Baada ya Taliban kuichukua Afghanistan, Al-Shabaab nao waongeza juhudi za kujilipua mabomu

Kulizungumzia suala usilolijua ni changamoto.. Mimi ni muislam, katika mafundisho si ruhusa kutoa nafsi ya mtu tena haswa ambaye hana ukorofi na wewe, dini yetu ina sheria zake na mipaka yake mpaka kwenye vita, ukisoma vizuri utagundua hawa wapuuzi wana yao, hawana elimu yaa kutosha (wako brainwashed) na wale wenye elimu ya kutosha wana matamanio yao binafsi..

Nakubali zipo aya(tuite aya ni maelezo) zinazozungumzia vita, ila kuzielewa aya za quraan unahitaji elimu na sio kubeba tu kile ulichokiona, quraan imeshushwa kidogo kidogo, aya zake zilikuwa zikishushwa kwa sababu maalum, hivyo inabidi ujue sababu ya kushushwa, sio kusoma pigana, kissha unachukua uoanga ukapigane, je unapigana kwa mazingira gani, quraan imezungumzia mambo yoote ya kijamii, na washenzi hawa vinhine vyoote hawafati zaidi ya aya wanazojichagulia, mie huwa nasema hawa si waislam..
Mtume baaada ya kutimuliwa maka na kwenda madina, aliingia mkataba wa amani na wapinzani wake.. Lakini wale mabwana ndani ya mkataba wakawavamia waislam, ndio aya(maelezo) kadhaa yakashuka kwamba piganeni nao na vita ikiisha, ruksa wapinzani kuja nchini mwenu na inabidi muwalinde.. Lakini hizi aaya nyingine hawazichukui wanachukua hii. Aya ya kupigana tena kinyume na mafundisho, mtume hakufunndiaha kua watoto, wakina mama ama adui aliiyesalimu amri, maadui zake kadhaa badaee walikuja kuwa waislam

Nakuwekea aya kadhaa za quraan na tafsir toka kwa aliyekuwa kadhi mkuu wa Kenya

Elimu nii pana saana, dini imesisitiza tusome, aya ya kwanza kushuka ni msisitizo wa kusoma, moja ya sababu ya kusisitizwa kusoma ni hii usijekuwa brainwashed vizuri.. Sasa wewe umesom juu juu madhara yakes ndio hayo inachukuliwa aya moja juu juu watu wanakuwa tayari wamekukamata..


Katika hii attachment , Za juu nii aya chini ni Maelezo ya aya.. Why imeshuka n.k

Hii ni elimu ndogo niliyonayo mimi wenye elimu zaidi watakuja kuongezea
ALLAH ndio mjuzi zaidi

View attachment 1900788View attachment 1900789
Upo sahihi, na watu wanachojisahaulisha ni kuhusu swala la Vita kati ya watu katika nchi halijaanza Sasa Wala kwasababu ya dini Fulani ila ni mambo yapo kitambo mfano Daudi na Goliath, kikubwa nikuombea Haki na Amani katika nchi zetu Ili kusitokee watu wakajipanga kutafuta Haki na Amani kwa njia ya mapigano.
 
Back
Top Bottom