Baada ya RC Mwanza kuzuia Kongamano la Katiba kutokana na COVID-19, tunaamini onesho la muziki la Fally Ipupa pia litazuiwa kwa sababu hizo hizo!

M-mbabe

JF-Expert Member
Oct 29, 2009
13,203
23,020
RC wa Mwanza jana katangaza kuwa kuanzia leo, mikusanyiko inayoruhusiwa jijini Mwanza ni ile inayouhusiana na ibada na misiba ili kuzuia kusambaa kwa maambukizi ya korona.

Assume yupo sahihi kuwa imekuwa proved scientifically maambukizi ya korona hayawezi kutokea ibadani na misibani.

Sasa, kuna hili onesho la mwanamuziki Mkongomani lililopangwa kufanyika tarehe 24 mwezi huu jijini humo humo. Wanaoratibu maandalizi ya hili onesho inawezekana labda hawajapata taarifa ya zuio la jana kutoka kwa RC kwani naona wanaendelea na maandalizi kama kawaida na wanaongea with confidence kabisa kwamba mamlaka tayari imekwisha toa kibali cha onesho hilo kufanyika.

Hapa sijaoengelea mikusanyiko mengine ya kwenye viwanja mbalimbali vya michezo - kwani leo kuna mechi za mpira wa miguu zinaendelea kufanyika hapa jijini bila ya zuio lolote.

Ushauri wangu kwa serekali ya Rais Samia - ihakikishe haki inatendeka na ionekane inatendeka miongoni mwa makundi yote ya raia wa Tanzania bila ubaguzi wa aina yoyote.
Vinginevyo Mungu anaweza kuchukizwa na hivyo kulazimika kuishushia nchi yetu pigo jingine.

Ukiachia divine intervention, serekali pia inatakiwa ikumbuke kuwa political harmony and stability kwenye taifa lolote like ni very critical katika kuvutia uwekezaji wa sekta binafsi, hususani ile inayohusiana na mitaji kutoka nje ya nchi.

Bado Rais Samia hajachelewa sana katika hili - anayo nafasi ya kurekebisha before it is way too late!
 
Hii nchi tatizo ni CCM sio katiba mpya wala JPM!!! Kuna wakati unatamani kila chama kingekua na Armed wing ili muwe na fair ground ya kupambana. Kushindana kwa hoja na chama chenye jeshi ni kupoteza muda tu.
 
Back
Top Bottom