Baada ya Spika Ndugai kuwalinda Wabunge 19 waliofukuzwa CHADEMA, ni wakati wa wanasheria kumuelimisha kuhusu kutii Katiba bila shuruti

Ileje

JF-Expert Member
Dec 20, 2011
6,911
2,000
Imekuwa mazoea spika Ndugai kuotoa maamuzi ya kisheria kwa kadri anavyojisikia.

Wakati Lipumba alipowafuta uanachama wabunge wa viti maalum wa CUF, Ndugai aliwafukuza wabunge wale bila kuhoji. Aidha CCM ilipomfuta uanachama Sofia Simba, alimfukuza ubunge bila kuhoji.

Cha kushangaza Mwambe alipojitoa CHADEMA na kujiuzulu ubunge na nyadhifa zake zote, Ndugai alimwita na kumruhusu aendelee na ubunge wake bila kuwa na chama cha siasa anachowakilisha. Aidha akina Rwakatare, Silinde, na Lijualikali walipofukuzwa uanachama CHADEMA Ndugai aliwaruhusu kuendelea na ubunge wao na akawahamisha viti bungeni na kuwaweka upande wa CCM!

Tabia na mazoea haya ya kukiuka katiba ya nchi, sheria na kanuni zake hayavumiliki hata kidogo. Ni muda muafaka taasisi zote za kisheria nchini ikiwemo Tanganyika Law Society kukemea vikali tabia hii ya Ndugai.

Ndugai anafanya hivi kwa makusudi kwa sababu anajua alikwisha jiwekea kinga ya kushtakiwa mahakama kwa hati ya dharula mwaka jana. Kinga ile itamfanya ajione yuko juu ya sheria hivyo ataendelea kusigina katiba kwa kadri anavyojisikia. Kuendelea kuendesha nchi bila kuheshimu katiba ni udikteta uliopitiliza.
 

Babati

JF-Expert Member
Aug 7, 2014
45,265
2,000
Huyu mzee ni chizi anatakiwa ashitakiwe kwa uhani kwa kosa la kuchezea katiba ya nchi.
 

Koryo2

JF-Expert Member
Nov 28, 2016
1,725
2,000
Kwa nini HADEMA wanajibizana na Mhe. Spika?. Kwa nini wasiende Mahakamani ili kupata HAKI juu ya Wabunge waliofukuzwa.
 

Kamakabuzi

JF-Expert Member
Dec 3, 2007
2,156
2,000
Bunge halali linaundwa na wabunge halali; na maamuzi yake yanakuwa hali kikatiba kwa kuwa Bunge lipo kikatiba. Sasa kama Bunge lina wabunge wasiokuwa halali kikatiba, then hata lenyewe halipo kikatiba kwa kuwa lina wabunge ambao kikatiba si wabunge! Na sheria wanazotunga na kupitisha, kwa kuwa zimepitishwa na wabunge wasikuwa halali, nazo zinakuwaje halali kikatiba?
 

Kiby

JF-Expert Member
Nov 16, 2009
6,317
2,000

Attachments

 • images-1.jpg
  File size
  6.7 KB
  Views
  0
 • IMG-20210503-WA0008.jpg
  File size
  58.9 KB
  Views
  0

Kamakabuzi

JF-Expert Member
Dec 3, 2007
2,156
2,000
Jaji Maige alisema jopo wamekubaliana na hoja za Mwanasheria Mkuu kwamba mlalamikaji amekosea kufungua kesi hiyo kwa kutumia ibara ya 26, bali alipaswa ajiegemeza katika ibara ya 83 ya Katiba ikiwa sambamba na kifungu cha 37 cha Sheria ya Uchaguzi.

Ibara hiyo inaelekeza utaratibu wa kuwasilisha malalamiko kama yaliyowasilishwa na mlalamikaji.
 

Ileje

JF-Expert Member
Dec 20, 2011
6,911
2,000
Jaji Maige alisema jopo wamekubaliana na hoja za Mwanasheria Mkuu kwamba mlalamikaji amekosea kufungua kesi hiyo kwa kutumia ibara ya 26, bali alipaswa ajiegemeza katika ibara ya 83 ya Katiba ikiwa sambamba na kifungu cha 37 cha Sheria ya Uchaguzi.

Ibara hiyo inaelekeza utaratibu wa kuwasilisha malalamiko kama yaliyowasilishwa na mlalamikaji.
Hii inahusiana vipi na Covid-19
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom