Ileje
JF-Expert Member
- Dec 20, 2011
- 8,758
- 12,174
Imekuwa mazoea spika Ndugai kuotoa maamuzi ya kisheria kwa kadri anavyojisikia.
Wakati Lipumba alipowafuta uanachama wabunge wa viti maalum wa CUF, Ndugai aliwafukuza wabunge wale bila kuhoji. Aidha CCM ilipomfuta uanachama Sofia Simba, alimfukuza ubunge bila kuhoji.
Cha kushangaza Mwambe alipojitoa CHADEMA na kujiuzulu ubunge na nyadhifa zake zote, Ndugai alimwita na kumruhusu aendelee na ubunge wake bila kuwa na chama cha siasa anachowakilisha. Aidha akina Rwakatare, Silinde, na Lijualikali walipofukuzwa uanachama CHADEMA Ndugai aliwaruhusu kuendelea na ubunge wao na akawahamisha viti bungeni na kuwaweka upande wa CCM!
Tabia na mazoea haya ya kukiuka katiba ya nchi, sheria na kanuni zake hayavumiliki hata kidogo. Ni muda muafaka taasisi zote za kisheria nchini ikiwemo Tanganyika Law Society kukemea vikali tabia hii ya Ndugai.
Ndugai anafanya hivi kwa makusudi kwa sababu anajua alikwisha jiwekea kinga ya kushtakiwa mahakama kwa hati ya dharula mwaka jana. Kinga ile itamfanya ajione yuko juu ya sheria hivyo ataendelea kusigina katiba kwa kadri anavyojisikia. Kuendelea kuendesha nchi bila kuheshimu katiba ni udikteta uliopitiliza.