Baada ya Uchaguzi Mkuu tujiandae kushuhudia mnyukano CHADEMA

maramia

JF-Expert Member
Jul 17, 2015
1,987
2,000
mleta mada inakua anaandikia mochwari mana inaonekana akili zake zimepulizwa n baridi y jokofu l kuhifadhia maiti......ccm kuanzia kesho lazma wavae bikini tu nepi,kinana,mwigulu,bulembo,lusinde wamekula hela za kampeni wanashikana uchawi sasa......majambazi na wanaondoka kuanzia kesho

Pole sana, baada ya matokeo yote kutangazwa wewe ndo utawekwa kwenye jokofu la maiti.
Kubali ninachokuambia Chadema itaishia atakapoanzia Magufuli.
 
peace2007

JF-Expert Member
Oct 9, 2007
213
195
Naamini baada tu ya kutangazwa matokeo ya Rais na wabunge, na CCM kuibuka na ushindi wa 62% kwa nafasi za ubunge na urais kwa 70% Ukawa hawatakuwa tena na nafasi ya hata kufanya tathmini ya kushindwa kwao ila wataanza kunyukana kumtafuta mchawi wa kushindwa kwao.

Naamini pia huo ndio utakuwa mwisho wao kisiasa, na kama nilivyowahi kusema huko nyuma huo ndio utakuwa mwisho wa kitu kinachoitwa Chadema.

Mbowe atanyukwa, Tundu Lissu atasakamwa, Prof Safari, Baregu na Salum Mwalimu wataandamwa mpaka watimke. Lowassa ndio kabisaaa, hakuna atakayetaka kulisikia hata jina lake.

Inatia huruma sana kwa Chadema iliyofikia hatua ya kuaminiwa na mamilioni ya watanzania kufa kifo cha kibudu na cha aibu kiasi hiki.

Watamkumbuka, watamlilia na watajutia matusi waliyomporomoshea Dk Wilbroad Slaa ambaye mpaka leo mimi namwamini, namkubali na ninamuunga mkono. Dk Slaa atabakia mshindi wa kudumu ktk Chadema.

Tukubali tusikubali kesho Chadema itapigwa mweleka ambao haikuwahi kuufikiria na viongozi wake wataparaganyika kuanzia hiyo kesho.

Utabiri wa mvua za El-nino ulisema zinaanza lini.....
 
