Baada ya uchaguzi kuna dhambi gani kuunda Serikali ya Umoja Tanzania?

kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
12,307
12,602
Mpaka sasa CCM na CHADEMA vina wafuasi wengi sana kwenye mikutano yao ya kampeni. Kama wingi wa watu ni mojawapo ya viashiria vya kuungwa mkono na watu wengi basi ccm na chadema vinaungwa mkono wa watu wengi.

Nionavyo mimi hamasa ni kubwa sana kwa vyama vyote, hivyo mtu atajidanganya mwenyewe kama atasema kuwa CCM au CHADEMA imeshinda uchaguzi huu wa 2020 kwa kishindo. Hata kama takwimu zitafanywa sionyeshe hivyo lakini kuna mtu au watu nafsi itawasuta kwelikweli.

Maendeleo hayana chama na Tanzania ni yetu sote na maendeleo yakija wadau ni sisi sote., Hivi kuna ubaya gani kama watanzania hawa wote wakijumuishwa kwenye selikali ijayo ili wajione sehemu ya serikali yao?
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
NAAPA, TENA NAAPA, hata kama sina mamlaka kwa vyama upinzani, wasije kubali mbinu chafu ya vyama tawala vikongwe Afrika ya kuomba serikali ya umoja wa kitaifa pale zinapoona mambo kwao magumu. Mbinu imetumika kuua nguvu ya vyama vya upinzani au nguvu ya kiongozi wa chama cha upinzani chenye nguvu. HAKIKA NAOMBA UPINZANI MSIKUBALI.

Tumeona mifano hiyo Zimbabwe na Tsivangirai (sic) (RIP), Kenya kwa Raila, hata Seif na CUF huko ZNZ etc

Ningeandika zaidi. Niishie hapa. Upinzani pambaneni mpaka mwisho.
 
Hakuna siasa za Poo hapa. Kama CCM imekuwa pekee ikipiga siasa miaka 5 huku vyama vya upinzani vikipigwa pingu na bado Leo hii baada ya miaka 5 inaendeshwa garidwe zito na CHADEMA jua wazi kuwa CCM haikubaliki na imeshindwa. Serikali ya umoja ni muhimu lakini bila kuishirikisha CCM. CHADEMA wanakijua hilo na watafanya hivyo. CCM ife mbele kwa mbele na majivu yake yatupwe baharini. Hatutaki kuiona wala kuisikia.
 
Hili jambo lilitakiwa kufanyika 2015.

Hata hivyo miundo ya serikali huongozwa na sheria zilizopo mfano Zanzibar katiba yao inawataka wawe na Serikali ya Umoja wa Kitaifa. Kwa upande wa Muungano hakuna kitu kama hicho
 
Kubwa hapa watanzania Kama wamiliki wa nchi yao kwa Sasa ni Kila bahada ya miaka mitano nikumpima mgombea vizuri na chama chake, akiingia madarakani na kufanya sivyo Basi wanapigwa chini kinaingia chama kingine, hapo eshima itakuepo.
 
Back
Top Bottom