Baada ya Rais Magufuli kutegua mtego huu, hawa jamaa wanakuja na jaribio gani jipya?

Mar 17, 2016
193
188
Stori kubwa weekend hii ilikuwa kutumbuliwa kwa Waziri wa mambo ya ndani mheshimiwa Charles Kitwanga anayesemekana kuwa rafiki mkubwa sana wa aliyemtumbua.Kwa mujibu wa taarifa ya Ikulu sababu kubwa ya kutumbuliwa kwa mheshimiwa huyu ni kujibu swali huku akiwa mbwii, japo wapo wanaoamini kuna zaidi ya hicho.

Kwa wale tunaongalia mambo kwa hicho la mbali hili lilikuwa jaribio la kwanza kali sana kwa Raisi hasa kutokana na kasi aliyoanza nayo hasa utumbuaji majipu. Nasema hv kwa sababu walioandaa jaribio ni watu makini sana hasa ukiangalia uteuzi wa tageti yao. Nchi hii ina skendo nyingi sana na kubwa kuliko hii ya Lugumi, lkn wao waliamua kuchagua Lugumi, kwanini?:
kinachotokea kuna wanaume wa shoka ambao wameitafuna Nchi hii vya kutosha huko nyuma ambao mkono wa Raisi Magufuli unaonekana ukiwafuata kwa kasi ya ajabu mno.

Wanaume hawa wa shoka wanajua karibu kila kitu kilichofanyika kiwe kabaya au kizuri na kimefanywa na nani, hawakugusi hadi utakapojaribu kuingilia interest zao au wanapodhani lazima uguswe ili mambo yao yaende. Kiufupi ni watu wabaya sana kwa taifa hili na wanauwezo mkubwa mno wa kupanga mambo yao ndio maana kwenye skendo kibao ktk Nchi wakaamua kuchagua Lugumi.

Unajua kwanini Lugumi? walijua huu ni mtihani mgumu sana kwa Raisi, kwa ufupi walijua hataweza kumtumbua kwa kuwa ni mtu wake wa karibu kitu ambacho kingempunguzia credibility na moral authority ya kuwatumbua wengine.Yaani walitaka wajenge mazingira kwamba Raisi anachagua watu wa kuwatumbua na tayari watu walikuwa wanaanza kuicheza ngoma hii. Hivo wakijua hatoweza kumtumbua Kitwanga na biashara ya utumbuaji na ufuatiriaji wa wanyanganyi wa Nchi hii ingeishia hapo, kwa lugha nyingine walikuwa wanajaribu kumkatisha tamaa Raisi kabla hajawafikia kwa kuibua uozo wa watu wake wa karibu kitu ambacho kingemlazimu aachane na biashara hiyo, hivyo wao wangebaki salama.

Sasa Raisi kafanikiwa kutegua mtego wao, lkn najua hawawez kukubali kirahisi kwa kuwa wapo vzr na wamejipanga.Swali ni je? Baada ya jaribio lao hili kufeli wanakuja na jaribio lipi tena kwa mkuu wa kaya?
 
Inakuwa ngumu sana kuelewa kwanini Lugumi na infosy hazijamtumbua Kitwanga kiasi cha kusubiri kamati ya bunge ila ulevi ambao hauna ushahidi wa kueleweka umemtumbua Kitwanga. Sio bure kuna kitu kimefichwa nyuma ya pazia
 
Bado hajakwepa lolote tunataka sasa wale wote waliohusika na kashifa ya Lugumi awaburuze mahakamani hapo ndio tutaamini mtukufu rais kweli kaja kupambana na ufisadi
 
Stori kubwa weekend hii ilikuwa kutumbuliwa kwa Waziri wa mambo ya ndani mheshimiwa Charles Kitwanga anayesemekana kuwa rafiki mkubwa sana wa aliyemtumbua.Kwa mujibu wa taarifa ya Ikulu sababu kubwa ya kutumbuliwa kwa mheshimiwa huyu ni kujibu swali huku akiwa mbwii, japo wapo wanaoamini kuna zaidi ya hicho.

Kwa wale tunaongalia mambo kwa hicho la mbali hili lilikuwa jaribio la kwanza kali sana kwa Raisi hasa kutokana na kasi aliyoanza nayo hasa utumbuaji majipu. Nasema hv kwa sababu walioandaa jaribio ni watu makini sana hasa ukiangalia uteuzi wa tageti yao. Nchi hii ina skendo nyingi sana na kubwa kuliko hii ya Lugumi, lkn wao waliamua kuchagua Lugumi, kwanini?:
kinachotokea kuna wanaume wa shoka ambao wameitafuna Nchi hii vya kutosha huko nyuma ambao mkono wa Raisi Magufuli unaonekana ukiwafuata kwa kasi ya ajabu mno.

Wanaume hawa wa shoka wanajua karibu kila kitu kilichofanyika kiwe kabaya au kizuri na kimefanywa na nani, hawakugusi hadi utakapojaribu kuingilia interest zao au wanapodhani lazima uguswe ili mambo yao yaende. Kiufupi ni watu wabaya sana kwa taifa hili na wanauwezo mkubwa mno wa kupanga mambo yao ndio maana kwenye skendo kibao ktk Nchi wakaamua kuchagua Lugumi.

Unajua kwanini Lugumi? walijua huu ni mtihani mgumu sana kwa Raisi, kwa ufupi walijua hataweza kumtumbua kwa kuwa ni mtu wake wa karibu kitu ambacho kingempunguzia credibility na moral authority ya kuwatumbua wengine.Yaani walitaka wajenge mazingira kwamba Raisi anachagua watu wa kuwatumbua na tayari watu walikuwa wanaanza kuicheza ngoma hii. Hivo wakijua hatoweza kumtumbua Kitwanga na biashara ya utumbuaji na ufuatiriaji wa wanyanganyi wa Nchi hii ingeishia hapo, kwa lugha nyingine walikuwa wanajaribu kumkatisha tamaa Raisi kabla hajawafikia kwa kuibua uozo wa watu wake wa karibu kitu ambacho kingemlazimu aachane na biashara hiyo, hivyo wao wangebaki salama.

Sasa Raisi kafanikiwa kutegua mtego wao, lkn najua hawawez kukubali kirahisi kwa kuwa wapo vzr na wamejipanga.Swali ni je? Baada ya jaribio lao hili kufeli wanakuja na jaribio lipi tena kwa mkuu wa kaya?

Moja kati ya nyuzi zenye viwango vya chini kabisa kifikra.

Wewe ndo umeanzisha haka kauzi kimkakati ukitaka kutaminisha rahisi kafanya jambo la kishujaa sana kumfuta kazi chapombe.

Mtumbuliwa ni mdau wa Lugumi na ni chapombe full stop.
Tunasubiri watumbuliwe wa ESCROW, RICHMOND na EPA sasa.
 
Back
Top Bottom