Baada ya uhakiki wa vyeti sasa tuanze kuwa na viwango vya ISO Serikalini...

FaizaFoxy

JF-Expert Member
Apr 13, 2011
71,266
2,000
Zoezi la uhakiki wa vyeti feki na wafanyakazi hewa lilikuwa la maana sana na umuhmu wa kipekee kwa kuongeza ufanisi, lakini halitoshi.

Ili kuboresha ufanisi na utendaji, uwajibikaji, na huduma kws jamii ni wakati muafaka sasa serikali ianze kupima kila shirika la umma, idara zote za serikali, wizara na taasisi zote za serikali kwa viwango vya kimataifa viijulikanavyo kama ISO.

Bila hivyo hakuna mwenye kuelewa anafata vigezo vipi vya ufanisi anapoteuliwa au kupata kazi kwenye sehemu tajwa.

Serikali itaendelea kutafuta wachawi mpaka dahari ikiwa watumishi wake hawana standard ya kuifata.

Hii ianze kwa mawaziri mpaka chini kabisa huko kwa watendaji wa mitaa.

Ushauri muhimu huu kwa serikali inayotaka matunda yake yajioneshe yenyewe bila kupigiwa debe.
 
mirisho pm

JF-Expert Member
Apr 10, 2012
3,525
2,000
Wazo zuri lakini ni next to impossible. ..
Hakuna sehem inayoajiri vilaza kama serikalini. ..
Ukiacha Hilo bado kuna uhaba na ubavu wa miundombinu ukiachilia mbali "maagizo hovyo kutoka juu"
Ufanisi wa ISO huwezi kupata kwenye mazingira hayo
 
chugamaica

JF-Expert Member
Dec 17, 2018
221
250
Hakuna "serikali ya kamataifa" bali kuna viwango vya kimataifa na huu ni ushauri.
Wanamichezo wenyewe niwakimataifa sembuse serikali! Waziri wa mambo ya nnje kazi yake ni nini? hizi balozi zetu zinaenda kufanya nini? ikiwa wewe ni mwanachama wa umoja wa Mataifa na ukaingia kusaini masheri yakimataifa na mataifa mengine wewe ni wakimataifa tu.ila mzee baba siyo wakimataifa hataki kuwa na mabeberu hataki. Ikiwa wewe unashirikiana ma mataifa mengine katika uchumi, siasa na mambo mengine ya kijamii wewe ni wakimataifa na hata na nchi wahisani /wazee wakuonea huruma wenye shida ndiyo maana ya neno "hisani" kule kwetu tunawaita (mabeberu ).

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Gagnija

JF-Expert Member
Apr 28, 2006
8,581
2,000
Zoezi la uhakiki wa vyeti feki na wafanyakazi hewa lilikuwa la maana sana na umuhmu wa kipekee kwa kuongeza ufanisi, lakini halitoshi.

Ili kuboresha ufanisi na utendaji, uwajibikaji, na huduma kws jamii ni wakati muafaka sasa serikali ianze kupima kila shirika la umma, idara zote za serikali, wizara na taasisi zote za serikali kwa viwango vya kimataifa viijulikanavyo kama ISO.

Bila hivyo hakuna mwenye kuelewa anafata vigezo vipi vya ufanisi anapoteuliwa au kupata kazi kwenye sehemu tajwa.

Serikali itaendelea kutafuta wachawi mpaka dahari ikiwa watumishi wake hawana standard ya kuifata.

Hii ianze kwa mawaziri mpaka chini kabisa huko kwa watendaji wa mitaa.

Ushauri muhimu huu kwa serikali inayotaka matunda yake yajioneshe yenyewe bila kupigiwa debe.
Anza kwenye kampuni yako ya makasha.
 
Hayo yote ni katika uhusiano wa Kimataifa lakini si serikali ya Kimataifa.

Tujikite kwenye ufanisi.
 
FaizaFoxy

JF-Expert Member
Apr 13, 2011
71,266
2,000
Kama taasisi zinavyoshindana kuwa na banda bora sabasaba au nanenae basi ni wakati muafaka ziishindanishwe kuwa na ufanisi bora wenye viwango vya kimataifa.
 
FaizaFoxy

JF-Expert Member
Apr 13, 2011
71,266
2,000
... naam; jukumu namba moja la Serikali yoyote ni usalama, amani, na haki sawa kwa wananchi wote! Hii ikikaa sawa, automatically vingine vitaji-set tu. ISO namba moja ni utawala wa Katiba na Sheria!
Bila kuwa na viwango vinavyopimika utaupataje huo ubora? Fikiri.
 
MTAZAMO

JF-Expert Member
Feb 8, 2011
16,149
2,000
Zoezi la uhakiki wa vyeti feki na wafanyakazi hewa lilikuwa la maana sana na umuhmu wa kipekee kwa kuongeza ufanisi, lakini halitoshi.

Ili kuboresha ufanisi na utendaji, uwajibikaji, na huduma kws jamii ni wakati muafaka sasa serikali ianze kupima kila shirika la umma, idara zote za serikali, wizara na taasisi zote za serikali kwa viwango vya kimataifa viijulikanavyo kama ISO.

Bila hivyo hakuna mwenye kuelewa anafata vigezo vipi vya ufanisi anapoteuliwa au kupata kazi kwenye sehemu tajwa.

Serikali itaendelea kutafuta wachawi mpaka dahari ikiwa watumishi wake hawana standard ya kuifata.

Hii ianze kwa mawaziri mpaka chini kabisa huko kwa watendaji wa mitaa.

Ushauri muhimu huu kwa serikali inayotaka matunda yake yajioneshe yenyewe bila kupigiwa debe.
Wazo zuri sana. Nafikiri waweke mpango mkakati wa miaka 5 kuelekea kwenye total compliance.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jurrasic Park

JF-Expert Member
Sep 13, 2013
3,754
2,000
Sasa kama keshasema serikali yake yeye ndo mwenye hati miliki hilo halisezekani. Jiwe anataka sifa tuu zimuendee yeye peke yake. Badala ya kuunda taasisi imara yeye anataka sifa tuuu

Vyeti vya sasa hivi vina QR code na vina mfumo mzuri labda iyo ISO inahusu mashirika ya kimataifa sio hizi drama drama za jiwe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
TIBIM

JF-Expert Member
Dec 1, 2017
8,022
2,000
Hakuna "serikali ya kamataifa" bali kuna viwango vya kimataifa na huu ni ushauri.
Ni
Hio ni ndoto kama tu stahiki zao awapewi hio motisa itoke wapi.Tofautisha tija na uwoga makazini.Kilichopo ni uoga na uoga sio tija wala nidhamu. Vyeti sio tija,tija ni utashi ndio maana mliowaondoa kosa vyeti wako nje nchi na private sector wanafanya tija nzuri tu tena kwa maslai bora zaidi hadi wengine wanashukuru walikuwa wakipoteza mda.Vyeti havikai darasani bali MTU idadi ya madereva vyeti wanaoongoza kwa kusababisha Ajali za kila mara tofauti na ya kabla awajaondolewa unawasemaje.Kilichotakiwa ni kuondoa wafanyakazi hewa wenye matatizo ya vyeti wangeachwa hadi wastaafu had waishe wenyewe ni umakini tu kwenye ajira mpya ili makosa yasijirudie.Unaondoa mfanyakazi mwenye tija tena Mtaalamu say daktari bingwa,MWALIMU anaewaulisha ,engineer nk kisa kasoro ya cheti alichokipata Miaka 20 iliyopita unaacha kuangalia utaalamu wake.
 
FaizaFoxy

JF-Expert Member
Apr 13, 2011
71,266
2,000
Sasa kama keshasema serikali yake yeye ndo mwenye hati miliki hilo halisezekani. Jiwe anataka sifa tuu zimuendee yeye peke yake. Badala ya kuunda taasisi imara yeye anataka sifa tuuu

Vyeti vya sasa hivi vina QR code na vina mfumo mzuri labda iyo ISO inahusu mashirika ya kimataifa sio hizi drama drama za jiwe

Sent using Jamii Forums mobile app
Tunaongea vitu viwili tofauti. Mimi naongelea ufanisi wewe unaongelea siasa. Siasa Tanzania ni mfu, tujikite kwenye huduma kwa jamii.

Unafikiri zoezi la uhakiki wa vyeti na wafanyakazi hewa lilikuwa la kisiasa?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom