Baada ya tetesi za Rais Magufuli kutembelea Mkoa wa Tabora, Mkuu wa Wilaya ya Tabora mjini Komanya Kitwala abadili gia angani

kavyilu

Member
Dec 14, 2019
28
53
Nianze kwa kuwasalimu wana jukwaa.

Moja kwa moja kwenye mada.

Kuna uvumi na tetesi za Mh. Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania kutembelea Mkoa wa Tabora (Tabora mjini)

Yapo makatazo Mh. Rais aliyatoa kwa wakuu wa mikoa na wilaya kuhusu michango.

Komanya Kitwala alikaidi agizo la Rais na badala yake kuagiza vitabu vya michango na kuvigawa kila kata. Waliopewa wakusanye michango ni Maafisa Elimu wa kata kwa kushirikiana na watendaji wao wa kata na mitaa.

Mtendaji yeyote aliekusanya michango kizembe alitishiwa lock up, na Mkuu wa wilaya akawa mkali kuhakikisha ujenzi wa madarasa unakamilika kwa michango ya wananchi.

Tabora mjini kero kubwa inayowakuta wananchi ni michango inayosimamiwa na Mkuu wa wilaya.

Hii ni kinyume na maagizo ya Mh. Rais ya kutaka michango itolewe kwa hiyari tena anaetaka ku hangia apeleke mwenyewe kwa mkurugenzi, Tabora mambo ni tofauti michango inasakwa nyumba kwa nyumba na watendaji wa kata wakihofia kushambuliwa na Mkuu wao wa wilaya.

Baada ya kusikia Mh. Rais atakuja Tabora na Wananchi wa Tabora wanatabia ya kuandika mabango kufikisha ujumbe kwa Rais wao, sasa amewageuka aliowatuma na kuwapa vitabu wachangishe.

Jana tarehe 20Jan 2021 ametangaza hataki michango ili kujiosha na kutengeneza ushahidi mbele ya wakubwa wake wa kazi.

Amepiga marufuku michango ambayo alikuwa akizurura kila kata ku-harass watendaji wa kata na Waratibu elimu,hii si sawa kwa kiongozi kukosa msimamo katika mambo unayoyasimamia.

Kwakuwa alishakaidi agizo la Rais kuhusu michango,ni vyema aendelee na michango kisha aandae majibu atakayojibu siku akiulizwa.

Sio kutuma watu tena kwa kuwatishia polisi au kuwatbua endapao watakusanya chini ya kiwango,sio unashinikiza darasa lijengwe huku kuliwa hakuna senti yoyote ya serikali wala wadau, kazi kuhimiza michango ya lazima kwa wananchi wenye njaa,halafu unasoma upepo.na kuona ulikuwa unakosea halafu unabadilika ili uonekane waliokusanya wewe hukuwatuma.

Swali kwani tamko litoke 20 Jan 2021 wakati katazo la Rais lilitoka zaidi ya miaka miwili iliyopita. Unamdanganya nani na kwa lengo lipi?

Jambo la mwisho ni kukumbushia ujenzi wa madarasa 124 ndani ya manispaa ya Tabora, katika ujenzi huu Mkuu wa wilaya alifanya harambee na kukusanya zaidi ya Mil 800 ,lakini tangu mwaka 2018 zilipokusanywa hakuna hata darasa moja lililojengwa.

Nitumie jukwaa hili kuuliza,hizo fedha zipo wapi na mkuu wa wilaya anampango gani? Au ndio Zinajenga lile jumba lako kule Mwanza?

Swala la Michango bado halijaeleweka kwa baadhi ya viongozi,hata hivyo nawapongeza viongozi wanaotafsiri na kusimamia maagizo ya Mh. Rais kwa wakati.
 
Acheni majungu.Mnaleta mambo yenu ya wivu mitandaoni.Acha kufuatilia maisha ya watu .Rais ana vyombo vyote vya ulinzi na usalama kwa mamlaka aliyonayo anapewa taarifa juu ya Mambo yanayoendelea katika kila eneo la nchi hivyo hayo Mambo unayoyasema kama ni kweli atakuwa anayafahamu na Kama Kuna ukiukwaji wa maagizo na maelekezo yake hatua za kinidhamu zitachukuliwa kwa wahusika wote vinginevyo ukiona kimya basi ujue huo ni umbeya wa hali ya juu mtoa taarifa utatakiwa ujitafakari kwa kina.
 
Kwani shule hazikamiliki? Na kwanini wengine wachange na wengine wasichange? Tatizo uvivu tu, asiyefanya kazi na asile Sasa hao watoto wenu waondoeni shule warudi nyumbani mkae nao, michango inayotakiwa kulalamikiwa na michango ya pesa nyingi Ila munachangishwa hela ndogo Kila mmoja Ili wote musiumie wewe unalalamika, hata Kama serikali imesema shule ni bure wewe Kama mzazi unatakiwa kuwajibika kutunza watoto wako na kuwapa elimu ikiwa wanaokusaidia wamekwambia ongezea maboresho shida iko wapi?
 
Duh mnamsagia kunguni, kuweni na huruma January hii ngumu akitumbuliwa sasa hivi anaweza akafa kwa stress.
 
