Baada ya Sudan ya Kusini sasa ni Tanzania ya Kusini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Baada ya Sudan ya Kusini sasa ni Tanzania ya Kusini

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Ligogoma, Feb 14, 2011.

 1. Ligogoma

  Ligogoma JF-Expert Member

  #1
  Feb 14, 2011
  Joined: Aug 27, 2010
  Messages: 2,138
  Likes Received: 858
  Trophy Points: 280
  Happy Valentine wana JF!!

  Tuzungumze ukweli kabisa, Tanzania ya Kusini (Lindi, Mtwara, Ruvuma na baadhi ya mikoa ya Pwani) sehemu ambayo imesahaulika sana hapa nchini!! Kwa wale waliofika maeneo hayo watakubaliana nami.

  Kwanza hawana vyanzo vya uhakika vya mapato na mazao waliyokuwa wanategemea yameporomoka vibaya sana thamani yake soko la dunia, especially korosho!

  Miundo mbinu kiukweli hatuwezi kucompare na mikoa ya kaskazini mfano barabara ya kwenda huko mpaka leo haijakamilika na ni takriban miaka kumi sasa tangu ianze kujengwa na haijakamilika bado!! Barabara gani (Urefu usiozidi 600 km) katika nyanda nyingine iliwahi kujengwa kwa miaka kumi. Ukija kwenye street roads ndiyo balaa kabisa achilia mbali hizo stand kuu zilivyo!!

  Wana bandari nzuri saaana but wakitaka kuagiza bidhaa kwenda na kutoka nje ya nchi mpaka Dar, bandari za Lindi na Mtwara za kazi gani?

  Umeme mpaka leo hawamo kwenye grid ya taifa, wanategemea vyanzo vidogo vidogo vya umeme!! Hata hivyo sehemu kubwa ya maeneo haya hayana umeme kabisa.

  Gesi imesafirishwa kutoka Mtwara mpaka Dar kwa njia ya pipe, why?

  Hakuna viwanja vya ndege vya maana, vipi Lindi au Nchingwea vyote vidogo sana na hakuna upanuzi wa kiwanja chochote kanda hiyo.

  Train, loh! Don`t talk about it hakuna hata reli ila ilikuwapo enzi za ukoloni wakang`oa!

  Kuna kila sababu ya kuanzisha vuguvugu la kujitoa katika hii nchi ya Tanzania na kuunda taifa jipya la Tanzania ya Kusini.
   
 2. SHERRIF ARPAIO

  SHERRIF ARPAIO JF-Expert Member

  #2
  Feb 14, 2011
  Joined: Aug 25, 2010
  Messages: 7,081
  Likes Received: 1,819
  Trophy Points: 280
  No!
  Kila mkoa upewe uwezo wa kujitegemea kivyake. Hapo ndio maendeleo yatakuwa fasta!
   
 3. B

  Byendangwero JF-Expert Member

  #3
  Feb 14, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Hayo tumeyasikia; kwa kuongezea,wamechangia marais 3 kati ya marais wanne waliowahi kuikwea nafasi hiyo hadi sasa; wamepewa heshima ya kuongoza idara ya usalama wa taifa kwa mda mrefu; mzee Kawawa ambaye anatokea huko ndiye aliyekuwa mtendaji mkuu serikalini kwa mda mrefu n.k. Hayo ni baabhi tu ya mambo yanayothibitisha kuwa eneo hilo la kusini halijatengwa, vinginevyo lisingelipewa heshima hizo zote.
   
 4. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #4
  Feb 14, 2011
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,124
  Likes Received: 1,709
  Trophy Points: 280
  Nadhjani jina tanzania tuliondoe tu na tubaki na TANGANYIKA!
   
 5. C

  ChiefmTz JF-Expert Member

  #5
  Feb 14, 2011
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 2,521
  Likes Received: 292
  Trophy Points: 180
  Mbona mikoa ya Kusini haina tofauti na Mikoa mingine. Kama hujatembea nyamaza
   
 6. N

  Ndinimbya Senior Member

  #6
  Feb 14, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 149
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kwa kweli mi siungi mkono kuhusu wazo hilo kwani tatizo lipo kwa viongozi wao ni wabinafsi na hawajengi kwao, hivi kama kiongozi mkubwa anaenda kujenga tanga we unafikiri atashawishi vip barabara bora au train iende kwao wakati tayari kaonesha ubinafsi wa kukaa na nduguze
   
 7. N

  NasDaz JF-Expert Member

  #7
  Feb 15, 2011
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 11,308
  Likes Received: 1,655
  Trophy Points: 280

  tukishajitenga makao makuu yawe rutamba!!!
   
 8. Cynic

  Cynic JF-Expert Member

  #8
  Feb 15, 2011
  Joined: Jan 5, 2009
  Messages: 5,154
  Likes Received: 628
  Trophy Points: 280
  Happy Valentine wana JF!!

  Tuzungumze ukweli kabisa, Sehemu kadhaa za Dar es Salaam (Goba, Gezaulole, Makongo, Ubungo Kibangu, Msewe, Makuburi) ni sehemu ambayo imesahaulika sana hapa Dar!! Kwa wale waliofika maeneo hayo watakubaliana nami.

  Miundo mbinu kiukweli hatuwezi kucompare na zinginge za Dar mfano hamna barabara ya kwenda huko mpaka leo ... Ukija kwenye street roads ndiyo balaa kabisa .....!!

  ...... nk, nk.

  Kuna kila sababu ya kuanzisha vuguvugu la kujitoa katika huu mji wa Dar na kuunda jiji jipya la Dar ya Wachovu.
   
 9. sabasita

  sabasita JF-Expert Member

  #9
  Feb 15, 2011
  Joined: Oct 29, 2009
  Messages: 1,508
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 145
  ha ha hahahaha..oooh weeee
   
 10. Babu Lao

  Babu Lao JF-Expert Member

  #10
  Feb 15, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 2,056
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Nadhani aloanzisha hii thread alikuwa hajua anachoongea, afadhali umemjibu :twitch::twitch::twitch:
   
 11. MaxShimba

  MaxShimba JF-Expert Member

  #11
  Feb 15, 2011
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 35,816
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160
  We had "MADARAKA MIKOANI" Labda umesahau, RTC nk. It didn't work.
   
 12. Madela Wa- Madilu

  Madela Wa- Madilu JF-Expert Member

  #12
  Feb 15, 2011
  Joined: Mar 24, 2007
  Messages: 3,074
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  Kuitegemea na Kujitenga ni vitu viwili tofauti.

  si lazima kujitenga ili ujitegemee.
  Unaweza kujitegemea bila kujitenga, pia unaweza ukajitenga na usijitegemee.
   
 13. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #13
  Feb 15, 2011
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  ewaaa sasa hapa tupo pamoja si kujitenga bali sera za chama changu tukufu CHADEMA za MAJIMBO, hilo ndo suluhisho maana kila jimbo litakuwa na mamlaka na uwezo wa kutumia rasilimali zake ipasavyo kuliko sasa ambako kila kitu mpaka kifikishwe dar halafu mgawanyo uwe sawasawa hata km mnazalisha au rasilimali zinatofautiana.
   
 14. b

  bakarikazinja Senior Member

  #14
  Feb 15, 2011
  Joined: Nov 9, 2009
  Messages: 179
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  wa kusema kijana juzi siyo tu mikoa ya kusini ipo mikoa mingi yenye shida kama hizo na wameisha sema mpaka wamechoka na sasa wameamua kukaa kimya kabisaaaa kwa hiyo jaribu kufanya utafiti utagundua mambo mengi sana
   
 15. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #15
  Feb 15, 2011
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,124
  Likes Received: 1,709
  Trophy Points: 280
  Kwahiyo kutemba kwako kooooooooooooooooote umeona ni sawa?
   
 16. L

  Leornado JF-Expert Member

  #16
  Feb 15, 2011
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 1,534
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Dah mbona Shinyanga, Kagera, Tabora na Singida nako hali ni mbaya?? na wao wajitenge au??

  mikoa ilioendela ni ile iliyokuwa wakati wa ukoloni strategically, na serikali yetu haijafanya mabadilio yoyote kuleta usawa kwenye mikoa yake.
   
 17. m

  mzee wa inshu Member

  #17
  Feb 15, 2011
  Joined: Jan 25, 2011
  Messages: 49
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Watu wa kusini inawapasa kujilaumu nyie wenyewe kwa kutokuwa sharp na kuchangamkia fursa zinazopatikana nchini kuanzia mikoani kwenu mpaka tanzania nszima. Wakati vijana kutoka mikoa ya kusini(wamachinga) wakijazana jijini Dasr es salaam na kufanya biashara ya uchuuzi wakiweka pembeni suala zima shule.

  Suala la miundombinu mibovu hiyo inatokanna nan nyie wenyewe kuridhika na hali hiyo mkiamini kuwa hiyo ndiyo stahili yenu mkiwaacha wenzenu wa mikoa minginwe wakipigia kelele balabala za lami za kata.

  ACHENI UMWINYI, WEKEZENI KATIKA ELIMU MTAONA MABADILIKO

  Mlibahatika kutoa kiongozi wa nchi pamoja na waziri wa miundombinu, mbon\a hawa watu wenu mlishindwa kuwaweka chini na kuongea nao juu ya matatizo yenu. Unafikiri nini kingetokea endapo kiongozi mkuu wa nchi angetokea mikoa ya Kagera, Kilimanjaro au Mbeya? Bilashaka visingizio vingekuwa vingi.

  Kwa msingi huu lazima ufahamu kuwa serikali kama serikali haitakuletea maendeleo endelevu ili hali wewe ukijiklita kwenye biashara ya min'goko na kui`pa kisogo elimu.

  Tembelea miji ya kilwa, lindi mjini, masasi. mtwara, nachimngwea na miji mingine kadhaa ya huko kusini utaoa namna ambavo wageni kutoka mikoa mballimbali wanavochangamkia fursa zipatikanazo kusini huku wenyeji wakitumbua macho kwa mshangao.

  Fanya utafiti, tafuta watu wa mikoa ya kusini ambao wamewekeza nje ya mikoa yao ni wangapi bilashaka ni idadi ndogo sana kulinganisha wageni wanaofuata fursa na ajira mikoa ya kusini.

  Wengi wa watu wa kusini hatupendi kuwekeza kwetu, Mtu akishajenga nyumba yake Mbagala basi hutomwona tena akirudi Lindi, Mtwara au Tunduru labda aitiwe msiba wa mzazi wake au unyago. Kama si hivo yawezekana asirudi kamwe au atarudi baada ya miaka 6 hadi 10.

  Suala la kujitenga halina mantiki endapo watu hawajitambui au kufahamu wajibu wao. Hata mkiachiwa hiyo gesi bado haitakuwa mkiombozi ilhali akili bado haija 'jitune' sawasawa.

  Rais wa awamu ilyopita alitoka kwenu, Rais wa sasa ni shemeji yenu, ok, mnachekelea kwa hilo lakini kaa mjue kuwa maendeleo yenu mmeyakalia nyie wenyewe hao hawana mchango mkubwa saaana kama wao.

  Suala la kushuka kwa korosho ktk soko la dunia kwa nini tuilaumu serikali yetu ya kibongo? Nikawaida ssana kwa trendi ya soko ku-fructuate kwa mazao na bidhaa zote.
   
 18. m

  mamakunda JF-Expert Member

  #18
  Feb 15, 2011
  Joined: Jul 4, 2010
  Messages: 371
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Hivi wewe umeshawahi kufika Kigoma? kwanza hakuna barabara ya uhakika inayounganisha mkoa wa kigoma na mikoa mingine,
  Haijaunganishwa na grid ya taifa ya umeme, ingawa wana ziwa tanganyika pale mjini penyewe maji ni ya mgawo umeme wala usiseme, wanawashangaa nyie mnavyosema umeme ni janga la kitaifa.
  Hata mkoa wa tabora ndo yale yale tu miundombinu mibovu pamoja na huduma mbalimbali,

  Kama alivyosema mjumbe mmoja aliyetangulia ni bora ya kunyamaza tu kama huelewi, Tanzania bara ni kubwa sana na sehemu kubwa hakuna maendeleo, Wenzetu tu wa kaskazini ndo walipata bahati hiyo.
   
 19. Mrembo

  Mrembo JF-Expert Member

  #19
  Feb 15, 2011
  Joined: Oct 9, 2008
  Messages: 392
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  cha kusikitisha, mikoa hiyo ndio ina wafuasi wengi wa Chama tawala
   
 20. Nyangomboli

  Nyangomboli JF-Expert Member

  #20
  Feb 15, 2011
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 2,312
  Likes Received: 651
  Trophy Points: 280
  una wapepo. wenzin mbona wanajikali mbeyi beach kweny majumba yashyoamilhka bure na hawana shida!?
   
Loading...