ukizungumzia kubadili baadhi ya maafisa nitakubali, ila swala la kuvunja Baraza ili kumuondoa Majaliwa kwenye System ni humu sana.Sidhani kama Samia hamhitaji kiasi hicho waziri aliyepo Sasa.

Nimegundua baada ya Magufuli kufariki,Majaliwa anaonekana kama kikwazo kwenye furaha ya Upinzani, hasa ukizingatia Majaliwa yupo kwenye nafasi nyeti sana kiserikali.
 
Natena wiza

JF-Expert Member
Mar 13, 2021
322
500
Katiba hairuhusu yote uliyoorodhesha.

Lazima Rais mpya avunje baraza la mawaziri.Ateuwe upya na awaapishe yeye km mteuaji.

Lazima Rais mpya ateuwe Waziri Mkuu mpya na Waziri Mkuu huyo ale kiapo mbele ya Rais.

Kikatiba hakuna kwamba nitaendelea na Hawa hawa. Lazima Waziri mkuu na baraza la mawaziri aliteuwe na liape mbele yake km Rais.
Maelezo yako yatabaki kuwa batili kwasababu Katiba imetaka hayo yafanyike endapo tu, Rais amepatikana kwa njia ya uchaguzi.
 
SAGAI GALGANO

JF-Expert Member
Nov 13, 2009
28,407
2,000
Mimi namkubali toka kipindi kile alivyoweka msimamo juu ya zile container za Makonda,kuwa kama zingetolewa bila kulipiwa ushuru angejiuzulu uwaziri. Makonda alinywea hadi msambwanda wake licha ya mikwala ya kwenda kwa Rais, hebu tujikumbushe kidogo
 
Mkirindi

JF-Expert Member
Mar 2, 2011
6,435
2,000
Uzi huu unakaribia sana na ukweli, Hao waliotajwa ni kweli hawaendani na Uongozi wa Mama na Mpango. Pia nionavyo ndio mwisho wa mawaziri wengi, katika mawaziri wanawake waliopo nadhani kuna kama watatu watakosa nafasi au kutumbuliwa , Gwajima, Ndalichako, UMMY na Jenista Mhagama.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom