Nianze kwa kuwasalimu wana jukwaa.
Moja kwa moja kwenye mada.
Kuna uvumi na tetesi za Mh. Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania kutembelea Mkoa wa Tabora (Tabora mjini)
Yapo makatazo Mh. Rais aliyatoa kwa wakuu wa mikoa na wilaya kuhusu michango.
Komanya Kitwala alikaidi agizo la Rais na badala yake kuagiza vitabu vya michango na kuvigawa kila kata. Waliopewa wakusanye michango ni Maafisa Elimu wa kata kwa kushirikiana na watendaji wao wa kata na mitaa.
Mtendaji yeyote aliekusanya michango kizembe alitishiwa lock up, na Mkuu wa wilaya akawa mkali kuhakikisha ujenzi wa madarasa unakamilika kwa michango ya wananchi.
Tabora mjini kero kubwa inayowakuta wananchi ni michango inayosimamiwa na Mkuu wa wilaya.
Hii ni kinyume na maagizo ya Mh. Rais ya kutaka michango itolewe kwa hiyari tena anaetaka ku hangia apeleke mwenyewe kwa mkurugenzi, Tabora mambo ni tofauti michango inasakwa nyumba kwa nyumba na watendaji wa kata wakihofia kushambuliwa na Mkuu wao wa wilaya.
Baada ya kusikia Mh. Rais atakuja Tabora na Wananchi wa Tabora wanatabia ya kuandika mabango kufikisha ujumbe kwa Rais wao, sasa amewageuka aliowatuma na kuwapa vitabu wachangishe.
Jana tarehe 20Jan 2021 ametangaza hataki michango ili kujiosha na kutengeneza ushahidi mbele ya wakubwa wake wa kazi.
Amepiga marufuku michango ambayo alikuwa akizurura kila kata ku-harass watendaji wa kata na Waratibu elimu,hii si sawa kwa kiongozi kukosa msimamo katika mambo unayoyasimamia.
Kwakuwa alishakaidi agizo la Rais kuhusu michango,ni vyema aendelee na michango kisha aandae majibu atakayojibu siku akiulizwa.
Sio kutuma watu tena kwa kuwatishia polisi au kuwatbua endapao watakusanya chini ya kiwango,sio unashinikiza darasa lijengwe huku kuliwa hakuna senti yoyote ya serikali wala wadau, kazi kuhimiza michango ya lazima kwa wananchi wenye njaa,halafu unasoma upepo.na kuona ulikuwa unakosea halafu unabadilika ili uonekane waliokusanya wewe hukuwatuma.
Swali kwani tamko litoke 20 Jan 2021 wakati katazo la Rais lilitoka zaidi ya miaka miwili iliyopita. Unamdanganya nani na kwa lengo lipi?
Jambo la mwisho ni kukumbushia ujenzi wa madarasa 124 ndani ya manispaa ya Tabora, katika ujenzi huu Mkuu wa wilaya alifanya harambee na kukusanya zaidi ya Mil 800 ,lakini tangu mwaka 2018 zilipokusanywa hakuna hata darasa moja lililojengwa.
Nitumie jukwaa hili kuuliza,hizo fedha zipo wapi na mkuu wa wilaya anampango gani? Au ndio Zinajenga lile jumba lako kule Mwanza?
Swala la Michango bado halijaeleweka kwa baadhi ya viongozi,hata hivyo nawapongeza viongozi wanaotafsiri na kusimamia maagizo ya Mh. Rais kwa wakati.