Baada ya uhuru watanzania weng leo tuko chini ya ukoloni wa kifikra(kisaikolojia) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Baada ya uhuru watanzania weng leo tuko chini ya ukoloni wa kifikra(kisaikolojia)

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Salary Slip, Jun 26, 2012.

 1. S

  Salary Slip JF-Expert Member

  #1
  Jun 26, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 25,034
  Likes Received: 37,811
  Trophy Points: 280
  Watanzani tulidai uhuru kutoka kwa wakoloni wa kizungu ili tuache kunyonywa na kukandamizwa.Sasa mtanzania mwenzangu hebu jiulize ktk hayo kweli tumefanikiwa?Hivi watu wanaotuibia kama mafisadi kwa kupora maliasili zetu,kuuza ardhi yetu n.k na kujinufaisha wao na ndugu ama jamaa zao wanatofauti gani na jinsi mzungu mkoloni alivyokuwa akijinufaishi na maliasili zetu?
  Wazungu walituchapa viboka bila kosa la msingi!Leo hii watu wakiandamana watapigwa na polisi na kudhalilishwa!Sasa hapa tofauti ya kiboko cha mzungu mkoloni na cha mtu mweusi kwa waandamanaji wasio na silaha tena kwa amani kiko wapi?
  Mkoloni alitubagua kwa naamna mbalimbali kuanzia shuleni,kwenye vyombo vya usafiri na hata ktk maeneo ya kuishi.Swali leo hii hatujibagui wenyewe kwa kuwa na wale walio nacho na wale wasio nacho?Maskini na tajiri leo wanasoma shule moja?wanaishi sehemu moja na hata wanakula pamoja?Mifano ni mingi mno.
  Tukija kwenye mada yenyewe watanzania hilo wanalitambua?Na kama wanalitambua mbona kila siku watawala ni wale wale na wanawachagua wenyewe?Kwenye mikutano yao ya kampeni mbona wanajazana na kuwashangilia na kuwashududia kama miungu watu?Alafu kila kukicha wanalia na maisha magumu!
  Najua kuna watu watakuja na hoja kwamba watanzania wengi hawana elimu ya uraia.Swali langu ni jee kumchukia na kumkataa mkoloni kulitokana na elimu ya uraia kwa watanzania wakati wa ukoloni?
  Jibu ni moja tu kwamba watawala wa leo wamefanikiwa sana kututawala kifikra(kisaikolojia) kuliko mkoloni na ndio maana kila siku watawala ni wale wale licha ya dhuluma zote wanazozifanya na wanazoendelea kuzifanya.Watanzania wengi leo imani yao iko kwa hawa watawala na wanaona ni bora waendelee kutawala licha ya uovu wao na wengi hawaamini kuwa nchii hii iaweza kuongozwa na chama kingine.Wako tayari kufa na tai shingoni.
  Hakika tutakuja kulaumiwa na vizazi vijavyo kwa kutokuchukua hatua.Watanzania wa leo ndio wajenzi wa msingi wa nyumba ya kizazi kijacho ila hata hivyo ni bahati mbaya hatutimizi wajibu wetu wa kuwaandalia msingi mzuri na badala yake tunawaachia urithi mbaya kwa mfano mashimo marefu na uharibifu wa mazingira baada ya rasilimali za madini kuporwa na wachache n.k.
   
 2. S

  Salary Slip JF-Expert Member

  #2
  Jun 26, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 25,034
  Likes Received: 37,811
  Trophy Points: 280
  Kazi ipo.
   
 3. Gwankaja Gwakilingo

  Gwankaja Gwakilingo JF-Expert Member

  #3
  Jun 26, 2012
  Joined: Jan 26, 2012
  Messages: 1,963
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  ni heri kupambana na mkoloni mweupe (mwingereza) kuliko kupambana na mkoloni mweusi ccm
   
 4. S

  Salary Slip JF-Expert Member

  #4
  Jun 27, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 25,034
  Likes Received: 37,811
  Trophy Points: 280
  Message sent.
   
Loading...