Baada ya Rais Samia kuimarisha mahusiano ya kimataifa, USA Kumwaga mabilioni ya kusaidia Elimu na Lishe Nchini

The Sunk Cost Fallacy

JF-Expert Member
Dec 1, 2021
19,586
14,137
Nawasalimu kwa jina la JMT na Kazi inaendelea..

Ni hivi,awamu ya 5 mahusiano ya Tanzania na Juiya ya Kimataifa yalitetereka Sana hadi kupelekea washirika wa Maendeleo kujitoa na kususa mfano ni Tanzania kuondolewa kwenye mpango wa MCC ambapo,Tzn Tulikuwa tunapokea zaidi ya dola za marekani mil.700 kwa ajili ya miradi mbalimbali ya elimu, miundombinu,umeme,maji nk kutoka serikali ya Marekani kupitia Millennium Challenge Corporation-MCC.

Hata hivyo baada ya Mabadiliko ya uongozi na kuingia Rais Samia ameboresha Sana mahusiano kiasi cha kupelekea washirika waliosusa na kujitoa kurudi tena kufadhili Tzn kama Denmark na Nchi nyingine za Nordic,WB,IMF nk..

Sasa USA imetangaza kuanza tena kwa mpango wa kuboresha Elimu na Lishe kwa watoto wa shule za msingi.Hope kabla ya 2025 Tzn itakuwa imerudishwa kwenye Mfuko wa MCC.

Ikumbukwe kwamba Tzn ilikuwa inapokea fedha nyingi kuliko Nchi zote za Afrika ndani ya MCC.Kupitia hizo pesa serikali ilijenga barabara ya Songea-Mtrwara,Tunduma-Sumbawanga,daraja la Malagarasi,Umeme Kigoma nk .

My take,

Mbowe,Lisu,Lema na Chadomo wenzao is insignificant na hakuna anaewasikiliza huko Duniani wanakopiga makelele.

Screenshot_20220208-103229.png


Screenshot_20220208-104400.png


Screenshot_20220208-163030.png
 
Jinsi unavyopokea mabilioni ya mcc na ndiyo unavyotoa mabilioni ya rasilimali za taifa kwenda mcc.

There is no free lunch
Which one is better to live your people die just to hide your resources or give up in order to save your people to secure life. Jk aliweza kuajiri kila mwaka kwa sababu ya huo mpango. Huoni jpm alikuwa anaua watu kisa ubabe wake usio na maana mpaka ikapelekea five years no ajira yeye anasisitiza umachinga tu.
 
Ni lini watanzania walikufa njaa kwa sababu ya mcc?
Kwanza walipojitoa hao mcc Tanzania ikapiga hatua hadi uchumi wa kati
Kwa hiyo Tzn hii maisha ni safi sio? Kenge na wajinga nyie, kama ni kula tuu hata mbwa wanakula.

By the way unajua kwamba zaidi ya 40% ya Watoto Wana utapiamlo na udumavu? Matokeo yake ndio haya sasa kuwa na watu wenye akili ndogo kama wewe,akili zako zinaishia kuwaza kula tuu..

NYie ndio wale mnalialia Kuhusu rasilimali kwamba wanachukua wageni lakini huyo anaelia hana hata mia wala teknolojia ya kuwekeza na kusaidiwa hataki.Hizo ni akili au matope?
 
Ni lini watanzania walikufa njaa kwa sababu ya mcc?
Kwanza walipojitoa hao mcc Tanzania ikapiga hatua hadi uchumi wa kati
Uchumi wa katibgraduates wanarundikana kila mwaka ajira hamna. Sasa ajira ndo zinaanza kufunguka.
Ukikosa ajira au kipato ndo kuuwa mwenyewe hata Kama unakula. Hatupo kwa ajiri ya kula tu
 
Uchumi wa katibgraduates wanarundikana kila mwaka ajira hamna. Sasa ajira ndo zinaanza kufunguka.
Ukikosa ajira au kipato ndo kuuwa mwenyewe hata Kama unakula. Hatupo kwa ajiri ya kula tu
Ajira zitakuja bila kuzitumia rasilimali kujenga ajira na fursa? Na walirundikana wakati wa uongozi wa yule mpuuzi aliyekuwa hamjui adui yake anagombana na kila mtu si jirani si wa mbali.

