Baada ya Tundu Lissu kuangukia pua Mahakamani, Spika Ndugai asema ukiheshimu mamlaka huwezi kupata matatizo

Doncy monco

Member
Jul 26, 2019
38
101
Baada ya Mahakama Kuu kanda ya Dar es Salaam kutoa uamuzi wake ambapo Tundu Lissu ameangukia pua, Spika Job Ndugai amesema kwamba kama watu wakiheshimu mamlaka yaliyopo basi huwezi kupata matatizo.

Spika Ndugai amezidi kusema...

"Mambo haya pengine mtayasikia wenyewe huko nje, mimi sitaki kuyasema.
Mambo haya ukiheshimu mamlaka huwezi kupata matatizo haya, haiwezekani bahati mbaya Spika hawezi jitokeza kila wakati kujibu kila mtu anaenda kwenye mitandao sijui ningeweka wapi sura yangu.

Hivi kumjulisha Spika kwamba mheshimiwa kuwa mimi sitaweza kuhudhuria bunge hili la 16 kwa kuwa nipo kwenye matibabu unaweza kunipigia simu au kuandika message taarifa utakua umetoa.

Kwa hiyo mengine yote unafanya isipokua kumwambia Spika mwaka unapita tuu nakuona, mengine yote unaweza kufanya ila kuwasiliana na huyu Spika haiwezekani itafika mahali watu wataruka na wewe tu na usipige kelele umeyataka mwenyewe kwa sababu taaratibu mnazijuaa. Kwa hiyo waheshimiwa wabunge Tukifuata taratibu wala hatutagombana

Habari ya zile fomu, zile za maaadili ni lazima tujaze ni takwa la katiba hata Mh Mbowe aliniandikia barua aliopokua gerezani mwezi wa 12 kwa mba nipo sehemu ambapo siwezi kujaza zile fomu nipo gerezani Segerea lakini nikitoka ntazijaza kwani kulikuwa kuna ugomvi alivyotoka alijaza lakini husemi , huandiki, huwasiliani wala hufanyi nini, wewe unapuyanga na yako ukitoka una yako"
 
Yani wauaji wa Lisu wanatamani hukumu hii kama ingekuwa inaua basi zile risasi zihamie kwenye hii hukumu immalize kabisa Lisu. Nduguyai Leo atapongezwa na wanywa damu kwa mvinyo murua wa damu ya mtoto mchanga ili kuongeza Nguvu za ushetani wao.
 
Alafu wanataka eti mandege ya serikali yakikamatwa, tuhuzunike pamoja.

Bora nihuzunike na shetani kuliko hawa watu!
Na hakuna anaye waomba Wasaliti na Vibendera kuasiadia au kuhuzunika pale ndeze za Tanzania zinapo kamatwa
Wacha ujinga
Hiyo ni teila bado dawa itawaingia
Hii ni mamlaka iliyo wekwa na Mungu
Nyie mashetani hamta weza kamwe
 
Haki inapatikana kwa Mungu tu, kwa binadamu utaumia moyo sana
Mkuu;
Hoja yako imebeba ukweli unaotoa hitimisho la kibinadamu.

Tunaenda mahakamani ili kubahatisha kama tutapata haki na sio kupata haki.

Msingi wa rufaa mahakamani ni kuonyesha kuwa haki hutolewa kwa kubahatisha.

Huwa ninashangaa kuona baadhi ya watu wanalalamika baada ya kushindwa kesi. Wao wanadhani haki isiyo na mashaka hupatikana mahakamani!
 
Na yeye Spika, kama hakuona taarifa rasmi kumhusu huyu ndugu mezani kwake huku akitambua masahibu yaliyompata, angemkumbusha kwamba.....

Bwana najua na wengine wote wanajua uliumizwa karibu ya kupoteza uhai wako na unaendelea kupigania uhai wako hospitali...

Lakini wakati unaendelea na matibabu yako, hebu fanya 1, 2 ,3 ili kusitokee shida huko mbeleni kwa sbb leo Mimi ninayejua nipo lakini naweza kesho na keshokutwa nikawa sipo kwa namna yoyote ...

Sasa tujiulize alifanya hivi kweli kama anamtakia mema huyu ndugu?

Ilikuwaje akaanzisha vita ya maneno tu na mgonjwa na kwa kuwa yeye ana nguvu za kimaamuzi na mamlaka akaamua kuyatumia ndivyo sivyo?

Leo anapata wapi ujasiri wa kutoa kauli hii ya kinafiki?

Mimi nasema there is no way tunaweza kuwaheshimu viongozi wa namna hii wenye uthubutu wa kutumia mamlaka yao kuumiza wengine.....!!!

Ni kuendelea kuwaonesha kuwa nguvu na mamlaka yao yanaweza kuwa challenged popote pale na kwa njia zozote halali.....

Walikuwepo viongozi waliokuwa wabaya na makatili kuliko hawa lakini walishaoza chini ya ardhi na roho zao zinasubiri hukumu ya mwisho ya Mungu aishiye milele....

Sembuse Ndugai na Magufuli?????
 
21 Reactions
Reply
Back
Top Bottom