Baada ya tamko zito la Dr. Slaa, Chadema sasa yatakiwa kutoa takwimu zao za Urais... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Baada ya tamko zito la Dr. Slaa, Chadema sasa yatakiwa kutoa takwimu zao za Urais...

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Rutashubanyuma, Nov 3, 2010.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Nov 3, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,806
  Likes Received: 419,846
  Trophy Points: 280
  Wapigakura wengi waliompigia kura Dr. Slaa wamefurahishwa na hatua ya utulivu wa Raisi wetu Mtarajiwa ambaye JK ametumia mabavu ya dola kujisimika madarakani kwa minajili ya udikteta..........

  Lakini wapigakura hao sasa wana kiu ya kuelewa ushahidi wa Chadema wa ni nani aliyeshinda kinyang'anyiro cha uraisi kwa sababu takwimu za NEC wanaamini ni matunda ya kuchakachua na wala hata hawazifuatilii hata kidogo...........

  Zipo jitihada za watu wasiofahamika malengo yao nini ambao tayari wameanza kutuma sms za uchochezi za kuhamasisha uvunjajii wa amani kwa kudai maandamano ya amani ya kupinga matokeo lakini swali la kujiuliza unapopinga kitu lazima uwe unacho chako mkononi cha kulinganishia vinginevyo utakuwa unatwanga maji kwenye kinu..............

  Hili sasa ndilo shinikizo la wapigakura kwa Chadema toeni takwimu zenu ili tutafakari hatua bora za kufanya kuhakikisha haki inatendeka....................

  Sisi siyo nyumbu wa kupelekeshwa bila maandalizi ya kutosha............
   
 2. luvcyna

  luvcyna JF-Expert Member

  #2
  Nov 3, 2010
  Joined: Feb 24, 2009
  Messages: 1,441
  Likes Received: 1,035
  Trophy Points: 280
  Ruta na ukweli kabisa nasikiliza taarifa ya habari hapa Dr anatoa tamko kali na kaja na kila aina ya uthibitisho wa kudhihirisha matokeo yanayotangazwa na Nec hayana uhalisia....... inaniuma sana mtu anavyotaka kuingia madarakani kwa mabavu ilihali anatambua fika kabisa ya kuwa watu hawamhitaji tena,
  INAUMA MNOO, ni ngumu kuvumilia hali kama hii
   
 3. M-mbabe

  M-mbabe JF-Expert Member

  #3
  Nov 3, 2010
  Joined: Oct 29, 2009
  Messages: 4,992
  Likes Received: 3,742
  Trophy Points: 280
  This one, coming from a seemingly die-hard CHADEMA follower, shows the highest level of maturity. Kudos!
  Kwa sisi wengine wote ambao ni wafuasi wa Dr Slaa (sijasema Chadema kwa vile najua wapo CCM wengi tu ambao ni wafuasi wakubwa wa Dr Slaa) nashauri tuiunge mkono approach hii kwa nguvu zetu zote.
  Embu tusaidiane kupata ushahidi wa rigging!
   
 4. M

  Magobe T JF-Expert Member

  #4
  Nov 3, 2010
  Joined: Mar 19, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 357
  Trophy Points: 180
  Naunga mkono ila nadhani uliopo kwa Dr Slaa unatosha kwa vile ni 'documentary' - yaani, ule amabao kila wakala alisaini kuwa anaafiki kura za huyu ni hizi na za yule ni zile. Tusubiri huo ushauri ufike mahali husika ila sisi wote tutulie na tulinde amani amani wakati wote whether kutapatikana mwafaka au kukosekana. Mimi ni mdau wa non-violence approach - peace building!
   
 5. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #5
  Nov 3, 2010
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  Askari tupo nyuma ya DR wa ukweli tunamsikiliza hatuwezi buruzwa kijinga jinga
   
 6. J

  JIWE2 Senior Member

  #6
  Nov 3, 2010
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 123
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Pamoja tunawakilisha
   
 7. Kasheshe

  Kasheshe JF-Expert Member

  #7
  Nov 3, 2010
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 4,690
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Savimbi aliipeleka Angola vitani kwa miaka zaidi 25, Maalifu Seif aliipeleka Zanzibar kutotulia kwa miongo fulani... sasa Mh. Dr. Slaa ana lake pia. Mwenyezi Mungu tulinde katika hili.


  Kwa katiba matokeo ya Urais tu ndio hayawezi ku-be-challenged mahakamani in case tume ikiyatangaza... sasa haya ya Mpendazoe mbona ngoma Rahisi sana kwa nini Dr. Slaa wasiende huko mahakamani?
   
 8. SOARES

  SOARES Member

  #8
  Nov 3, 2010
  Joined: Jul 6, 2007
  Messages: 89
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 15
  Kumetolewa hoja kuwa ili kutokupingana na katiba yetu ya sasa kuwa Rais akishatangazwa hakuna mamlaka inayoweza kubatilisha, naona ni bora kusimamisha utangazi wa matokeo unaofanywa ili kuziba mianya ya kuletewa Dikteta Sultani
   
 9. The Invincible

  The Invincible JF-Expert Member

  #9
  Nov 4, 2010
  Joined: May 6, 2006
  Messages: 4,723
  Likes Received: 1,218
  Trophy Points: 280
  Hujaacha bado kutumia makalio kufikiri?
   
 10. bfsam2000

  bfsam2000 Member

  #10
  Nov 4, 2010
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 20
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 5
  nina taarifa za karibu,jumla ya kura za ubunge na uraisi kwa bukoba mjini zina tofauti ya elfu ishirini.

  sasa sijui hizo elfu ishirini kwenye ubunge zimeharibika au Vipi?

  na sehemu nyingi pia jamaa data wanazo
   
 11. G

  Gaza Senior Member

  #11
  Nov 4, 2010
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 103
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Hatua bora ni kuishinikiza tume isitishe matangazo ya kupika .tumechoka na dhuluma kwa kusingizio cha amani
   
 12. C

  Challenger M Member

  #12
  Nov 4, 2010
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 81
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  sawa kabisa hii ndio ya kuibana maana hawana hata haibu
   
 13. Eliphaz the Temanite

  Eliphaz the Temanite JF-Expert Member

  #13
  Nov 4, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 2,836
  Likes Received: 362
  Trophy Points: 180
  Yes we can! This time tunapinga matokeo kisayansi!
  Kwanza ushahidi wote ukusanywe simu, matokeo halali vituoni, mikakati haramu ya uchakachuaji. Tuwapelekee wahisani wote duniani kwanza tumzuie asiendeleze utembezaji bakuli kama kawaida yake. Pili tuwashitaki kwa wananchi!
   
 14. Duduwasha

  Duduwasha JF-Expert Member

  #14
  Nov 4, 2010
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 5,142
  Likes Received: 2,177
  Trophy Points: 280
  Sureyes we can kupinga tu hata mimi Simkubali kutawaliwa na dikteta uchaguzi kiasi kidogo sana umekuwa wa haki lakini tume hakuna haki record ya kuchelewa kutoa matokeo ipo india tu sababu ina idadi kubwa ya watu Tume gani mgombea anakutwa na masanduku ya kupiga kura then anatangazwa kashinda kha udhalimu ndio utawala wa sheria huu. (Nyerere alisema kwa mujibu wa sheria za dikteta) Me nadhani wakimaliza utawala wao 2015 bora wakimbie mbali sana tena na familia zao ila tutawakamata tu mla huliwa na sie tutakuja kumla tu jamaa jinsi alivyo hata ujumbe wa nyumba kumi hauwezi sasa nchi inayumba kodi zetu na pesa za uomba omba anaotumia jina letu anazifanya kama akauti zake kufanyia udhalimu.. Nikipata nauli nitaenda kumpasha
   
 15. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #15
  Nov 4, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,507
  Likes Received: 19,922
  Trophy Points: 280
  sio pumba hii mazee?? heh!!
   
 16. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #16
  Nov 4, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,507
  Likes Received: 19,922
  Trophy Points: 280
  tuko pamoja
   
 17. JohnShaaban

  JohnShaaban JF-Expert Member

  #17
  Nov 4, 2010
  Joined: Aug 23, 2007
  Messages: 465
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  "Ukikuta mahali mawazo ya vijana na wazee yanafanana, ujue hapo pamedumaa" - J. S. Warioba
   
 18. MwanaCBE

  MwanaCBE JF-Expert Member

  #18
  Nov 4, 2010
  Joined: Sep 23, 2009
  Messages: 1,773
  Likes Received: 544
  Trophy Points: 280
  Ni Slaa au Mkwere ndo mwenye lake jambo??? We vipi wewe!!!!
   
 19. g

  guta Senior Member

  #19
  Nov 4, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 179
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Hapo naungana na wewe, naomba takwimu zichapishwe hata kwenye gazeti moja wapo itolewe kama toleo maalumu liwe limeambatanishwa.
   
 20. Mtumishi Wetu

  Mtumishi Wetu JF-Expert Member

  #20
  Nov 4, 2010
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 4,986
  Likes Received: 427
  Trophy Points: 180
  Tupo pamoja, tume iache kabisa kutangaza matokeo pumba! Ushahidi wote wa mawakala vituo vyote ukusanywe, INTERNATIONAL COMMUNITY FRATENITY ijulishwe huo ukola wa hawa jamaa, ili waaibike na dhuluma zao.
  Wasipewe respect tena ya kuwa wazungumzaji wa democracy duniani, ijulikane kuwa ni serikali ya KIDECTATOR. Maana kuwazuia muda huu wasitawale ningumu. Maandalizi na mikakati bora ya kuwa na utawala madhubuti wa kidemocrasia ianze sasa.
  The best way to have a good idea is to have lots of ideas. Linus Pauling.
   
Loading...