Baada ya Sakata la KIBITI kuisha:Serikali itangaze mapori Yote Kuzunguka DSM kuwa Mashamba ACTIVE

Utakuwa mji wa ajabu usio na msitu
tatizo liko wapi mkuu
Badala ya Miti pori sasa kuna Mikorosho...
Badala ya majani pori sasa kuna michicha,mihogo, mahindi...
ni mipango, sisi wengine tunabonyeza herufi tu huku kusogeza siku sio lazima yafanywe...
 
bado kuna watu wenye uwezo wa kuyafanya kuwa productive kwa capacity yao.
ndio maana nimezungumzia karibu na jiji maana kuna kila aina ya mtu na uwezo.

Masikini hafanyi soil anaysis, Masikini hawezi kuchimba kisima cha umwagiliaji,Masikini hawezi kusafisha hekari 10+ kwa mashine(Chain saw mfano), Masikini hawezi kufanya green housefarming, wengine hawana taarifa sahihi.
Mfano eneo hilo ni safi pia kwa kilimo cha korosho.
Kumbuka tanzania ni nchi ya 08 duniani kwa kuzalisha korosho.
na eneo lote nililosema inakubali na inawezekana Ila masikini anaweza asiweze pia labda akiwezeshwa.
Ni vizuri tuwape nafasi wanaojikongoja na wale wenye uwezo wa kwenda kwa mbio za farasi mkuu...

Nashukuru kwa mchango wako muruwa, kama umeona sehemu ya post yangu hapo juu nimesema kwa bajeti hii ya wizara ya kilimo huko bado kutaendelea kuwa pori la uhakika. Na kwq bahati mbaya sana wenye uwezo sio lazima wapende kuwekeza kwenye kilimo achia mbali kwenye hilo pori zito. Kuna sehemu zenye ardhi nzuri kama kaskazini, nyanda za juu kusini, kati nk wangalau watu wanawekeza na sio huko pwani jua linawaka toka saa 12 asubuhi mpaka saa 1 usiku. Halafu uchimbe maji ukutane na ya chumvi. Ili hilo pori lipungue ni kuwekeza kwenye viwanda tu. Vinginevyo serekali iache kuwaambia watu wakalime kisha kuja kulaliwa bei ya mazao yao waliyoyapata kwa shida.

Ww uko kinadharia zaidi na hilo sio ww tu bali ni hata viongozi wengi wanaohimiza wengine wakalime wakati wao wako ofisini na wakistaafu hawaendi kulima na hata wakilima wanaishia kupata hasara. Mwisho wanaomba wateuliwe kwenye bodi mbalimbali za umma.
 
mkuu hili ni jukwaa la siasa.
Hicho nimeweka kama kionjo cha kisiasa, kuonyesha jitihada za wanasiasa pia katika kuexplore agriportunities
ningeandika jukwaa mchanganyiko au biashara usingeona mifano ya hivyo.

sasa kama kuandika jukwaa la siasa mambo yanayohusisha wanasiasa kwa good faith ni kosa. Hapo inabidi upeleke mapendekezo kwa mkuu Melo na Timu yake jukwaa hili lifutwe...
Hukuelewa tulia mkuu. Hatukuzuii siasa hapa ila kwa vile una kitu Mungu kakuzawadia basi tumia hiyo zawadi kuelewa nachokimaanisha. Ndo hayo tu!
 
Back
Top Bottom