Baada ya siku 100: Tunapoachana kwenye Mataa na Rais Samia

Siyo hisia kaandika ukweli mtupu! Labda wewe ni mbunge ndiyo maana unaona hayakuhusu.

Kuna kaji orodha chao wakisikia katiba mpya, Chadema, Mbowe, Corona na tahadhari zake wanapagawa kwa kiwango kisicho mfano.

Tunaendelea kuihuisha orodha yao.

Hawana hoja bali maslahi yao binafsi tu.
 
Mama Samia huko uliko pokea salamu hizi.

Katika siku 100 zako za mwanzo ulianza vizuri ukitupa matumaini mapya nasi tukakupongeza. Lakini baada ya hizo kupita ghafla umetubadilikia.

Ama kwa hakika unayoyafanya sasa si mageni hapa duniani na huu wimbo unakuhusu:




"Neema alimwambia Chidumule yule bwana aliyezaa naye kaja. Hivyo asifike nyumbani kwake wala kazini asimfuate. Hata akimwona njiani asimsalimie."

Tuna habari kuwa wenzetu serikalini kwa gharama zetu, nyie na jamaa zenu tayari mmeshapata chanjo tena ile adimu kabisa ya Pfizer kwa gharama zetu.

Kwa kuchanjwa kwenu sasa Corona ni suala la historia. Kwani hata mkiambukizwa, kwamba mtahitaji hata kufika hospitali tu, uwezekano huo ni mdogo sana. Corona haiwahusu tena na kimsingi sasa kwenu Corona haipo.

Bila shaka mliyezaa naye sasa yupo. Kama ilivyo kuwa kwa Neema hamtuhitaji tena. Kwa vitendo na hata kwa maneno mmeonyesha hivyo:

1. Mmetuongezea mzigo wa gharama za maisha kwa kuongeza kodi za mafuta ya magari.
2. Mmetuletea tozo mpya kwenye miamala ya simu:


3. Vigogo nyie kulipa kodi tu hakuwahusu.
4. Kuna wabunge 19 kinyume cha katiba mzigo wa malipo yao mmeuweka kwetu.
5. Wizi wa pesa tunazokamuliwa kama ripoti kadhaa za CAG zinavyoonyesha umeamua kuufumbia macho.
6. Mashirika yanayozalisha hasara mnazotuvisha sisi unaendelea kuyakumbatia.
7. Wenzetu mnaendelea kupeana takrima za magari na majumba ya mabilioni ya pesa kwa gharama zetu.
8. Waraka huu sasa unatuhusu sisi, bila shaka mnapopanga kutuokotezea chanjo kanjanja zisizowahusu nyie:


9. Ninyi mnapotumbua kwa gharama zetu:


10. Sisi ni mwendo wa kugumia:


Kwani uzalishaji unaongezeka au umeongezeka? Vipi basi hata mkaongeze kodi na tozo mpya mpya kama kuna janga linalotuhusu sote, achilia mbali kutokudhibiti matumizi ya vilivyopo?

Tumekuelewa mama yetu. Yule bwana yupo. Hata njiani tukikuona hatutakusalimia.

Hiyo form ya chanjo ibadilishwe iseme hivi
" I will not hold any organization for any adverse events that may happen after being vaccinated"

Hii kwanza sio chanjo kama chanjo za kawaida imepewa jina la chanjo kwa sababu watu wasije kudai fidia kwa yatakayo tokea.

Pia ipo kwa majaribio.

Ni mawazo tuu
 
Hiyo form ya chanjo ibadilishwe iseme hivi
" I will not hold any organization for any adverse events that may happen after being vaccinated"

Hii kwanza sio chanjo kama chanjo za kawaida imepewa jina la chanjo kwa sababu watu wasije kudai fidia kwa yatakayo tokea.

Pia ipo kwa majaribio.

Ni mawazo tuu

Tatizo kubwa ni kuwa serikali ya JMT inatoa chanjo kinyume cha utaratibu. Kwani kabla ya mtu kuchanjwa ilipaswa kupimwa:

1. Blood Pressure
2. Sukari mwilini
3. Urefu
4. Maambukizi ya UVIKO

Hayo ni kwa mujibu wa maelekezo ya mtengeneza chanjo.

Yote hayo hayafanyiki na JMT inatoa chanjo. Kwanini basi kupanua uwanja hadi kwa organizations zingine?

JMT bado haina nia ya wazi ya kupambana na ugonjwa huu.

Umeona validity ya karatasi ilipo?
 
Back
Top Bottom