Baada ya Sakata la KIBITI kuisha:Serikali itangaze mapori Yote Kuzunguka DSM kuwa Mashamba ACTIVE

mitale na midimu

JF-Expert Member
Aug 26, 2015
10,158
2,000
Naamini Mungu atasikia kilio cha watanzania wengi na kupitia vyombo vyetu au njia yoyote ile Sakata la Kibiti kupita...

Kuna watu wanaposikia Pori hawawezi kuelewa hadi wapande daladala(Noah/Landlover/pickup ndio daladala za huko) moja Inatokea Bagamoyo mjini hadi Matipwili au kuendelea zaidi hadi Saadan kwa kukatia kona kijiji cha Makurunge Mkwajuni. Hapo utapita katikati ya Pori kubwa sana linalosemekana kuwa ni shamba la Muwekezaji ECOEnergy, wengine wanasema ni la Serikali ya zanzibar walipewa na Mwalimu enzi hizo, Wengine wananchi walijichukulia maeneo huko kabla ya kufurushwa na kuonekana ni wavamizi wajuzi wanajua.

Hapo katikati kuna vijiji visivyo rasmi kama Gama, Makaani, Number 4 n.k eneo hilo pia linavibandari vidogo vidogo visivyo rasmi.
Maeneo kama hayo ukilinganisha na mapori yote yanayozunguka jiji na yaliyoko mkoa wa pwani yafanyiwe utaratibu wa kuendelezwa kwa watu ambao wako tayari.

Kamwe asiachwe mtu anaejiita muwekezaji miaka mingi bila kupanda hata mpapai.

Pakichangamka pote huko kwa utaratibu mahususi hapata kuwa kivutio cha waarifu na kama maficho ya watu wenye nia ovu.

Zile miaka ya Mtu kusema anashamba hekari 500 kumbe ana Pori la hekari Miatano miaka karibu 20 bila kuwa na kitu sio sawa utakuwa unamiliki incubator na maficho ya waarifu.

nawapongeza pia CHADEMA kwa kuonyesha jitihada za kufanya msitu shamba huko bagamoyo sijui ni wapi na waliishia wapi na wanazalisha nini ila kwa hatua hiyo wanastahili kupongezwa...

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
187,548

Yapo malalamiko ya mashamba kuporwa yarudishwe, kodi za mazao zifutwe, mkaa waachwe wachome n.k halafu tuone kama damu itaendelea kumwagika
 
Automata

JF-Expert Member
Mar 3, 2015
2,262
2,000
umenena vema sana mkuu ila kwa ishu ya BALANCE OF NATURE lazima tuwe na mapori.Sema tu yanapaswa kuwekewa uangalizi makinifu
  • Huyu jamaa anataka tugawane ardhi yote leo hii, je tukigawana ikaisha 2050 vizazi vyetu vitatumia nini?
  • Si ungi mkono pendekezo lake, itafutwe njia mbadala
 
tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
30,884
2,000
kweli, ila maeneo mengi yanayopaswa kuwa mashamba pwani ni mapori
Mkuu huko pwani kusema utafanya shamba ni kupoteza nguvu, muda na fedha. Huko jua huwa ni kali sana kiasi kwamba mengi ya mazao hukauka haraka. Huko panahitaji uwekezaji wa viwanda zaidi lakini sio kilimo. Tatizo la viwanda ni wangapi wana uwezo wa kuvijenga, achia mbali nia ya kujengea huko Pwani? Kulingana na bajeti ya wizara ya kilimo ilivyo huko kutaendelea kuwa pori kubwa sana.
 
Automata

JF-Expert Member
Mar 3, 2015
2,262
2,000
Yapo malalamiko ya mashamba kuporwa yarudishwe, kodi za mazao zifutwe, mkaa waachwe wachome n.k halafu tuone kama damu itaendelea kumwagika
  • Au siyo waachwe wachome mkaa watakavyo then mvua zikikosekana tunaanza kulia ukame, njaa
  • Naunga mkono hoja ya kufutiwa ushuru wa mazao tena ni kwa Tanzania nzima ila si ku entertain uchomaji wa mkaa
  • Miti (Misitu/Mapori) ndio uhai, Bila misitu mvua hamna na mvua ikikosekana msururu wa wamatatizo unaibuka
 
mitale na midimu

JF-Expert Member
Aug 26, 2015
10,158
2,000
Mkuu huko pwani kusema utafanya shamba ni kupoteza nguvu, muda na fedha. Huko jua huwa ni kali sana kiasi kwamba mengi ya mazao hukauka haraka. Huko panahitaji uwekezaji wa viwanda zaidi lakini sio kilimo. Tatizo la viwanda ni wangapi wana uwezo wa kuvijenga, achia mbali nia ya kujengea huko Pwani? Kulingana na bajeti ya wizara ya kilimo ilivyo huko kutaendelea kuwa pori kubwa sana.
mkuu mbona huwa uko negative na kilimo sana mkuu.
ukienda kiwangwa ni pwani lakini mji wote ni mananasi na ni pwani.
sehemu nyingi tu kilimo kinakubali pwani...
 
Gama

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
10,831
2,000
  • Au siyo waachwe wachome mkaa watakavyo then mvua zikikosekana tunaanza kulia ukame, njaa
  • Naunga mkono hoja ya kufutiwa ushuru wa mazao tena ni kwa Tanzania nzima ila si ku entertain uchomaji wa mkaa
  • Miti (Misitu/Mapori) ndio uhai, Bila misitu mvua hamna na mvua ikikosekana msururu wa wamatatizo unaibuka
huyu anayependekeza mapoli yaondolewe hajui umuhimu wa mapori
 
Rweye

JF-Expert Member
Mar 16, 2011
16,383
2,000
T
Naamini Mungu atasikia kilio cha watanzania wengi na kupitia vyombo vyetu au njia yoyote ile Sakata la Kibiti kupita...

Kuna watu wanaposikia Pori hawawezi kuelewa hadi wapande daladala(Noah/Landlover/pickup ndio daladala za huko) moja Inatokea Bagamoyo mjini hadi Matipwili au kuendelea zaidi hadi Saadan kwa kukatia kona kijiji cha Makurunge Mkwajuni. Hapo utapita katikati ya Pori kubwa sana linalosemekana kuwa ni shamba la Muwekezaji ECOEnergy, wengine wanasema ni la Serikali ya zanzibar walipewa na Mwalimu enzi hizo, Wengine wananchi walijichukulia maeneo huko kabla ya kufurushwa na kuonekana ni wavamizi wajuzi wanajua.

Hapo katikati kuna vijiji visivyo rasmi kama Gama, Makaani, Number 4 n.k eneo hilo pia linavibandari vidogo vidogo visivyo rasmi.
Maeneo kama hayo ukilinganisha na mapori yote yanayozunguka jiji na yaliyoko mkoa wa pwani yafanyiwe utaratibu wa kuendelezwa kwa watu ambao wako tayari.

Kamwe asiachwe mtu anaejiita muwekezaji miaka mingi bila kupanda hata mpapai.

Pakichangamka pote huko kwa utaratibu mahususi hapata kuwa kivutio cha waarifu na kama maficho ya watu wenye nia ovu.

Zile miaka ya Mtu kusema anashamba hekari 500 kumbe ana Pori la hekari Miatano miaka karibu 20 bila kuwa na kitu sio sawa utakuwa unamiliki incubator na maficho ya waarifu.

nawapongeza pia CHADEMA kwa kuonyesha jitihada za kufanya msitu shamba huko bagamoyo sijui ni wapi na waliishia wapi na wanazalisha nini ila kwa hatua hiyo wanastahili kupongezwa...

Umeanza vizuri sema umeharibu kuweka siasa mwishoni. Hivi nyie watu katika huu utawala kwanini bado hamuelewi side impact ya kuhusisha siasa katika mambo fulani? Endeleeni na itawagharimu
 
mitale na midimu

JF-Expert Member
Aug 26, 2015
10,158
2,000
T

Umeanza vizuri sema umeharibu kuweka siasa mwishoni. Hivi nyie watu katika huu utawala kwanini bado hamuelewi side impact ya kuhusisha siasa katika mambo fulani? Endeleeni na itawagharimu
mkuu hili ni jukwaa la siasa.
Hicho nimeweka kama kionjo cha kisiasa, kuonyesha jitihada za wanasiasa pia katika kuexplore agriportunities
ningeandika jukwaa mchanganyiko au biashara usingeona mifano ya hivyo.

sasa kama kuandika jukwaa la siasa mambo yanayohusisha wanasiasa kwa good faith ni kosa. Hapo inabidi upeleke mapendekezo kwa mkuu Melo na Timu yake jukwaa hili lifutwe...
 
mitale na midimu

JF-Expert Member
Aug 26, 2015
10,158
2,000
huyu anayependekeza mapoli yaondolewe hajui umuhimu wa mapori
zaidi ya MISITU(ambayo mingi iko reserved), mbuga za wanyama, maeneo ya hifadhi hayo mapori yenye vichaka na ambayo hayapo kwenye ratiba za kuwa hifadhi sijui umuhimu wake labda usaidie umuhimu wa yale mapori mkuu.
 
tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
30,884
2,000
mkuu mbona huwa uko negative na kilimo sana mkuu.
ukienda kiwangwa ni pwani lakini mji wote ni mananasi na ni pwani.
sehemu nyingi tu kilimo kinakubali pwani...
Mkuu kilimo kimenitenda hivyo nakijua vizuri. Mtanzania mwenye maisha ya chini kabisa nchi hii ni mkulima. Hivi hujawahi kusikia hii kejeli inayosema kama kazi imekushinda kalime?

Kama hilo pori lingekuwa productive lisingekuwa hivyo ndugu yangu, ndio maana nikasema ishauri serekali ihimize ujenzi wa viwanda na sio mashamba yakawatie watu umasikini.
 
mitale na midimu

JF-Expert Member
Aug 26, 2015
10,158
2,000
Mkuu kilimo kimenitenda hivyo nakijua vizuri. Mtanzania mwenye maisha ya chini kabisa nchi hii ni mkulima. Hivi hujawahi kusikia hii kejeli inayosema kama kazi imekushinda kalime?

Kama hilo pori lingekuwa productive lisingekuwa hivyo ndugu yangu, ndio maana nikasema ishauri serekali ihimize ujenzi wa viwanda na sio mashamba yakawatie watu umasikini.
bado kuna watu wenye uwezo wa kuyafanya kuwa productive kwa capacity yao.
ndio maana nimezungumzia karibu na jiji maana kuna kila aina ya mtu na uwezo.

Masikini hafanyi soil anaysis, Masikini hawezi kuchimba kisima cha umwagiliaji,Masikini hawezi kusafisha hekari 10+ kwa mashine(Chain saw mfano), Masikini hawezi kufanya green housefarming, wengine hawana taarifa sahihi.
Mfano eneo hilo ni safi pia kwa kilimo cha korosho.
Kumbuka tanzania ni nchi ya 08 duniani kwa kuzalisha korosho.
na eneo lote nililosema inakubali na inawezekana Ila masikini anaweza asiweze pia labda akiwezeshwa.
Ni vizuri tuwape nafasi wanaojikongoja na wale wenye uwezo wa kwenda kwa mbio za farasi mkuu...
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom