Baada ya upinzani kuonesha kusitasita, watanzania wanaitazama Lumumba kama sehemu pekee ya kuwekeza kwa Tanzania ya kesho

KARLO MWILAPWA

JF-Expert Member
Apr 10, 2019
2,589
4,600
Licha ya sababu mbalimbali za kiuchumi na kisiasa zilizofanya nchi yetu kuanzisha mfumo wa vyama vingi mwaka 1992 na uchaguzi wa kwanza kufanyika 1995 lakini bado CCM ni tumaini pekee la watanzania. Kuanzia uchaguzi wa 1995 mpaka wa mwaka 2015, CCM imekuwa ikishinda na ushindi wa kishindo unaokumbukwa ni ule wa 2005 uliomuingiza Mhe. Kikwete madarakani licha ya ushindani, CCM ilishinda kwa 80.5% ya kura zote.

Kila uchaguzi CCM unashinda na kwakweli ni jambo la kujivunia kwamba bado Imani na matumaini ya watanzania kwa CCM ni makubwa, kuendelea kuaminika kuzitumia rasilimali za taifa kwa maendeleo ya nchi si jambo la kutilia shaka uwezo wa CCM na Imani ya watu kwa CCM. Tumejenga Imani hii toka vizazi, tangu mapambano ya kudai uhuru chini ya TANU mpaka Tanganyika huru na hatimaye Tanzania. Tumeshuhudia tawala nyingi zinazokaa madarakani kwa miongo zaidi ya mitatu hugeuka tawala za mabavu na damu lakini mtazamo huu ni kinyume na CCM ambayo kwa kipindi chote kimesimamia utawala wa haki na sheria .

Lengo la mfumo wa vyama vingi ni kuwa na vyama mbadala wa kilichopo madarakani lakini kwa zaidi ya miaka 25 sasa vyama vya upinzani vimekosa sifa ya kuitwa mbadala na vimeonesha kusitasita katika nia na dhamira ya kuwa mbadala. Kusitasita huko kwa upinzani kumeonekana baada ya kuonesha utata wa utekelezaji wa majukumu yake kama chama na kupelekea kukombiwa na wanachama wake ambao ni nguzo kubwa katika ustawi wa chama.

Ikumbukwe mwaka 2017 aliyekuwa mwenyekiti wa ACT na mgombea wa chama hicho kwa nafasi ya urais Mama Anna Mghwira aliachana na chama chake na kujiunga na CCM na alikilalamikia chama chake chake cha zamani kwa kusitasita katika utekelezaji wa majukumu yake. Kusitasita huko kukaingia CHADEMA na kupelekea aliyekuwa mgombea wa urais kupitia chama hicho Edward Lowassa kuondoka na kujiunga na CCM mwaka 2019.

Baada ya wanachama hao ambao ni muhimu katika vyama vyao kwa nafasi na majukumu yao kukimbia vyama vyao na kujiunga na CCM kumeonesha dhahiri ni kwa namna gani CCM inavyoaminika kwa watu wote, ni jinsi gani CCM inavyoaminika na ilivyobeba matarajio na matumaini makubwa ya watanzania na hii inatoa picha na tafsiri kwamba watanzania wanaitazama Lumumba kama sehemu pekee ya kuwekeza kwa Tanzania ya kesho kisiasa na kiuongozi.

Tanzania ni yetu sote
 
Back
Top Bottom