Baada ya safari ya kilometa 458m, Roboti ya InSight Probe imefika kwenye sayari ya Mars

Dr Mathew Togolani Mndeme

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
201
808
Wale wenzangu wenye interest na elimu ya maumbo ya angani (Astronomy) na elimu ya chanzo, mabadiliko na hatima ya ulimwengu (Cosmology) siku nyingi tumekua kimya humu jamvini. Ngoja leo niandike kidogo baada ya historia nyingine kuwekwa jana katika elimu ya sayansi ya safari na elimu ya maombo ya angani kuwekwa jana usiku.
1543319255634.png

Figure 1: Namna Chombo cha InSight Probe kitakavyofanya kazi juu ya Mars (Chanzo NASA)

Masaa kadhaa yaliyopita roboti/ chombo cha tafiti za angani (Spacecraft) kinachoitwa Interior Exploration using Seismic Investigations, Geodesy and Heat Transport (InSight) Probe kimetua kwa mafanikio kwenye sayari ya Mars. Safari hii ilianza ramsi miezi sita na nusu iliyopita siku ya tarehe 05/05/2018 na imekua ya umbali wa kilometa milioni mia tano na hamsini na nane (458M kms) ikiwa ni wastani wa mwendokasi wa kilometa 10,000 wa lisaa. Umbali huu ni sawa na safari 600 kwenda na kurudi toka mwezini au safari 11,430 za kuzunguka dunia. Maandalizi ya safari hii na chombo hiki imetumia miaka kumi na iumejumuisha wanasayansi wa fani mbalimbali kwa ushirikiano wa nchi nane wakiongozwa na taasisi ya NASA ya Marekani.

InSight Probe inaungana na vyombo vingine viwili ambavyo tayari viko kwenye sayari ya Mars (chombo cha Opportunity kinachofanya general exploration ya Mars tangu mwaka 2004 na Curiosity kinachofanya tafiti za kimaabara wa geologia na uwezekano wa kuwepo mazingira ya uhai tangu 2012). InSight Probe yenyewe pamoja na tafiti zingine, itajikita katika kuchunguza na kutafiti muundo wa ndani (internal structure) wa sayari ya Mars. Hii ni pamoja na kupima uwepo wa matetemeko, kiwango cha joto ndani ya sayari, na iwapo ndani ni kimiminika au ni miamba pekee na ni ya aina gani.
1543319289416.png

Figure 2: Chombo cha InSight Probe kitakavyofanya kazi (Chanzo NASA)

Nini ni cha kipekee kuhusu InSight Probe?
Tofauti na mission nyingine zilizotangulia za sayari ya Mars na maumbo mengine ya angani, kinachovutia kuhusu InSight Probe ni teknolojia iliyotumika kurusha roboti hii. Teknoloji ahii ndio imetumika kwa mara ya kwanza. Moja ya changamoto kubwa zinazokabili safari za angani na vyombo vinavyotumwa kufanya tafiti ni muda wa mawasiliano kutoka vilipo hadi duniani. Vyombo hivi vinatunama taarifa kutoka huko na pia taarifa hutumwa kutoka duniani kama vile kuvipa maelekezo ya nini cha kufanya, kubadili mwelekeo, kubadili mwendokasi, kuviepusha na majanga, na kufanya updates za software. Baadhi ya vyombo hutumia masaa na vingine siku/wiki/miezi kwa data kusafiri kati ya huko viliko na duniani. InSight Probe imefanikiwa kutatua tatizo hili kwa kuwezesha taarifa (data / signals) kutumwa na kufika muda huohuo (real-time communication).

1543319325373.png

Figure 3: Safari ya Insight Probe toka duniani hadi Mars

Kikubwa kilichofanyika ni chombo hiki kurushwa kikimbatana na satellite/vyombo vingine viwili vidogo (microsatellites) vijulikanavyo kama Mars Cube One (kwa kifupi MarCO) vyenye size ndoka mithili ya briefcase. Ili kuharakisha na kurahisisha mawasiliano, Satellites hizi vinawasiliana kwanza na InSight Probe huko juu kisha navyo vinawasiliana na vituo vya mawasiliano ya anga (deep space stations) zilizoko duniani. Spacecraft (Atlas V 401) iliyorusha roboti ya InSight Probe iliviachilia vyombo hivi mara baada ya kuruka na vikasafiri vyenyewe kuelekea Mars wakati InSight Probe inaendelea na safari ya kuingia katika anga la Mars. MarCo Cube One A and B hazijaenda kutua kwenye Mars kama InSight Probe bali vyenyewe vinazunguka kwenye orbit ya sayari kwa ajili ya kufanikisha mawasiliano. Kwa mara ya kwanza, MarCo zimewezesha kuingia kwa chombo katika sayari ya Mars and kutua (entry and landing) huku taarifa (signals) zikipatikana moja kwa moja duniani. Pia picha za awali zilirushwa duniani mara tu baada ya kutua na kupokelewa. Haya ni mafaniko makubwa sana.
1543319355013.png

Figure 4: Mars Cube One (A and B) vikionesha antenna za mawasiliano (Chanzo NASA)

Nini kinafuata?
Baada ya InSight kutua kinachofuata na kile wanachoita deployment, yaani kukiweka tayari ili kuanza kazi yake ya utafiti. Wakati zoezi la kuingia na kutua kwenye sayari linakua automatated wakati chombo kinatengenezwa, deployment na mazoezi mengine ya utafiti yatakayoendelea yatafanyika kwa ushirikiano na wanayansi walioko duniani (control station).

Kufanikiwa kwa InSight Probe kutua kwenye sayari ya Mars kutabadilisha kabisa safari zingine za anga za mbeleni. Pia itasaidia sana katika maandalizi yanayoendelea ya kupeleka kinachoweza kwenda na kurudi kutoka Mars (space rocket) mradi unaotegemewa kufanikiwa ndani ya miaka mitano hadi kumi ijayo. Pili itasaidia maandalizi ya kupeleka watafiti kwenda Mars na kurudi safari ikiwa ni mara ya kwanza kwa binadamu kufika kwenye sayari nyingine nje ya nyumbani kwetu duniani.
1543319385525.png

Figure 5: Timu ya wanasayansi waliofanikishwa uundwaji na uaandaaji wa safari (Chanzo NASA)

Tahadhari
Hata hivyo ni mapema kushangilia sana kilichofanikiswa maana kutua kwenye sayari ni jambo moja na kufanya kazi iliyokusudiwa ni jambo lingine. Huko nyuma kumewahi kuwa na mission zingine za Mars ambapo vyombo vilifanikiwa kutua lakini vilishindwa kufanya kazi iliyokusudiwa na kufa. Hata hivyo kwa ubora wa teknolojia iliyotumika, kuna matumaini makubwa kwamba chombo hiki kitafanikisha yaliyokusudiwa.

Kuna mengi ya kuzungumzia kuhusu chombo hiki, safari yake na kazi itakayofanya ila niishie hapa nisikuchoshe wewe msemaji.

Imaandikwa na Mwalimu MM (mmmwalimu@gmail.com)

https://edition.cnn.com/2018/11/26/world/nasa-insight-mars-landing-today/index.html

Tatizo tunaingilia matakwa ya Mola,

Loh. Umenifurahisha ndugu yangu. Mungu hana ugomvi kabisa na sayansi. Yeye ndio chanzo cha hekima, elimu na maarifa yote. Kuweza kufikisha vyombo vya kibinadamu angani ni moja ya miujiza aliyoiweka ndani yetu ili tujue ukuu wa uumbaji wake, tushangae uweza wake na mwisho wa siku tumheshimu na kumwabudu yeye pekee
 
Najaribu kuiwaza km 10000/h kwa chombo chenye uzito inafananaje.maana ule mwendo wa jet fighter huwa hauzidi 1500km/h.

Dah msungu sio.
I would avoid the word "mzungu" and limit myself to the wonders of science and technology. Knowledge/ science goes far beyond the racial boundaries and skin colours. Any intelligent person or community passionate about science and its application...and when put in a supportive/conducive environment.. and resources made available... can do anything and even the sky will not be a limit. You will be surprised that some of the key engineers in this project are people of colour (men and women)
 
Wala sina tatizo kwa hilo,ila kwa sasa wacha tuwapongeze walithubutu wakaweza kwanza.
 
Asante mtoa post lakin Nishawahi skia eti NASA wamefanya uchunguzi na kugundua kuwa binadamu anaweza kuishi huko Mars bila shida yoyote.. sasa je? Bado hawajamaliza huo uchunguzi wao mpka leo .. au hzo habari zilkua za uongo?
 
NASA hawajawahi kusema hivyo. Uchunguzi unaofanyika swali la msingi la kisayansi wanalojaribu kujibu sio kutizama iwapo mwanadamu anaweza kuishi bali wanatizama uwezekano wa sayari hiyo ku-support maisha. Je kuna mazingira yanayo-support viumbe hai? Na kama yapo ni ni yepi na ni viumbe wa aina gani wanaishi au wamewahi kuishi humo? Kwamba hiyo life itakua ni mwanadamu, au wadudu, au mimea, au wanyama, au uwepo tu wa maji (H2O), au viumbe wengine wageni tusiowajua, hilo litakua ni jambo jingine.

Hadi sasa hypothesis inayotumika ni kwamba kumewahi kuwa na uhai kwenye sayari ya Mars. Kuna sababu kadhaa ila mojawapo ni ukweli kwamba uso au ardhi ya Mars unaashiria uwepo wa geological features za kwamba kumewahi kuwa na maji (mfano mabonde na ile mifereji inayobaki eneo ambalo mto au mafuriko yamewahi kupita). Vyombo vitatu vilivyoko huko (Curiosity, Opportunity na InSight Probe) pamoja na satelites kadhaa zinazoizunguka sayari hiyo vinaendelea kukusanya data na hivyo huenda mengi yakajulikana siku za karibuni.
 
Asante mkuu, hii ni taarifa njema,
 
Ni fuel au source energy gani iliyotumika kukisafirisha chombo hicho
Engine yake inauwezo mkubwa sana bila shaka maana kusafiri kilomita 10,000 kwa saa siyo mchezo
 
Ni fuel au source energy gani iliyotumika kukisafirisha chombo hicho
Engine yake inauwezo mkubwa sana bila shaka maana kusafiri kilomita 10,000 kwa saa siyo mchezo
In space kitu kikiwa kwenye motion kitaendelea kuwa kwenye motion mpaka itokee nguvu ya kukizuia, therefore chombo kikisha toka duniani kikawa anga za juu kikiwa na speed flani hata ukizima engine kitaendelea kukimbia kwa speed hiyo hiyo kwakuwa hakuna gravity wala friction
 
Nimeangalia hizo videos hapo,hakika Africa hatuna chetu duniani kama kweli haya mambo yanafanyika.

Sisi tubaki tu kudanganyana ila mzungu siyo binadam wa kawaida,kubali au kataa hawa wana kitu special wamepewa.
 
9 Reactions
Reply
Back
Top Bottom