Mama hana huo ujinga ndio maana unaona fursa zinafunguka sasa na wadau wa maendeleo kote Duniani wanampa mkono ,usipochangamkia ni ujinga wako hakuna atakuja kukuita kwako .
 
Kumwaga mabilioni ya fedha kwenye Taifa ambalo Rais wake yupo busy kuhamasisha ufisadi kwenye Serikali yake ni sawa na kutwanga maji kwenye kinu🐒🐒🐒
 
Swali : Tungekuwa wapi bila Rais Samia?
Jibu : Tungekuwa mbali mno

1: Uchumi wa Tanzania ungekuwa wa kati daraja la juu tofauti na hali ilivyo sasa ambapo Tanzania imeporomoka kutoka nafasi yake ya 8 kati ya nchi 10 zenye uchumi bora Africa mpaka nje ya top 10 na kuzidiwa na vinchi kama Ghana na Angola

2: Nidhamu na uwajibikaji kazini ungekuwepo.Leo hii tunashuhudia wananchi wakihoji kuhusu hali ya umeme nchini pasipokuwa na majibu au majibu yenye uwalakini. Lakini pamoja na hayo bado viongozi wamebaki wakiwa maofisini pasipo kuwajibika kwa namna yoyote.

3: Kwa miaka kadhaa Tanzania imekuwa ikiifanya juhudi kubwa kujikwamua kiuchumi kwa kuanzisha miradi mikubwa na ya kimkakati. Licha ya kwamba tangu Rais S.S.H aingie madarakani hakuna mradi wowote wa kimkakati ulioanzishwa bali pia hata ile miradi iliyokuwa ikiendelea imekuwa ikisuasua

4: Umeme usingekuwa wa mgao.Tangu Rais S.S.H aingie madarakani hali ya upatikanaji wa umeme nchini imekuwa mbaya sana.Hali hii imepelekea kurejea kwa mgao wa umeme ambao watanzania wengi walishausahau tangu miaka kadhaa iliyopita.Hali inayopelekea kuwatesa wananchi hususan wale wanaotegemea umeme kujipatia vipato katika shughuli zao za kila siku.

5; Hali ya upatikanaji wa maji imekuwa ya kusuasua.Kwa miezi kadhaa hususan katika jiji la Dar es salaam pamekuwa na mgao wa maji.Hali iliyopelekea kukosekana kwa maji kwa muda mrefu katika maeneo mengi.Hali ambayo hakuwahi kushuhudiwa hapo awali.

6: Tozo zisizokuwa na tija na zilizoua uchumi wa wengi.Serikali ya awamu ya sita imedhulumu na kunyang'anya kwa nguvu fedha za wananchi kwa kigezo cha tozo katika miamala ya simu.Mama mjane anapomtumia mgonjwa wake hospitali kwa ajili ya matibabu anakatwa fedha ambayo kimsingi haikuwa ya biashara. Kwa mujibu wa report kutoka Vodacom hivi karibuni miamala ya simu imepungua kwa asilimia zaidi ya 30!.Hili si jambo la kupuuza hata kidogo kwa uchumi wa nchi.Ni sawa na kutoa fedha mfuko wa kushoto na kuhamishia Kulia.

7: Kupanda kwa bei ya Mbolea.Mara tu baada ya awamu ya sita kuingia madarakani bei ya mbolea ilipanda karibu mara mbili ya bei ya awali.Hii ni imepelekea uchumi wa watanzania wengi ambao ni masikini na wanategemea kilimo kudhoofika.

8; Kupanda kwa bei ya mafuta ya kupikia
9; Kupanda kwa bei ya mafuta ya petrol
10; Kupanda kwa bei ya bidhaa za ujenzi kama cement,Nondo n.k
11; Teuzi za viongozi wasiokuwa na weledi kwa kigezo cha favour/Undugu/Kujuana (Mf. Riziwani Kikwete,Nape Nauye n.k) Tanzania ina vijana wasomi na wenye upeo mpana wa kifikra. Lakini cha kushangaza teuzi zimekuwa hazina matumaini ta kuipeleka Tanzania kule tunapotarajia.