ngoshwe

JF-Expert Member
Mar 31, 2009
4,134
2,000
Julius S. Mtatiro
9 hrs ?
HATUWEZI KUSHINDA UBUNGE SEGEREA...
Ndugu zangu, kwa moyo mkunjufu kabisa napenda kuwajulisha kuwa hatuwezi tena kushinda ubunge wa jimbo hili kwenye uchaguzi uliofanyika jana.
Matokeo ya majumuisho ya kila kata yanaonesha kuwa mgombea wa Chadema, Bi. Anatropia Theonest ana wastani wa kura 2000 - 2500 kwa kila kata.
Mimi nina wastani wa kura 4000 - 5000 kwa kata na mgombea wa CCM ana wastani wa kura 5000 hadi 6000 kwa kata.
Hii ina maana kuwa kura za UKAWA kama zingelipigwa kwa mgombea halisi wa UKAWA tungeishinda CCM kwa zaidi ya kura 20,000 lakini kwa sababu zimepigwa kwenda vyama viwili tunaweza kushindwa kwa wastani wa kura 5000 hadi 10,000.
Haya yaliyotokea hapa Segerea ni funzo kubwa kwa vyama vyetu na wanasiasa wetu kuheshimu na kusimamia makubaliano, kuwa na roho ya kufikiria mustakabali wa taasisi na watu wetu kuliko MASLAHI BINAFSI. Kwa hatua ya sasa sitaeleza hujuma za ndani kwa ndani tulizofanyiana ndani ya UKAWA hadi kufika hapa.
Nachoweza kusema ni Asante Mungu na asante wana Segerea, asante watu wote waliojitoa kufa na kupona kutusaidia, lakini pia asante kwa wale wote waliotusaliti kimya kimya ili kuchochea mgawanyiko wa kura hizi.
Naahidi kushiriki katika hatua zote za kumsaidia mshindi wa uchaguzi wetu ili atangazwe rasmi kuwa mbunge wa wana Segerea. Mimi nitaendelea na majukumu mengine lukuki ya kulijenga taifa letu.
Kwa sababu yaliyosababisha kukosa ushindi wetu ni mambo ya ndani ya vyama vyetu, sitachukua hatua zozote wala kukata rufaa kwa sababu wananchi hawakutunyima ushindi, tumeugawanya wenyewe.
Nawapongeza madiwani wa UKAWA walioshinda kwenye kata zote 13 za jimbo letu, tulishirikiana na kupambana pamoja hadi kuleta ushindi huu, nawataka wachape kazi kufa na kupona na waisimamie manispaa ya Ilala bila woga, nawaomba wakatumie mipango na ushauri tuliowahi kupanga pamoja ili kuwatendea wana Segerea yale waliyoyatarajia.
Mwisho, nataka kuwaeleza watanzania wote kuwa sina kinyongo na mtu yeyote kwa matokeo haya. Mimi ni kati ya watu wanaoamini kuwa SIASA SI AJIRA...Nitaendelea kuwatumikia watanzania kwa njia zote muhimu nje ya vyombo vya maamuzi.
Nataka kuwaambia wananchi wa Segerea kwamba niko imara sana, sijayumba wala kutetereka, nawapenda sana nyote na poleni na MSHTUKO wa matokeo haya na muda si mrefu tutayaweka hapa.
Ni mimi,
Mtatiro Julius,
Segerea.
 
DE FULE

JF-Expert Member
Jan 10, 2013
1,179
2,000
Wewe unasubiri kura zihesabiwe ndiyo ujue umeshindwa? Wakati Lowassa amewaambia Ukawa muwapigie kura wabunge na madiwani wa CCM na wengi wamemwitikia unafikiri Ukawa mtashindaje?

Ukawa njooni msome hii....
 
DE FULE

JF-Expert Member
Jan 10, 2013
1,179
2,000
Matokeo yakiishatangazwa ndiyo utajua kama mimi ni nabii na ni nani mpumbavu kati yangu na wewe. Just cool down brother Mwinula jnr.

Manabii wengi kweli tena maarufu walitabiri. Kaja kuwin nabii asiyefahamika kabisaaa.....
 
aboos

Member
Dec 15, 2015
39
95
Naamini baada tu ya kutangazwa matokeo ya Rais na wabunge, na CCM kuibuka na ushindi wa 62% kwa nafasi za ubunge na urais kwa 70% Ukawa hawatakuwa tena na nafasi ya hata kufanya tathmini ya kushindwa kwao ila wataanza kunyukana kumtafuta mchawi wa kushindwa kwao.

Naamini pia huo ndio utakuwa mwisho wao kisiasa, na kama nilivyowahi kusema huko nyuma huo ndio utakuwa mwisho wa kitu kinachoitwa Chadema.

Mbowe atanyukwa, Tundu Lissu atasakamwa, Prof Safari, Baregu na Salum Mwalimu wataandamwa mpaka watimke. Lowassa ndio kabisaaa, hakuna atakayetaka kulisikia hata jina lake.

Inatia huruma sana kwa Chadema iliyofikia hatua ya kuaminiwa na mamilioni ya watanzania kufa kifo cha kibudu na cha aibu kiasi hiki.

Watamkumbuka, watamlilia na watajutia matusi waliyomporomoshea Dk Wilbroad Slaa ambaye mpaka leo mimi namwamini, namkubali na ninamuunga mkono. Dk Slaa atabakia mshindi wa kudumu ktk Chadema.

Tukubali tusikubali kesho Chadema itapigwa mweleka ambao haikuwahi kuufikiria na viongozi wake wataparaganyika kuanzia hiyo kesho.

teh teh teh Leo tar 26 DEC wapi mnyukano?
au we ni msengerema?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom