Baada ya soko LA filamu bongo kubuma, wasanii wameanza kutumia uwanja wa siasa kutafuta kiki.

Nibozali

JF-Expert Member
Oct 15, 2016
572
1,000
Kiukweli wasanii wetu tuwahurumie kwa sababu soko LA kazi zao kwa sasa siyo zuri, na kama mnavyofahamu msanii yeyote yule bila habari za hapa na pale za Mara kwa Mara zinazomhusu yeye lazima atapotea kwenye ramani.
Ukiangalia kwa sasa kazi zao zilizokuwa zinawafanya watrend kwenye ramani soko lake limebuma. Sasa wamebaki wanatumia uwanja wa siasa kutengeneza headlines. Mfano ni akina Wema Sepetu. Mtu kama Wema hana impact yoyote kwenye masuala ya kisiasa lakini utakuta na yeye anatumia uwanja huo kujitafutia kiki eti amehama chama ili tu na yeye a make headlines. Kusema ukweli ukiwa na wanachama miamoja kama Wema hawawezi kukisaidia chama chako kupiga hatua maana yeye mwenyewe tu alipo ni uchafu kwa skendo zake.

Ingawa umerudi kwenye chama chetu lakini sioni impact ya Wema bali naona tu alitaka kutrend kwenye vyombo vya habari maana kwa sasa Siasa ndiyo imekuwa mkombozi wa wasanii kuendelea kusikika coz kazi kwa SAS zimebuma

Ni hayo tu
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom