Baada ya Tume ya uchaguzi kuvuka lengo la uandikishaji wapiga kura CCM kutoa semina elekezi kwa viongozi wake wa serikali za mitaa

Mambo mawili makubwa yamejitokeza hivi karibuni kwanza CCM imeshinda uchaguzi wa serikali za mitaa kwa kishindo, pili Tume ya taifa ya uchaguzi imevuka lengo kwa kuandikisha wapiga kura wengi kuliko ilivyotarajiwa.

Hii maana yake ni kuwa uchaguzi mkuu wa 2020 utakuwa na wapiga kura zaidi ya milioni 29 hii ni historia.

Kwa kuliona hilo CCM inatarajia kutoa semina elekezi kwa viongozi wake wa serikali za mitaa ikiwa ni matayarisho ya kushiriki kikamilifu katika uchaguzi mkuu.

Ikumbukwe kuwa wananchi wengi wamejiandikisha kupiga kura baada ya kuridhishwa na maendeleo yanayoletwa na serikali ya awamu ya 5 na kwa mara ya kwanza tangu tupate Uhuru watanzania wameanza kuona thamani ya kura zao.

Hongereni CCM.

Maendeleo hayana vyama!
Mkuu,
Hongereni sana kwa ushindi wa kishindo! Kwa kweli ulikuwa wakishindo kikubwa. Maana hadithi zake zimesikika ulimwengu mzima. Dunia yote sasa inajuwa kwamba Chama chenu kinajuwa hasa kupindua.
Hichi chama kimekuwa maarufu sana kwa kupindua pindua kila kitu. Kwa mfano hupindua maneno, watu, kura, matokeo ya uchaguzi, na kadhalika.
Kwa hakika kwa wasifu wake huu ni lazima kishinde kwa mshindo mkubwa mno. Na kwa kweli kitaendelea kuleta mshindo mpaka pale watu watakapoamua kukataa kupinduliwa! Vyenginevyo mtaendelea kusherehekea ushindi wenu wa kupindua pindua. Ila muwe waangalifu musije mukapinduana wenyewe kwa wenyewe!
 
Nimeamini kama hukubaliki hata ujipake manukato hutoboi. Juzi mtendaji wa mtaa wetu kaitisha kikao kujitambulisha na kujadili maendeleo, hayo mahudhurio ni aibu.

Yeye na wapambe wake wakaishia kusema kwa sauti kubwa kuwa wao ndio waliochaguliwa, na kama kuna wengine tulikuwa tunawataka walijitoa hivyo tufanye kazi na yeye kwakuwa yuko tayari.

Alipoona inafika jioni idadi bado ni ndogo sana, akawa anasema mtu aliyetokea kwenye kikao hata akipata matatizo asiende hapo ofisini. Hapo nikawa najiuliza hiyo wanayosema wanakubalika ndio ipo hiyo?
Tulitoboa na kuwabwag 2015 na hii ya TAMISEMI kama tangu muanze unashindwa bora mjiunge na CCM tu maana 2020 utakuwa aibu

USSR

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tulitoboa na kuwabwag 2015 na hii ya TAMISEMI kama tangu muanze unashindwa bora mjiunge na CCM tu maana 2020 utakuwa aibu

USSR

Sent using Jamii Forums mobile app

Hamna uwezo wa siasa za ushindani, sana sana mnategemea mbeleko za vyombo vya dola. Huna cha kujisifia kama mwanaume iwapo vyombo vya dola ndio nguvu yako.
 
Back
Top Bottom