Baada ya Samia, Museveni kukutana, sasa Tanzania kuanza kununua sukari kutoka Uganda

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,267
5,367
280264405_708044270399042_9001829009166658956_n.jpg

Tanzania inatarajiwa kuanza kununua sukari kutoka Uganda ikiwa ni ishara ya kuashiria kulegea kwa moja ya migogoro ya kibiashara iliyodumu kwa takriban miaka mitatu.

Rais Samia Suluhu, katika siku ya kwanza ya ziara yake ya siku mbili Nchini Uganda alikubaliana na mwenyeji wake Rais Yoweri Museveni kwamba Kampala pia itaipatia nchi yake dawa za kupunguza makali ya VVU (ARVs).

Taarifa ya pamoja iliyotolewa baada ya mkutano wa viongozi hao Mei 10, 2022, Uganda itasambaza tani 10,000 za sukari ili kujaza pengo la uzalishaji Nchini Tanzania.

Ikumbukwe kuwa Tanzania ilipiga marufuku sukari kutoka Uganda mwaka 2019, ikisema sukari hiyo haikuwa ikizalishwa Uganda.

Uganda, kwa miaka mingi, imeilaumu Tanzania kwa kuanzisha vikwazo vingi visivyo vya ushuru ambavyo vimekwamisha biashara kati ya nchi hizo mbili.


Source: The Citizen
 
Itakuwa powa sana huenda hata Bei ikashuka, Rais nikama mlezi ktk familia na Ndivyo inavyotakiwa uhangaike huku na huko ili kuhakikisha vifaranga wako wanakula, nimpongeze Mama kwa hilo hakika Anaipanua diplomasia.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom