Baada ya ushindi wa CDM Arumeru awamu inayofuata iwe L. Lusinde

Losambo

JF-Expert Member
Nov 8, 2011
2,612
864
Updates:

WanaJF tayari offically CDM wameshachukua jimbo, nashauri wanasheria watujuze ni charges gani ambayo Lusinde anaweza kuchukuliwa ili kila mtu ajue?

Nina uchungu sana na Lusinde wakuu.

WanaJF kama hali ikiwa hivi, ni wazi ushindi upo mlangoni mwa CDM. Anyway hiyo ndiyo siasa na asiyekubali kushindwa si mshindani. Lakini napenda niwakumbushe kitu kimoja kuwa kama kuna mtu aliyedhalilisha viongozi wa CDM hasa wa ngazi za juu, kati na chini basi ni mbunge wa Mtera Mh. L. Lusinde.

Napenda kutoa wito, huyu jamaa asiachwe hivi hivi. Ashungulikiwe ipasavyo kwa kuburuzwa mahakamani ili iwe fundisho kwa wabunge wasio na stara katika kampeni.

Hivyo wanasheria wa CDM, wanaharakati mbali mbali, na makundi yote ya kijamii kwa hili la Lusinde tusimfumbie macho wakuu.

Kwa kweli ametukana matusi mbele ya watoto, watu wazima ambayo ni kinyume na maadili ya uchaguzi, mtanzania n,k

Najua mpo katika hekaheka za kujua nani mshindi lakini kitendawili kipo tayari kutegeuliwa.

Nawakilisha.
 
Ngoja mkuu tushangilie ushindi..yule mshenzi tunamshughulikia vyema.

Ni mtu hatari sana, ni imani yangu alitumwa kuja kutukana huku Arumeru na CCM. Wana Arumeru watakuwa wameshamwadhibu kwa kumnyima mgombea wake na lilibaki la kwetu amfuate Lema ili akaone jela ilivyo kama kuna kutafutiana naniiii
 
Thats real Kamanda huyu jamaa lazima apandishwe kizimbani haiingii akilini mtu kama huyu tena anawakilisha wananchi wa jimbo lake na pia ni mtunga sheria lakini kwa kampeini hizi mtunga sheria kachakachua sheria lazima kieleweke.Hapa lazima sheri ichukue hatua yake japokuwa Bongo hakuna haki but atleast hata majaji wameona na kusikia kupitia news na kuhadisiwa so its my hope that wakati ukifika basi atasomewa mashitaka moja kwa moja.
 
Yupo leba amejifungua mtoto anayeitwa Nassari

Lakini jamaa alitukana sana na ndiyo maana hata wanaCCM wenyewe wamelegea kwa matusi yale. Tuanze kwa kutoa siku saba ili CCM itoe tamko rasmi juu ya Lusinde wakishindwa tujue cha kufanya.
 
Thats real Kamanda huyu jamaa lazima apandishwe kizimbani haiingii akilini mtu kama huyu tena anawakilisha wananchi wa jimbo lake na pia ni mtunga sheria lakini kwa kampeini hizi mtunga sheria kachakachua sheria lazima kieleweke.Hapa lazima sheri ichukue hatua yake japokuwa Bongo hakuna haki but atleast hata majaji wameona na kusikia kupitia news na kuhadisiwa so its my hope that wakati ukifika basi atasomewa mashitaka moja kwa moja.

Naunga mkono hoja.
 
Hebu wanasheria watuambie kuna sheria imevunjwa na Lusinde? Ana kesi ya kujibu kwa matusi ailiyotoa pale jukwaani? Kama hamna, basi sheria ya umma itumike kumhukumu 2015,ile video wapelekewe wananchi wake kule Mtera
 
Raisi kama anapenda chama chake amwachishe ubunge huyu mbunge matusi. Iwe fundisho kwa wengine kutoongea kwa kudharau wananchi.
 
Hebu wanasheria watuambie kuna sheria imevunjwa na Lusinde? Ana kesi ya kujibu kwa matusi ailiyotoa pale jukwaani? Kama hamna, basi sheria ya umma itumike kumhukumu 2015,ile video wapelekewe wananchi wake kule Mtera

Mkuu ana kesi ya kujibu badala ya kunadi sera amekashfu watu binafsi akiwemo Dr. Slaa, Mbowe, wapenzi na wanachama wa CDM. Makosa yapo mengi kwa wanasheria wanajua hilo.
 
Hebu wanasheria watuambie kuna sheria imevunjwa na Lusinde? Ana kesi ya kujibu kwa matusi ailiyotoa pale jukwaani? Kama hamna, basi sheria ya umma itumike kumhukumu 2015,ile video wapelekewe wananchi wake kule Mtera

huyu jamaa kajidharirisha sana hata kama hana elimu asingefanya utumbo wote huo,, kweli hawa ndio vijana wa CCM walioandaliwa vema kuongoza watanzania? mimi ningeambiwa nisingeamini ila kwa kuwa nimeona basi naamini kuwa mfumo wa kuwapata wabunge sio sahihi maana wengine hata hawafai kuwa baba wa familia. Lusinde umejianika kiasi gani usivyo na hekima na busara.. kweli ukubwa wa pua sio wingi wa makamasi...
 
Mbunge mteule wakati wa kutoa neno la shukrani, ampeleekee salamu kuwa wakati wa ku-deal naye umefika.
 
Yaani huyo lusinde katafuta umaarufu vibaya. Angekuwa anatoa hoja bungeni tungemfahamu ila kaja kwa style siyo.
 
Back
Top Bottom