Baada ya Rais Magufuli kukemea mazishi ya " kienyeji" ya DC Mmanda, je marehemu wa Corona sasa watazikwa kwa heshima?

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
82,745
139,517
Nadhani hili ndio jukumu la kwanza la Waziri mpya wa Katiba na Sheria Dkt. Mwigulu Nchemba kuhakikisha marehemu wote wanaokufa kwa Corona wanapata haki ya msingi ya kuzikwa kwa heshima.

Binafsi nilikerwa sana kwa namna rafiki na mwanasheria wangu DC Mmanda alivyozikwa " kienyeji" bila kufuata mila wala desturi ya kabila na jamii yake.

Karipio la Rais Magufuli kwa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara limenipa faraja kubwa na nipo tayari kuchangia endapo familia yake itaamua Wakili Mmanda akazikwe kwa upya nyumbani kwso Rombo.

Mungu mbariki Rais Magufuli!

Dominica njema.
 
Hilo karipio kalitoa lini na wapi johnthebaptist!?
Nadhani hili ndio jukumu la kwanza la waziri mpya wa katiba na sheria Dr Mwigulu Nchemba kuhakikisha marehemu wote wanaokufa kwa Corona wanapata haki ya msingi ya kuzikwa kwa heshima.

Binafsi nilikerwa sana kwa namna rafiki na mwanasheria wangu DC Mmanda alivyozikwa " kienyeji" bila kufuata mila wala desturi ya kabila na jamii yake.

Karipio la Rais Magufuli kwa mkuu wa mkoa wa Mtwara limenipa faraja kubwa na nipo tayari kuchangia endapo familia yake itaamua Wakili Mmanda akazikwe kwa upya nyumbani kwso Rombo.

Mungu mbariki Rais Magufuli!

Dominica njema.
 
Swala la namna mazishi ya wagonjwa was corona yatakavyokua si lilitangazwa na serikali?Yeye kama mkuu wa nchi mbona hakulikataa?Tatizo walijua hili janga wao kama viongozi halitawakumba.
 
Mimi anachoniuaga magufuli yeye ni kama sio sehemu ya serikali, waziri mkuu alipose a swala la mazishi liwe na watu kumi sijui yeye sijui alikua anajifukiza leo anajidai eti kachukizwa kwaio siku zote hizo alikua haoni mpaka DC alivozikwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Corona sio ebola, watupe miili ya ndugu zetu tukizike mchana kwa heshima zote. Kama ni hizo PPE tutanunua.
 
Nitakuwa wa mwisho kuamini kwamba Rais hukuambiwa kwamba mteule wako muwakilishi wako amefariki na tutamzika kwa taratibu ABCD,alikuwa na nafasi ya kushauri(ushauri mzuri alioutoa).
 
Wewe usipomuona mzee Mgaya huwa unachanganya mambo sana. Je Advocate Mmanda alifariki na Covid-19? Au sababu ya hofu ndio maana Rc wa mtwara akakurupuka kutomsafirisha marehemu? Na sababu ya haya matatizo ikabidi wachukue tahadhali ya kuvaa gowns na masks wakati wa mazishi?
 
Wewe usipomuona mzee Mgaya huwa unachanganya mambo sana. Je Advocate Mmanda alifariki na Covid-19? Au sababu ya hofu ndio maana Rc wa mtwara akakurupuka kutomsafirisha marehemu? Na sababu ya haya matatizo ikabidi wachukue tahadhali ya kuvaa gowns na masks wakati wa mazishi?
Kuna plastic bags wangemfunga hata ,hata mimi sikupendezwa na uzikaji ule hata jeneza lilikuwa la bei rahisi halina hadhi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sijaelewa kwanini mh kasema hivyo
Kwani hakuona ile clip au alishindwa kutoa order ya DC azikwe vizuri na asafirishwe??

Kwenye hili nimeona anakimbia lawama Wakati alikua anao uwezo wa kutoa amri na ikatekelezeka.
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom