Bilionea Asigwa
JF-Expert Member
- Sep 21, 2011
- 16,515
- 28,487
WAZIRI Mkuu wa Norway, Erna Solberg amemuomba Waziri Mkuu Kassim, Majaliwa ahakikishe Tanzania inatuma wawakilishi wa Serikali kwenye mkutano wa uwekezaji, unaopanga kujadili fursa za uwekezaji barani Afrika utakaofanyika jijini Oslo, Norway, Oktoba mwaka huu ambapo focus kubwa itakuwa Tanzania.
Waziri Mkuu wa Norway alisema mkutano huo umeandaliwa na taasisi binafsi ya Norway Africa Business Association (NABA) na kwamba anazo taarifa kuwa utalenga kujadili fursa za uwekezaji barani, lakini ‘focus’ ikiwa ni Tanzania.
“Ni vyema Tanzania ikatuma wawakilishi kwenye mkutano ili waje kuelezea fursa zilizoko nyumbani. Serikali ilete watu wa kuja kuelezea hali halisi ikoje nchini Tanzania,” alisema.
Alisema ili fursa za uwekezaji ziweze kutumika ipasavyo, ni vyema Tanzania ikawa na mfumo wa kimahakama unaotoa haki bila upendeleo (a fair judicial system), kwani utasaidia kujenga hali ya kujiamini kwa wafanyabiashara wanaokuja kuwekeza Tanzania.
“Mfumo huu utaleta hamasa kwa wawekezaji, kwani watajua kwamba mitaji yao iko salama na inalindwa kisheria, hivyo hawatakuwa na hofu,” alisema. “Hata hivyo, napenda kusisitiza kuwa makampuni yanayotoka nje na kuja kuwekeza Tanzania hayana budi kuheshimu sheria za nchi yenu pamoja na za huku wanakotoka,” alisisitiza.
Solberg ametoa kauli hiyo juzi alipokutana na Waziri Mkuu Majaliwa na kufanya naye mazungumzo ya ana kwa ana kwenye mkutano wa siku moja wa Wakuu wa Nchi ulioitishwa kujadili suala la kupambana na rushwa duniani.
Source: Habari Leo