Baada ya Sabaya, waliompiga risasi Lissu wajue na wao iko siku wataenda jela

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,013
144,371
Moja ya funzo kubwa tunalopata kutokana na hukumu ya Sabaya ni kuwa, hata ukitumika na wakubwa ,ipo siku hawatakuwapo na hata wakiwepo, wanaweza wasiwe na msaada kwako hivyo yatakukuta tu kama yalivyomkuta Sabaya leo hii.

Mliomshambulia Lissu kwa risasi mkoani Dodoma,, mjue siku yenu ipo na inakuja na mtawajibika kwa matendo yenu bila kujali mtamtaja nani mbele ya Pilato kuwa ndie aliewatuma. Mwenzenu alitaja watu/mtu fulani lakini haijamsaidia hivyo bado nyie.

Hata waliomua Raisi wa zamani wa Burkina Faso, Thomas Sankara, miaka mingi iliopita,leo wanapandishwa kizimbani kujibu mashitaka.

Tuombe uzima tu.
 
Unaota wewe, kwa upelelezi upi ama mahakama zipi?

Hili la sabaya limetumika kisiasa tu tangu lini hizi mahakama zimeanza tenda haki
 
Unaota wewe, kwa upelelezi upi ama mahakama zipi?

Hili la sabaya limetumika kisiasa tu tangu lini hizi mahakama zimeanza tenda haki
Hata.kipindi like Sabaya yuko ofisini,watu wasingeweza kuamini kuwa kuna siku atakwenda jela, hivyo sio kosa lako bali unathibitisha tu udhaifu wa mwanadamu kutokujfunza kurokana na yaliyotangulia.
 
Hata.kipindi like Sabaya yuko ofisini,watu wasingeweza kuamini kuwa kuna siku atakwenda jela, hivyo sio kosa lako bali unathibitisha tu udhaifu wa mwanadamu kutokujfunza kurokana na yaliyotangulia.
Unafahamu nafasi ya kukata rufaa imeachwa wazi, Basi udhaifu huu nao uko kwako kwa kuamini sabaya ataishi jera miaka 30
 
Kati ya utetezi mbovu mahakamani kuwahi kutokea, huu wa sabaya utabaki on top

Apunguziwe adhabu ya makosa ya ukatili wa kupiga watu, unyang'anyi, ubakaji, utakatishaji fedha kwa utetezi wa kua amelipia mahari mwanamke na anahitaji kuoa, seriously?

Aisee hao mawakili walikua na namna nyingi ya kumpiga hela tena kwa mbinu nyingi lakini sijui kwanini walichagua hii?
 
Back
Top Bottom