12: Ukosefu wa uzalendo na ubadhirifu miongoni mwa watumishi wa umma.Siku si nyingi tumeshuhudia kiongozi mkuu wa serikali akiwaasa watumishi wake wale kwa urefu wa kamba zao.Hii inaashiria kwamba hata kiongozi mkuu anashiriki katika ulaji huo.Hali hii ni hatari kwa rasilimali za nchi.

13; Wananchi hususan wa hali ya chini kukosa nafasi katika nchi yao.Siku si nyingi tumeshuhudia wafanyabiashara ndogondogo maarufu kama machinga wakinyanyaswa kwa kuhamishiwa katika maeneo yasiyokuwa tija kwao.Vuta nikuvute hii imepelekea hali ya unyonge na sintofahamu miongoni mwao na kupelekea kuongezeka kwa umasikini miongoni mwa watanzania

14; Mikopo isiyokuwa na tija kwa taifa.Tangu Tanzania ipate uhuru viongozi wake wote walisisitiza kufanya mambo yetu kwa fedha zetu wenyewe bila kutegemea wahisani. Tanzania imebarikiwa rasilimali za kila aina.Mito,Maziwa,Bahari,Madini kama Tanzanite,Mbuga za wanyama,Gesi n.k Inashangaza Sana kuona kiongozi badala ya kusisitiza au kubuni namna ya kuzitumia rasilimali hizi ziweze kuwa na tija kwa watanzania,Badala yake tumekuwa tukijivunia mikopo!

15 ; Kuongezeka kwa gharama za uunganishaji umeme kutoka 27,000 iliyokuwepo mpaka zaidi ya 300,000 ya hivi sasa.Hali hii imepunguza mno kasi ya usambaaji wa umeme

16 ; Muingiliano baina ya mihimili kwa kigezo cha uchama.Inasikitisha kuona kiongozi wa mhimili mmoja anakosa uwezo wa kuikosoa na kuurekebisha mhimili mwingine kwa kuhofia kibarua chake.hili tumelishuhudia baada ya kuona spika wa bunge la JMT kujiuzulu baada ya kuhoji kuhusu mikopo na tozo.

17 ; Safari zisizokuwa na tija wala umuhimu kwa taifa.Tumeshuhudia safari nyingi mno za nje ya nchi,Safari hizi zimekuwa zikiigharimu nchi fedha nyingi.Safari za vikao visivyokuwa na tija kama mkutano wa kujadili athari za gesi ya ukaa sidhani kama ina tija hususan kwa nchi ambazo bado uchumi wake ni mdogo

18 ; Kukosekana uhuru na ukandamizaji wa demokrasia. Tunaweza kusema kwamba pia hata katika awamu zilizopita hili lilikuwepo, Lakini hili la sasa limekuja kwa namna tofauti.Wakati mwingine baba anaweza kumpa mtoto adhabu ya kulima shamba,Mtoto akalia na kulaumu sana,Lakini shamba hilohilo baadaye likaleta chakula mezani wote wakala na kufurahia. Ila tofauti iliyopo sasa,Hakuna chakula kinachokuja mezani!

19 ; Kushughulikia zaidi mambo yasiyokuwa na tija kwa wananchi kuliko yale yenye umuhimu na tija kwa watanzania. Imekuwa jambo la kawaida kwa awamu hii kujihusisha zaidi na makongamano,Semina elekezi,Birthday Party pamoja na hafla mbali mbali badala ya kujikita katika kufufua na kubuni miradi ya kimaendeleo itakayosaidia kuwapunguzia wananchi mzigo wa umasikini na kuinua uchumi.Hafla ya machifu na watemi si muhimu kama hafla ya utiaji saini mradi wa uchimbaji na usambazaji wa gesi ya Mtwara!

20 ; Kukosekana ajira. Ubunifu na uibuaji wa miradi mipya si tu umekuwa na tija kiuchumi Bali umekuwa ukiajiri vijana wengi.Kukosekana kwa ubunifu na sera mbovu za serikali zimesababisha kukoseka kwa ajira miongoni mwa vijana wengi

Hakika ni mambo mengi ambayo yamekuwa yakifanyika kinyume na matarajio ya watanzania wengi ambao waliwaamini viongozi wao na kuwaweka madarakani huku wakiwa na matumaini makubwa ya kuondokewa na maradhi, ujinga na umasikini ambao ndio maadui wakuu wa taifa kama ilivyobainishwa na Mwl Nyerere badala yake watanzania hao ambao wengi ni masikini na wameteseka kwa umasikini kiasi cha kusahau tarehe zao za kuzaliwa huku wakishuhudia wale waliowachagua wakikata keki ikulu!

Wacha kazi iendelee!
Rubbish 🚮 🚮🚮🚮,namba za Uchumi ndio zinazungumza sio hiasia zako za nyege.
 
Nawasalimu kwa jina la JMT na Kazi inaendelea..

Ni hivi,awamu ya 5 mahusiano ya Tanzania na Juiya ya Kimataifa yalitetereka Sana hadi kupelekea washirika wa Maendeleo kujitoa na kususa mfano ni Tanzania kuondolewa kwenye mpango wa MCC ambapo,Tzn Tulikuwa tunapokea zaidi ya dola za marekani mil.700 kwa ajili ya miradi mbalimbali ya elimu, miundombinu,umeme,maji nk kutoka serikali ya Marekani kupitia Millennium Challenge Corporation-MCC.

Hata hivyo baada ya Mabadiliko ya uongozi na kuingia Rais Samia ameboresha Sana mahusiano kiasi cha kupelekea washirika waliosusa na kujitoa kurudi tena kufadhili Tzn kama Denmark na Nchi nyingine za Nordic,WB,IMF nk..

Sasa USA imetangaza kuanza tena kwa mpango wa kuboresha Elimu na Lishe kwa watoto wa shule za msingi.Hope kabla ya 2025 Tzn itakuwa imerudishwa kwenye Mfuko wa MCC.

Ikumbukwe kwamba Tzn ilikuwa inapokea fedha nyingi kuliko Nchi zote za Afrika ndani ya MCC.Kupitia hizo pesa serikali ilijenga barabara ya Songea-Mtrwara,Tunduma-Sumbawanga,daraja la Malagarasi,Umeme Kigoma nk .

My take,

Mbowe,Lisu,Lema na Chadomo wenzao is insignificant na hakuna anaewasikiliza huko Duniani wanakopiga makelele.

View attachment 2112706

View attachment 2112707
FB_IMG_1644311990503.jpg
 
Nyie hamjui tu watu weupe wanavyotuona takataka...miaka 60 ya uhuru tunapewa misaada ya namna hii? Namna wana program akili zetu kuendelea kuwa za kijinga na kuwaza misaada tu...nchi imejaliwa ardhi, mito kibao, maziwa lakini tunatoa hadi gego la mwisho kupewa misaada ya namna hii?? Hivi watu weusi inawezekana tuna laana??
 
Just imagine ka nchi kama Singapore kalivyo progress, very advanced, nchi iliyokuwa masikini wa kutupwa na wamepata uhuru baada ya sisi, walikuwa masikini kiasi kwamba walitaka kuiuza Singapore kwa Malaysia, tuna shida gani vichwani sisi jamani?
 
Nyie hamjui tu watu weupe wanavyotuona takataka...miaka 60 ya uhuru tunapewa misaada ya namna hii? Namna wana program akili zetu kuendelea kuwa za kijinga na kuwaza misaada tu...nchi imejaliwa ardhi, mito kibao, maziwa lakini tunatoa hadi gego la mwisho kupewa misaada ya namna hii?? Hivi watu weusi inawezekana tuna laana??
Bora msaidiwe saizi Ili vizazi vyenu visije kushindwa kama nyie,Kama mumeshindwa kumbe wawaache mfe?👇👇

Screenshot_20220208-164641.png


Screenshot_20220208-164049.png
 
Back
Top Bottom