Baada ya RC Makonda kutoa saa 24 kwa Wabunge walioko Dar: Jeshi la Polisi lawataka Wabunge walioko Dar kuripoti Kituoni

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar, limesema baada ya RC Makonda kutoa saa 24 kwa Wabunge walioko jijini humo kurejea Bungeni, limewataka wale ambao bado hawajaondoka, kuripoti kwa hiyari yao katika ofisi ya Upelelezi, Kanda Maalum kwa mahojiano

View attachment 1442715
Sioni tatizo katika barua hii. Ni wito wa 'mahojiano' tena kwa 'hiyari' ya mhusika. Hiyo ndiyo busara ya Simbachawene.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kongwa? Kwanini kusiwe na maendeleo hata Kama chadema haipo,kwani serikali inatekeleza ilani ya chadema au ya CCM? Ilani ya CCM ndio inayotumika sio kongwa tu hata Jimbo la HAI, na chadema iwepo isiwepo hakuna kinachozidi Wala kupungua, halafu chadema haionewi ila inatafuta kiki zisizo na faida utavunja vipi Sheria halafu usichukuliwe hatua kisa tu wewe ni chadema?

View attachment 1442959
Huyu mzee kashageuka kabisa

Ova

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wanasiasa wengine wanapewa vyeo vinavyo wazidi uwezo wao. Wanaendelea kuaibisha waliowateua.
 
Hili la mkuu wa mkoa kutoa tamko la kukamata wabunge wa upinzani waliopo Dar hali ya kuwa halipo popote ndani ya katiba ni jambo la kusikitisha sana, ifike hatua uteuzi unapofanyika utengwe muda wa kupeana ABC kuhusu mipaka ya mteuliwa na kuelezana machache kuhusu sheria.Huenda shida ilitokea baada ya kufuta semina elekezi na mkuu pale aliposema hakuna semina elekezi watakwenda kuelekezana huko huko kazini.
 
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar, limesema baada ya RC Makonda kutoa saa 24 kwa Wabunge walioko jijini humo kurejea Bungeni, limewataka wale ambao bado hawajaondoka, kuripoti kwa hiyari yao katika ofisi ya Upelelezi, Kanda Maalum kwa mahojiano

View attachment 1442715
kwa sasa Taifa letu linapambana na pandemic mbili; COVID19 na Upumbavu
 
Ngoja tuone nani ataenda. Wabunge wengi wa CCM na mawaziri wapo mjini wakizunguka tu. Polisi hawana mamlaka ya kumsummon mtu kwa matamko tu ya kisiasa as long as mtu hajavunja sheria yoyote.

Mtu wa kudeal na Wabunge ni Speaker na tayari keshatoa maagizo ya kwamba hawa watu warudishe fedha za posho walizolipwa kabla hawajaamua kuji-isolate
Hawa hapa;
1. Mbunge Victor Mwambalaswa
2. Mbunge Andrew Chenge
3. Mbunge Hussein Mwinyi
4. Mbunge Julian Shonza
5. Mbunge Palamagamba Kabudi
6. Mbunge Steven Masele
7. Mbunge Mkuchika George
8. Mbunge Mtulia
Inaaminika hawapo Bungeni lakini wanachukua “per diem” kama kawaida.
 
Back
Top Bottom