Kuna clip nimesikia zinatbea kwwnye magurup ya chama wapambe wa mkuu wa wilaya wanazodoana na wanaompinga
Tatizo la tabora ni majungu,lkn tatizo la DC ni ubabe usiokuwa na mipaka.hata katibu na mwenyekiti wa chama hawaelewani
 
Duh mnamsagia kunguni, kuweni na huruma January hii ngumu akitumbuliwa sasa hivi anaweza akafa kwa stress.
Kweli kabisa watu hawana huruma,wanamuharibia mwenzao hata kama anachangisha si kwa nia njema? Ukute na yeye anafanya hivo kutetea posho yake isiguswe,sasa mzee akisikia kwamba wilayani kwake kuna michango itakuwaje?
 
Mwenye mkoa wa tabola hana kerere. Katibu tawala nae ni mtu wa kazi,lakini mkuu wa wilaya ni vurugu tu.
Nakumbuka aliwahi kutuhumiwa kutoelewana na madereva wake,akawa anabadili dereva hadi wakafika 14,aligombana na katibu tawala wake wa wilaya,akaletewa katibu tawala mpare nae nasikia siku hizi ni maji na moto,hawaelewani kabisa. Katibu tarafa amegombana nao mpaka mmoja amehamisha ofisi kumkimbia dc ,aliebaki kila siku anawekwa ndani

Huyo kikwala konanywa ni mkorofi saana
 
Nianze kwa kuwasalimu wana jukwaa.

Moja kwa moja kwenye mada.

Kuna uvumi na tetesi za Mh.Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania kutembelea Mkoa wa Tabora (Tabora mjini)...

Katiba mpya katiba mpya.... Lazima tuwe na NATIONAL PILLARS (misingi ya kitaifa itakayosimamia maamuzi/mipaka ya viongozi na mipaka/majukumu/wajibu wa wananchi ktk nyanja zote, katiba itakayotoa dira na tafsiri ya kimfumo, Nini tunataka kufanya,nani atafanya kwa namna gani,wakati gani, kwasababu gani!!!.

Katiba itakayotupa sheria,miongozo,kanuni na makatazo ya wapi tunapolipeleka TAIFA. Tofauti na hivyo tutaendelea kuviziana kwa makatazo, busara, utashi na maono ya mtu mmoja Mmoja jambo ambalo ni hatari kwa ustawi na maendeleo endelevu ya Taifa.
 
Hapo yaliyoandikwa ni kweli tupu fitina kwangu mwiko,yeyote anehusika aende kwenye kata mbali mbali awaulize wananchi atakutana na hii taarifa ya michango,kama uliambiwa wachangie kwa mkurugenzi wewe unatukuta ndani unamaana alieelekeza hakutafakari faida na hasara za michango?
 
Kuhusu ugomvi katibu tawala wake yule mpare ni kweli,wametifuana mpaka sasa ofisi inawaka moto,wakwanza walivurugana akaondoka,huyu mpaka kamnyenyekea kwa kiwango kisichoelezeka lakini yule dc haambiliki wala hashauriki.

Kuna katibu tarafa anaitwa Brauni kaamua kulimbia ofisi,maana maudhi mengi hayavumiliki
 
Acheni majungu.Mnaleta mambo yenu ya wivu mitandaoni.Acha kufuatilia maisha ya watu .Rais ana vyombo vyote vya ulinzi na usalama kwa mamlaka aliyonayo anapewa taarifa juu ya Mambo yanayoendelea katika kila eneo la nchi hivyo hayo Mambo unayoyasema kama ni kweli atakuwa anayafahamu na Kama Kuna ukiukwaji wa maagizo na maelekezo yake hatua za kinidhamu zitachukuliwa kwa wahusika wote vinginevyo ukiona kimya basi ujue huo ni umbeya wa hali ya juu mtoa taarifa utatakiwa ujitafakari kwa kina.
Hata humu ni chanzo rasmi kabisa cha swrikali/wahusika ikiwemo Mh Rais kupata taarifa. Hata hao unaosema ni rasmi/timu ya kumfikisha Rais taarifa nao ni binadamu tena watanzania hawa hawa wenye sifa kuu ya kuficha maovu na kulingana.

Ni mara ngapi Maris wamedanganywa na hivyo vyombo/taasisi rasmi unavyovisema vikiwemo na vikiahuhidia..... Hata raia mmoja ana haki na wajibu wa kutoa taarifa kwa njia inayofaa kwa kuzingatia/bila kuathiri misingi ya maadili na maslahi ya Taifa ikiwemo kutumia vyombo vya habari km mitandao ya kijamii.

NIKUKUMBUSHE.....TAARIFA ZA SHULE YA JIMBO LA UBUNGO...inayowalaza nje usiku kucha hao unaowaita mamlaka halali za kumpasha habari Mh Rais amezipata kupitia Media tena za kijamii akiwa ziarani hukoooo Kamera au tuseme kupitia JUNGU km unavyotaka iwe.

Hivi Watanzania tumelogwa na nani? Na kwa bandiko lako dhahiri nawe ni mpiga dili au mhitimu uko mtaani unayewaza nawe ukipata nafasi uchumie tumbo....
 
Hata humu ni chanzo rasmi kabisa cha swrikali/wahusika ikiwemo Mh Rais kupata taarifa. Hata hao unaosema ni rasmi/timu ya kumfikisha Rais taarifa nao ni binadamu tena watanzania hawa hawa wenye sifa kuu ya kuficha maovu na kulingana...

Huo ndio ukweli na mimi niliposoma comment yake nikajiuliza hivi taarifa za wanafunzi kukaa chini alizipata wapi
Nashangaaa
 
Back
Top Bottom