Baada ya Rais Magufuli kutema cheche, RC Kunenge aenda Ubungo Shule ya Msingi King'ongo, apiga mkwara

Kokoto nondo mchanga zimepelekwa site naona ujenzi umeanza faster

Ova

Sent from my SM-N920T using JamiiForums mobile app
Afu ukiwauliza mmefanya mchakato saa ngapi,kukutana na kamati za shule,kujadili..n.k

Lakini kama Rais asingesema ukiomba hela ya shule, watakavyo kuelezea michakato yake utachoka hata kabla hujaanza aisee!

Wanaudhi sana watu wa hizi Manispaa na Halmashauri. Wanajifanya kujua michakato kumbe upigaji tu. Wakuu wa shule hubanwa na mainjinia pindi hela zikitoka za ujenzi au ukarabati.

Mkuu wa shule akigangamala utasikia mainjinia wanakataa jengo kisha inakula kwa mkuu wa Shue.

Kuna changamoto kubwa sana kwenye Local Govement! Mungu atunusuru;

Vyombo vya usalama vimemfikishia mzee taarifa,akaizungumzia ndo wanakurupuka kujenga, Mhe. Akiwa anatumbua tumsamehe tu!
 
Wapinxani hawapo tena,mnatengeneza kiki,yaaani mnajitekenya wenyewe
 
Aende na shule ya Msingi Goba watoto wanakaa darasani ila chini kwenye mchanga.

Pia Shule ya Msingi Tegeta A nayo ipo kata ya Goba watoto wanasomea chini ya mti nje, yaani Kwa kweli jimbo la Ubungo maendeleo yapo nyuma sana sana.
Sera za jiwe ni za kipumbavu sana huwezi kuwatenga raia kisa wamechagua mbunge wa upinzani. Huo ni upumbavu! Lakini ukisimama majukwaani unawadanganya raia eti maendeleo hayana chama
 
..basi kulikuwa hakuna haja ya kujitapa kuwa Jpm anagawa mabilioni ya elimu bure kila mwezi wakati kuna wanafunzi hawana madawati, na shule hazina matundu ya choo ya kutosha.
Ona aibu sasa, Shule nyingi wanapata huduma bora zaidi kuliko wakati mwingine wowote kuanzia aipoingia Mwinyi madarakani. Huo ndio ukweli, kama unapinga weka data sio maneno matupu. Hatujaona maandamano ya wanafunzi tangu JMK alipoondoka, hiyo tu inaashiria mambo yamebadilika kuelekea kule ambako kila Mtanzania anatarajia.
 
RC Aboubakar Kunenge amefika katika Shule ya Msingi King'ongo wilayani Ubungo, Dar es Salaam baada ya Rais Magufuli kueleza kukerwa na wanafunzi shuleni hapo kukaa chini. Rais ameagiza atakaporejea Dar es Salaam madarasa shuleni hapo yawe yamekamilika na wanafunzi hawakai chini.

===

Akiwa mkoani Kagera, rais Magufuli alisema“Kuna maeneo hata Dar es salaam kuna mapungufu, kuna Shule moja ipo Ubungo, ina Wanafunzi wengi tu, Wanafunzi wapo Dar es salaam Ubungo bado wanakaa chini, madarasa yamebomoka, madawati yamevunjika, DC, DED na RC wapo na Mbunge yupo na ni Prof. tena wa Elimu”

“Namshukuru Mwandishi ameitoa kwenye mitandao kuwa Wanafunzi wanakaa chini, Viongozi wa kule wakaanza kusema ni masuala ya kisiasa, hayo sio masuala ya kisiasa, hayo Mimi ndio napenda kuyajua” aliongeza rais Magufuli.

“Ninazungumza nikiwa Kagera lakini nikienda Dar es salaam niyakute madarasa ya Shule ya Barango yamekamilika na Wanafunzi hawakai tena chini, nitaenda kuitembelea Mimi hiyo Shule, alibainisha rais Magufuli wakati akizungumza mkoani Kagera leo.

View attachment 1680653View attachment 1680654View attachment 1680655View attachment 1680656

RAIS MAGUFULI ATAKA VIONGOZI KUSHUGHULIKIA MAPUNGUFU
View attachment 1680666
- Asema, kuna Shule ya Msingi Ubungo, Dar iitwayo Barango bado Wanafunzi wanakaa chini huku madarasa mengine yakiwa yamebomoka

- Amesema atakapoenda anataka kukuta madarasa yamekamilika

Soma > Rais Magufuli awataka Viongozi kushughulikia mapungufu akisema kuna wengine bado wamelala

#JFLeo https://t.co/vC948tBDdi




Hapo tayari ana orodha ya kuwatimua anasubiri tu aingie site
 
Ona aibu sasa, Shule nyingi wanapata huduma bora zaidi kuliko wakati mwingine wowote kuanzia aipoingia Mwinyi madarakani. Huo ndio ukweli, kama unapinga weka data sio maneno matupu. Hatujaona maandamano ya wanafunzi tangu JMK alipoondoka, hiyo tu inaashiria mambo yamebadilika kuelekea kule ambako kila Mtanzania anatarajia.

..Ni aibu serikali kujitapa kununua madege toka kwa mabeberu huku watoto wetu hawana madarasa, madawati, na wanajisaidia machakani.
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom