Baada ya RC Arusha kumkimbia Lema Leo,RPC aingiza siasa Msibani,Lema anyimwafursa ya kutoa salamu,

Confederate Spy

JF-Expert Member
Sep 6, 2012
426
144
Leo ilikua siku ya kuaga mwili wa askari wa usalama barabarani aliyepata ajali maeneo ya New Sokoine Road. Katika zoezi hili la kuaga mwili wa Marehemu Mbunge wa Arusha Mjini Mh.Godbless Lema alikuwepo na MC alitangaza ratiba kuwa muwakilishi wa wananchi na kiongozi pekee aliyekuwepo Godbless Lema ataongea kutoa salamu za rambirambi.

Pia alitangaza kuwa Mkuu wa Mkoa na RPC walikua njiani kuja mahali hapo lakini alifika RPC pekee na Mkuu wa Mkoa aliingia mtini.Umati uliokuwepo ulipigwa na butwaa baada ya kuona MC anabadili utaratibu wote uliokuwepo na miongoni mwa viongozi waliotoa salamu za Rambirambi jina la Mbunge wao Godbless Lema halikuwepo.Ratiba ilibadilika baada ya MC kuitwa na Kamanda wa polisi wa mkoa na kumpa maelekezo yalioliengua jina la mbunge wa Arusha.

WAOMBOLEZAJI WACHACHAMAA:

Waombolezaji walinung'unika sana na hapa kuna mjadala mkali. Ni jambo la ajabu sana kuona viongozi wa jeshi la polisi wanaingia katika fitna za kisiasa na hasa mkoa wa Arusha ambako jeshi hili linatumika na viongozi wa kisiasa. Mzee mmoja alijikuta akipaza sauti ‘Vipi Mbunge wetu'? Polisi acheni siasa,tena mnafanya siasa msibani?

MH.GODBLESS LEMA ATOA RAMBIRAMBI SH.500,000/=

Hata hivyo Mh.Godbless Lema alitoa Rambirambi ya Sh.500'000. Alitoa laki 3 kwa ajili ya majeruhi walioko hospitali hadi muda huu na Sh.Laki 2 kwa familia ya traffic aliyefariki.

MKUU WA MKOA ATIA AIBU

Mkuu wa mkoa baada ya kugundua Mh. Lema yupo eneo hilo aliishia kwenye parking na kugeuza. Wananchi waliangua kicheko baada ya kutafsiri kitendo hicho kama njia mojawapo ya kumkimbia Mh.Lema. Mkuu wa mkoa alisikika akiwaambia maofisa walioenda kumpokea kuwa ‘Nimepata dharura,nitarudi kabla shughuli haijamalizika'

My Take: Sijui kwa siasa hizi na utendaji huu wa jeshi la polisi Arusha chini ya RPC Sabas tunaupeleka wapi mkoa huu? Aibu walizotia leo mkuu wa mkoa na kamanda Sabas zimewafanya wadharaulike sana na wananchi.
 
Rasimu ya Katiba Mpya ilitakiwa kufuta
Cheo cha RC hawana lolote hao zaidi ni
majungu na fitna tu.
 
RC alikuwa hajajiandaa cha kuongea in the presence of Kamanda Lema hahaaaaaaa ...........
 
Lema amewakaa shingoni hao wasudu policcm na rc wao. Bahati mbaya kwao ni kwamba wananchi wengi sana wa Arusha wako bega kwa bega na mbunge wao hata wasipompa nafasi ya kuongea msibani, wananchi watamsikia mahali kwingine.
 
Lema amewakaa shingoni hao wasudu policcm na rc wao. Bahati mbaya kwao ni kwamba wananchi wengi sana wa Arusha wako bega kwa bega na mbunge wao hata wasipompa nafasi ya kuongea msibani, wananchi watamsikia mahali kwingine.
Wananchi walichachamaa leo hadi Aibu.Wamejidhalilisha sana.Hadi Muda huu hapa maeneo ya Kwa Mromboo wananchi wanajadili hili na kulaani sana tukio la leo..Mkuu mwita,karibu kiwanja hiki tupate nyama choma kama upo Arusha.Hali ya hewa leo inaruhusu sana huku Arusha
 
Lol Mh Godbless Lema ni Kamanda wa ukweli yaani serikali yote inamuogopa Arusha ndio kaishika hakunaga,Lema ni jembe kweli kweli.Hadi Policeccm wanaamua kubadilisha ratiba!!Mungu muongezea Mh Lema ulinzi na maisha marefu hawa ndio viongozi tunaowahitaji.
 
Lema amewakaa
shingoni hao wasudu policcm na rc wao. Bahati mbaya kwao ni kwamba
wananchi wengi sana wa Arusha wako bega kwa bega na mbunge wao hata
wasipompa nafasi ya kuongea msibani, wananchi watamsikia mahali
kwingine.

Mbona hueleweki ww? Kwani Lema akwenda kuuaga mwili wa POLICDM?
 
inawezekana Rc alitaka kupigia wagombea udiwani wa Maccm KamPeni Kwenye msiba so alipomuona kamanda Lema tuMbo likachafuka
 
Kwa kweli ni ujinga lakini imethibika kwamba ukiwadhalilisha wapinzani unapanda cheo kwa hiyo hiyo no kazi njema kwa polisi na rc
 
Duh Ndiyo maana jamaa tangu mwaka juzi hoja yangu ni kuwa tui-disband police force.Ni police service,ni huduma kwa jamii kuliko ilivyo hivi sasa.Hivi Kamanda wa Police wa Mkoa mbona amejidhalilisha hivi?Nimeona habari hizi kwenye mitandao ya kijamii.Hii ni aibu kubwa sana.Huyo mkuu wa Mkoa ndiyo katia aibu kabisa,kujificha nyuma ya magari na kusema kwamba umepata dharura huku ukijua si kweli na wananchi wameshtukia ni fedheaha ya mwaka
 
Ujinga kabisa huu unashindwa kutimiza majukumu yako kkwasababu ya mtu, haha hafai hata kuwa iongozi wa watu
 
Duuuuuuuu! Aisee sasa hii ni kali. Ila ninamshauri RPC kutofanya siasa ambayo haiwezi na kwa hakika hata yeye analijua moyoni kwa hapa Arusha hawezi kupambana na kamanda Lema japokuwa yeye anamiliki silaha za moto na jeshi la polisi lakini mh Lema anao watu kwa maelfu wanaomsikiliza na kutii kwake kutokana na uongozi wake usio na HILA moyoni.

Ushauri wangu!
RPC acha kutumika na kuingilia mgogoro usiokuhusu na umwachie RC ambaye ni mjumbe wa kamati ya siasa wa ccm mkoa wa Arusha ambaye inafahamika kabisa ameletwa hapa Arusha kumzibiti mh Lema na Lowassa katika harakati zao za kisiasa. La sivyo utalihatarisha jeshi la polisi maana wana Arusha kama unavyowajua hawaogopi risasi za moto na nakusihi ujaribu kupitia majalada ya RPC waliokutangulia ili uweze kuijua vizuri historia ya wananchi wa Arusha mambo wanayoweza kuyafanya hata kama yatahatarisha uhai wao kwa kiongozi wanayempenda kama kamanda Godbless Lema.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 

Similar Discussions

1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom