Baada ya Rais Samia kutaja neno DEMOKRASIA makofi yalipungua, kwanini?

pakaywatek

JF-Expert Member
Dec 28, 2014
4,636
6,261
Ukifatilia hotuba Rais bungeni aligusia mambo mengi na wabunge walipiga makofi kama yote, lakini aliposema Uhuru na Demokrasia ni msingi wa amani katika nchi makofi yalipungua sana.

Labda CCM hawaamini kuwa madarakani bila kuminya Demokrasia? Hau wabunge wengi wanajua mpira ukiwekwa na refa akiwa huru wengi hawatarudi bungeni?

Nawasilisha.

Samia.PNG
 
Hayo ni maneno tu kaongea,Rais pia ni mwanasiasa.
Rejea haya maneno"hata wote mkichagua upinzani bado CCM itashinda"
Angevunja Bunge ngoma iwekwe kati irudiwe hapo ndo ningeamini.
Au angesemema wazi anaanza katiba mpya na tume huru.
 
Kwahiyo leo unajileta upande ambao hukuwahi kuuamini, ama ujumbe wako ni upi hasa.
 
Wajumbe bado tuna endelea kuwamind wote waliopitishwa kimazabe na mwendazake
Nalog off
 
wabunge wengi mle ndani wanajijua hawakupatikana kidemokrasia, so ni wazi kabisa hawatapenda neno hilo...hata kama ingekuwa ni wewe, ni sawa na mtu anayetaka kuchafua kitumbua chako kwa mchanga!!!.
 
Nyie wasomi inabidi mjifunze kuwa mitazamo ya watu iko very complex. Msijidanganye kuwa kila mtu ni shabiki wa hiyo demokrasia. Mwaka 92 asilimia 80 ya watanzania waliikataa demokrasia.

Kama mnatumia akili zenu hiyo ni meseji tosha kwamba kama ambavyo nyinyi mnaianini demokrasia tupo pia ambao hatutaki hata kuisikia.

Najua kwa usomi wenu mnatuona wajinga tusioelemika ila ukweli ndiyo huo. Kila mtu yuko huru kufikiri anavyotaka.

Kwanza katiba yetu inasema nchi yetu ni ya kijamaa. Ujamaa na demokrasia wapi na wapi? Ndiyo maana mlipewa demokrasia kwenye makaratasi. Kwenye uhalisia tunaendesha nchi kwa kufuata katiba inavyosema: ujamaa.
 
Mkuu, muda si mrefu utajua hujui..

Kwa mazingira ya sasa, kuendesha nchi kimabavu, kiimla na kidikteta siyo endelevu.

Na ndo sabb mwendazake (Rip) alilazimika kutawala kwa kutumia mbinu batili kama utekaji, kupoteza watu, kubambikizia kesi za uongo wasio na hatia, nk. Siyo kila mtu anaweza kufanya hivyo!
 
Ukifatilia hotuba Rais bungeni aligusia mambo mengi na wabunge walipiga makofi kama yote, lakini aliposema Uhuru na Demokrasia ni msingi wa amani katika nchi makofi yalipungua sana.

Labda CCM hawaamini kuwa madarakani bila kuminya Demokrasia? Hau wabunge wengi wanajua mpira ukiwekwa na refa akiwa huru wengi hawatarudi bungeni?

Nawasilisha.

View attachment 1761474
Walihisi labda neno linalofuata ni kuvunja bunge ili turudi kwenye uchaguzi huru na haki ndiyo maana walitegea kupiga makofi!
 
Ukifatilia hotuba Rais bungeni aligusia mambo mengi na wabunge walipiga makofi kama yote, lakini aliposema Uhuru na Demokrasia ni msingi wa amani katika nchi makofi yalipungua sana.

Labda CCM hawaamini kuwa madarakani bila kuminya Demokrasia? Hau wabunge wengi wanajua mpira ukiwekwa na refa akiwa huru wengi hawatarudi bungeni?

Nawasilisha.

View attachment 1761474
Kumbe wengi waliona hili, hilo ndilo jambo chungu zaidi maskioni mwa wabunge wa ccm.
 
Back
Top Bottom