Baada ya uchaguzi Zanzibar sasa kazi tu

singidadodoma

JF-Expert Member
Nov 11, 2013
4,394
1,536
UCHAGUZI wa marudio Zanzibar umefanyika kwa amani na utulivu wa hali ya juu hadi kufikia hatua ya kutangazwa mshindi katika uchaguzi huo, Dk Ali Mohmmed Shein wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kupata kura 299,982 sawa na asilimia 91.4.

Akitangaza matokeo hayo, Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Jecha Said Jecha alisema idadi ya wapiga kura waliojiandikisha ni 503,580 na waliojitokeza kupiga kura juzi ni 341,865, idadi ambayo ni sawa na asilimia 67.9 ya watu wote waliojiandikisha. Kura zilizoharibika kwenye uchaguzi huo zilikuwa 13,538 sawa na asilimia 4.0.

Tunapenda kumpongeza Dk Shein kwa kupata ushindi huo wa kishindo. Lakini, pia pongezi maalumu ziende kwa vyama vyote vilivyoshiriki katika uchaguzi huo kwa amani na utulivu, licha ya baadhi ya vyama kuamua kwa hiari yao kutoshiki.

Hiyo ndiyo demokrasia. Penye ushindani lazima apatikane mshindi. Vyama vingine vilivyoshiriki uchaguzi huo ni pamoja na ADA Tadea, ADC, AFP, CCK, DP, SAU na TLP. Tunampongeza Rais mteule Dk Shein kwa kauli yake aliyotoa baada ya kutangazwa mshindi na kupokea cheti cha ushindi huo.

Kauli yake hiyo ni ya kizalendo na ya kutia moyo kwa mustakabali wa maisha yenye ustawi kwa Wazanzibari wote. Shein ameahidi kutenda haki kwa kila Mzanzibari na kwamba hatamdhulumu mtu yeyote haki yake.

Amesema atahakikisha Zanzibar inapaa kimaendeleo kwa kukuza uchumi kufikia kati ya asilimia 8 hadi 10 katika miaka mitano ijayo. Alitamka wazi pia changamoto ya kazi hiyo inayomkabili katika kipindi cha miaka mitano ijayo na kwamba yuko tayari kutumika tena kwa uaminifu na kwa watu wote, bila kujali itikadi zao za kisiasa.

Katika hotuba yake, pia Dk Shein hakufumbia macho mgogoro wa kisiasa uliopo Zanzibar na kuahidi kuushughulikia kwa kuwaomba wananchi wote wampe ushirikiano katika hili, kwani yeye peke yake si rahisi kuweza kuukabili vilivyo hadi kupata muafaka kwa manufaa ya Wazanzibari wote.

Hapa tungependa kutoa rai kwamba hakuna ubishi tena kuwa hatua hiyo ya kurudia uchaguzi na kupatikana kwa washindi, kumekamilisha kazi iliyobaki baada ya uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 25, mwaka jana sambamba na uchaguzi mkuu wa Tanzania Bara, kufutwa kutokana na matatizo ya ukiukwaji wa taratibu.

Kupatikana kwa Rais wa Zanzibar ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, wawakilishi na madiwani ni ushindi tosha kwa Wazanzibari wote na kinachobaki sasa ni kuchapa kazi.

Huu ni wakati muafaka sasa wa kujikita katika kuimarisha shughuli za kiuchumi kwa kufanya kazi kwa bidii na kwa kushirikiana bila kujali itikadi zetu za kisiasa, kwani maendeleo hayana itikadi.

Wakati mgogoro wa kisiasa utaendelea kushughulikiwa na viongozi wetu, wananchi wajikite katika shughuli za uzalishaji mali na kiuchumi ili kujikwamua kutoka katika umasikini na kujenga jamii yenye ustawi sawia wa kiuchumi, kisiasa na kiutamaduni. Tuhakikishe kudumisha amani, utulivu na mshikamano ili kufikia uchumi wa kati tunaousaka.
 
labda kazi ya fitna.

sisi tutaendelea kuitangaza Tanzania kama wabakaji wakuu wa demokrasia.
1458587327227-jpg.331606
 
Mtu kushinda kwa asilimia zaidi ya 90 ni dalili kwamba uchaguzi ulikua sio wa haki. Kutoka kwenye kushindwa mara ya kwanza hadi kupata asilimia 97 sasa hivi ni kichekesho kwa kweli...hapa demokrasia imebakwa
 
Eti pemba wapiga kura uwakilishi na udiwani walifika elf 5 hadi 6 kwenye vituo vingi vya kupiga kur na kufanya CCM ipate kura sooo+ na vyama vingine kugawana kura 100 tu. Kwa misururu ipi?
 
Back
Top Bottom