Baada ya ukweli kuhusu sakata la Bernard Morrison 'Kuvuja', huenda Yanga SC 'ikanyang'anywa' alama zake na viongozi wake kufungwa na kukamatwa

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
40,149
2,000
Taarifa nilizozipata kutoka katika Chanzo changu 'Nyeti' zinasema kwamba kilichogundulika juu ya Sakata zima la Mchezaji Bernard Morrison ni kwamba Klabu ya Yanga 'imedanganya' kuhusu 'Mkataba' wake na kwamba hata 'Sahihi' yake pia 'imefojiwa' kinyume na Sheria. Ukweli kamili wa hili upo njiani kutolewa kwa Watanzania ili 'Wahuni' na 'Matapeli' wa Soka la Tanzania wajulikane na waumbuke rasmi.

Chanzo changu hicho Kimeendelea kusema kwamba sehemu ambayo Yanga SC 'imejikoroga' ni katika Tarehe ya Mkataba wa Mchezaji Bernard Morrison ambapo Yanga SC 'wamedanganya' Umma kuwa 'alisajiliwa' tarehe 15 na Kuuwasilisha TFF wakati Mchezaji aliwasili nchini tarehe 17 na hata Mawasiliano yake ya Email yana Ukweli wote pamoja na Tiketi yake ya Ndege.

Hivyo basi 'Adhabu' ambayo huenda Yanga SC 'ikakumbana' nayo katika 'Hukumu' inayoenda 'Kutolewa' leo ni ama 'Kunyang'anywa' Alama ( Points ), Kupigwa Faini Kubwa, Kuzuiwa Kufanya Usajili, Kushushwa Daraja, Viongozi wake Kukamatwa, Kushtakiwa na Kufungiwa kabisa. Na kama TFF wakisema walipeleke hili 'Suala' huko FIFA kuna uwezekano Klabu ya Yanga 'ikafutwa' katika ramani.

Chanzo hicho kimemalizia kwa kunielezea kuwa kumbe baada ya Uongozi wa Yanga SC hasa kupitia 'Wadhamini' wao GSM kuona kwamba wanaenda 'Kuumbuka' walienda Kutoa 'Rushwa' ya Tsh Milioni 20 TFF ili hili 'Suala' lisiende mbali lakini Uongozi Imara na wenye 'Uweledi' wa TFF ukakataa huo 'Upuuzi' na kuwaambia Yanga SC hili 'Suala' lazima lifike mwisho ili liwe Fundisho nchini.

Baada ya Yanga SC na GSM kujua kuwa 'wameshalikoroga' na Mashabiki wao hawatawaelewa wameamua 'Kuwahadaa' kwa Kufanya 'Usajili' wa aliyekuwa CEO wa Simba SC Senzo Mbatha Mazingisa huku 'wakiwadanganya' kuwa 'wanamsajili' Mchezaji Clatous Chama na akina Deo Kanda. Hii yote Yanga SC wanafanya kama kutafuta 'Huruma' kwa Mashabiki na Wanachama Wao.

Namalizia kwa kusema 'sijakulazimisha' ukubaliane na nilichokiwasilisha hapa ila Yanga SC jana walifurahi lakini leo watalia sana na Moto utawaka.
 

Cvez

JF-Expert Member
May 19, 2018
1,546
2,000
Wiki iliyopita na wiki hii ni tamu sana .... Kama mzani unapanda huku unashuka kule
 

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
40,149
2,000
Haaf Viongoz Wa Simba Waache Kutuletea Watendaji Kutoka Nje, Coz Hawa Wanaangalia Masrah Tu Hawana Mapenzi Na Timu, Hivi Unafikiri Kama Ceo Wa Simba Angekua Labda Mwina Kaduguda Ama Try Again Hatakama Angejiuzulu Asingehamia Yanga, Maana Anajulikana Ni Simba Damu.

Unapotafuta 'Mtaalam' si lazima sana hadi umpate Mtu mwenye Usimba mwingi kama tulivyo Mimi na Wewe Mkuu. Dunia imebadilika sana Mkuu!!!
 

mtu chake

JF-Expert Member
Aug 20, 2010
21,527
2,000
Tanzania Simba na Yanga hata ziboronge vipi haziwezi kupewa adhabu eti ya kushushwa daraja.

Hata kama ingekuwa ligi ni MTOANI, Simba na Yanga zitabebwa bebwa zusitoke.

Magazeti yenyewe kila siku front pages ni Simba au Yanga, bila hivyo hayauzi


Ile ni biashara ya WATU.
Nakubaliana na wewe Mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 

mwanateknolojia

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
805
1,000
Yanga wakuabali tu na kuomba radhi kwa Morrisoni yaishe! Jamaa alishachomoa betry siku nyingi wao wamemng'ang'ania, sasa wataumbuka zaidi! Suala la kumuajiri Senzo halina mashiko, na wala haliwezi kuitikisa Simba labda Mo Dewji angehamia huko ningesema sawa! Lakini huyo wa kuajiriwa na kulipwa mshahara hana tofauti na kocha au mchezaji wa klabu!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom