Baada ya Uchaguzi: tamu na chungu ya Tanzania

Uliza_Bei

JF-Expert Member
Feb 17, 2011
3,216
988
Kwa ufupi tumeiona kwa mwelekeo huu Zanzibar Maalim ameongoza lakini huenda akatangazwa Mwinyi (CCM itashangilia na ACT wazalendo na kambi ya upinzani watabaki wenye huzuni).

Upande wa Madiwani na Wabunge hali inaonyesha asilimia 98% watatoka CCM bila kujali walipita bila kupingwa, wameshinda au wametangazwa kibabe. Tamu itakuwa shamrashamra na bashasha za Chama tawala wakijimwambafai kwa ushindi bila kujali nani ameumizwa kufikia hapo. Chungu ni kuwa kambi ya upinzani itaendelea kulia, kuhuzunika na kulalamika ndani na nje ya nchi.

Chungu hii itamwagika na kuathiri hasi (negative effect) kwa serikali ya Zanzibar na ile ya Muungano ya Tanzania kwa miaka yote mitano ijayo 2020-2025 kiasi cha kuharibu mipango ya maendeleo kwa kiasi kikubwa nchini.

Tamu kwa sababu serikali itakuwa huru bila kuhojiwa na hata bunge litakuwa la kupitisha na kujibu "ndiyooooo" bila hoja mbadala.

Chungu kwasababu wananchi hawatakuwa na wawakilishi wa kuwasemea shida zao. Tamu kwa CCM miaka 5 na chungu kwa kambi ya wananchi na upinzani miaka 5. Huenda ikawa tiketi ya CCM kuondoka madarakani baada ya kuwa wananchi wamejilaumu kwa miaka 5 wakipitia machungu.

Ninatabiri kwa miaka 5 Watanzania wote tutakuwa wapinzani wa serikali maana kambi ya upinzani ya kisiasa itakuwa haipo. Tujiandae kwa hayo.
 
Hahaha tuache kujidanganya kuanzia sasa hakuna uchaguzi, tukimchoa mbunge tumroge afe tupate mwingine mpaka tumpate tumpendaye.
 
Maendeleo hayana chama, unga mkono juhudi, tusonge mbele. Kwani ili uendelee lazima upate wa kukupinga?. Nani anayekupinga ili kufanikisha mipango ya familiya yako?
 
Watu wameona isiwe tabu, mtu umepigwa risasi na bado hujapona vizuri halafu tena tukuongezee majukumu ya Urais, ni afadhali tukuonee huruma kwa kumpa kura Magufuli ili ukatibiwe vizuri
 
Maendeleo hayana chama, unga mkono juhudi, tusonge mbele. Kwani ili uendelee lazima upate wa kukupinga?. Nani anayekupinga ili kufanikisha mipango ya familiya yako?
Tutaongea mkono juhudi lakini tutegemee hayo
 
Watu wameona isiwe tabu, mtu umepigwa risasi na bado hujapona vizuri halafu tena tukuongezee majukumu ya urais, ni afadhali tukuonee huruma kwa kumpa kura magufuli ili ukatibiwe vizuri
Lakini wote tutakumbana na negative effect na yeye atakuwa anapambana na hali yake
 
uchaguzi wa ajabu sana huu,litakuwa bunge la kula bata tu,bunge butu kuwahi kutokea,halitakuwa na nguvu za kuikoromea serikali
 
Maendeleo hayana chama, unga mkono juhudi, tusonge mbele. Kwani ili uendelee lazima upate wa kukupinga?. Nani anayekupinga ili kufanikisha mipango ya familiya yako?
Umoja wa taifa ni zaidi ya maendeleo, Hitla alifanya maendeleo makubwa kwa taifa lake, ila dunia daima itajuta kwa kiumbe huyo kuwahi kuishi.
Mnafeli wapi hata msiige mazuri kwa jirani BBI.
 
Back
Top Bottom