Ngaliba Dume
JF-Expert Member
- Oct 6, 2010
- 1,710
- 3,669
Baada ya Mkuu wa mkoa wa Dsm kuibuka na kusema kuwa ameagiza mtaa uitwe jina la Kardinal Pengo,mchambuzi wa Historia na nguli wa mambo ya uhifadhi wa habari za harakati za Uhuru,Sheikh Mohamed Said ameibuka na kusema hakuna mahali ambapo katika historia ya nchi hii kanisa katoliki wakiwemo Mapadre na maaskofu waliombea uhuru upatikane haraka.
Mzee Mohamed Said anasema katika mikutano yote ya TANU nchi nzima,ni Sheikh Takadiri pekee ndio alizunguka na Nyerere na kuomba dua kabla na baada ya kila mkutano.Mzee Said anasisitiza kuwa hata katika hotuba zake,Nyerere mwenyewe alikiri kukaa na kufunga na Wazee wa Kiislam ili kuombea Uhuru upatikane haraka,na wala hakukuwa na mahali ambapo Mapadre au Maaskofu walionekana kuambatana na Nyerere katika harakati za Uhuru.
Kisa cha Nyerere Bagamoyo kuombewa dua na wazee wa Kiislam na kuchinja mbuzi,ni moja ya uthibitisho wa wazee wa kiislamu wengi wakiwa masheikh kuunga mkono harakati za uhuru na sio mapadre wala maaskofu.
Mzee Said anasema kura 3 iliyofanyika Tabora ambapo ilimuondoa jemedari wa Siasa za TANU Sheikh Zubeir Mtevu ndio ulikuwa mwanzo wa kuuzika mchango wa Waislamu katika harakati za uhuru,na baada ya Uhuru Nyerere aliwaweka kando wazee wote wa Kiislam na kuwajumuisha wakristo ambao hawakuwa na mchango wowote katika siasa za kudai Uhuru.
Huyu Zubeir Mtevu ndio alitumwa Mafia na Nyerere kwenda kueneza TANU,maana kwa aina ya watu wa MAFIA kisiwani,Nyerere alijua hataweza kuingia na kukubalika.Mzee Said anasema hali hii ya kuwaondoa masheikh na kuingiza wengine ilishagunduliwa na Sheikh Takadiri na kuna siku alishawahi mnyooshea Nyerere kidole mbele za watu kuwa kuna dalili baada ya uhuru akawatenga wazee wa Kiislamu na kuingiza watu wake ambao hawakutoa mchango owowte katika harakati za Uhuru.
Hii hoja ya Mzee Mohamed Said inakuja baada ya Makonda kusema kuwa ameagiza Kardinali Pengo apewe mtaa Dsm kwa mchango wake,sasa bingwa huyu wa Historia anajenga hoja,ni mchango upi alioutoa Pengo katika nchi kuwashinda watu kama Zuberi Mtevu,Mshume Kiyate,Sheikh Katadiri na wengine ambao mpaka leo hawajaenziwa??