Baada ya rais kikwete kutia saini muswaada wa kataba kuwa sheria ,chadema waibuka upya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Baada ya rais kikwete kutia saini muswaada wa kataba kuwa sheria ,chadema waibuka upya

Discussion in 'KATIBA Mpya' started by jamii01, Nov 30, 2011.

 1. jamii01

  jamii01 JF-Expert Member

  #1
  Nov 30, 2011
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 1,837
  Likes Received: 372
  Trophy Points: 180
  Chadema waweka msimamo wao kuhusi Rais kusaini muswada wa katiba kuwa sheria

  Mwandishi wa mtandao huu kutoka Dar es Salaam Neema Kishebuka anaripoti kuwa ,Chama cha Demokrasia na Maendeleo kimeweka bayana msimamo wake kuhusina na muswada ambao umesaini wa Rais kuwa sheria ambayo itaanza kutumika Desemba Mosi.

  Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za makao makuu ya chama Hicho John Mnyika amesema kuwa pamoja na Rais kutia saini muswada huo kuwa sheria bado chama chake kiko katika msimamo huo huo kuwa hakitashiriki katika mchakato wowote wa kuhusian na katiba mpya hadi pale serikali itakapo kubali kurekebisha masuala kadhaa ambayo yameonekana kuwa mabovu ndani ya muswada wa sheria Hiyo.

  Mnyika amewatoa hofu watanzania wote na kusema kuwa wao kama kamati iliyoundwa kutoka ndani ya chama Hicho walikwenda kumuoan Rais ili kumshauri asisaini muswada wa heria Hiyo hadi pale utakapo fanyia warekebisho ushauri ambao Rais kikwete amekiuka na kuusaini na badala yke kudai kuwa marekebisho yatafanyiwa kazi .

  ‘’ Watanzania watuelewe kuwa hatujakubalian na Rais Jk na serikali yake kuwa apitishwa Muswada wa Sheria ya katiba Mpya sisi tulimfuata na mapendekezo yetu tuliyaweka katika waraka tuliompatia kuwa msimamo wetu upo pale pale kwamba asisaini , na kama atasaini basi sisi hatupo tayari kushiriki kwa njia yoyote kwani tupo kwa ajili ya haki za watanzania hatuwezi kukubali katiba Mbovu ‘’ alisema Mnyika

  Hata Hivyo Mnyika ameongeza kusema kuwa pamoja na kuwa wao walikubaliana kuboreshwa kwa maeneo ambayo yanaonyesha hayana faida kwa wananchi yaboreshwe ili kuleta katiba iliyo Bora na kwamba hata saini walizowekeana baina yao na serikali si Rais asaini muswada huo wala si Rais asisaini muswada Huo, bali yafanyike maboresho.

  Amesema wao kama chadema wamesitisha maandamano ila amewataka viongozi wote wa chama Hicho kuelekea kwa wananchi kuwaeleza muswada aliosaini Rais ulivyo Mbovu.
  Ameleeni baadhi ya watu wanaodhani Chadema imenunuliwa na ccm na kusema kuwa hawaungi mkono sheria Hiyo inayotarajiwa kutumika wakati wowote kuanzia sasa na kwamba rais anayo nafasi ya kuzuia sheria hiyo isianze kutumika kwa manufaa ya watanzania ili kuleta katiba Boiiora na si Bora katiba.
  Hivi karibuni kamati ndogo ya watu saba iliyoundwa na chadema ilikutana na kufanya mazungumzo yaliyodumu kwa takribani siku mbili , huku chadema wakipeleka mapendekezo yao kwa Rais Kikwete ili kuhusian na muswada wa sheria ya mchakato wa katiba mpya ambapo mnyika kwa niaba ya CHADEMA Na Enanuel Nchimbi kwa niaba ya serikali wote kwa pamoja walitia saini makubaliano ya kuwepo na mawasiliano ya mara kwa mara kati ya serika,li na wadau mbali mbali juu ya kuboresha sheria Hiyo kwa lengo la kudumisha muafaka wa kitaifa kwenye mchakato wa sheria mpya.

  Kingine walichokubaliana na chadema na serikali ya Jk kuwepo kwa haja ya sheria Hiyo kuendelea kuboreshwa pamoja na kwamba imepitishwa na Bunge ili kujenga hali ya kuaminiana na mwafaka wa kitaifa.
  Hata Hivyo kurugenzi ya mawasilino ya Ikulu ilitoa taarifa kuwa Rais Jk amesaini muswada wa sheria ya mabadiriko la katiba 2011.
   
 2. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #2
  Nov 30, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,107
  Likes Received: 22,163
  Trophy Points: 280
  Kuna "contradiction" ya hali ya juu:

  '' Watanzania watuelewe kuwa hatujakubalian na Rais Jk na serikali yake" mbele kidogo:
  "Kingine walichokubaliana na chadema na serikali ya Jk" Sasa huu ni uandishi wa habari mbovu ama ni kama nilivyowahi kusema kwenye post moja humu JF kuwa "wamekubaliana kutokukubaliana"?
   
 3. Kamakabuzi

  Kamakabuzi JF-Expert Member

  #3
  Nov 30, 2011
  Joined: Dec 3, 2007
  Messages: 1,500
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  kuna mambo hawakukubaliana "Watanzania watuelewe kuwa hatujakubalian na Rais Jk na serikali yake kuwa apitishe Muswada wa Sheria ya katiba" lakini kuna mabo wamekubaliana " walikubaliana kuboreshwa kwa maeneo ambayo yanaonyesha hayana faida kwa wananchi"
  Nadhani hapo umeelewa walichokubaliana na kile ambacho hawakukubaliana! Its not a contradiction!
   
 4. Mohammed Shossi

  Mohammed Shossi Verified User

  #4
  Nov 30, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 3,986
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  Nalingojea hilo tamko kwa hamu na tamu
   
 5. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #5
  Nov 30, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,107
  Likes Received: 22,163
  Trophy Points: 280
  Kwa hiyo unakubaliana na mimi kuwa "wamekubaliana kutokukubaliana" au sio?

  Halafu soma vizuri imeandikwa "kingine walichokubaliana" kingine kipi?
   
 6. m

  muaminifu Member

  #6
  Nov 30, 2011
  Joined: Nov 28, 2011
  Messages: 10
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kwahyo tunapingaje?..kama maandamano hakuna sasa 2subiri tena wakakubaliane yaliyoshindikana ikulu?..
   
 7. LordJustice1

  LordJustice1 JF-Expert Member

  #7
  Nov 30, 2011
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 2,264
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Kwani FaizaFox kuna lolote kuhusu CDM unaloelewa?
   
 8. made

  made JF-Expert Member

  #8
  Dec 1, 2011
  Joined: Jun 29, 2010
  Messages: 746
  Likes Received: 246
  Trophy Points: 60
  Hivi ni nani mwenye uhakika kama mlikubaliana au laa!mmetoka Ikulu mnachekacheka tu then huku mnatuambie hamjakubaliana,kwanza kwa nn mlienda Ikulu kama hatumtambui Rais,Mnajua nyie wanasiasa mnatuchanganya sana au kwa kuwa yenu yanaenda?Kwani wale walioandamana kule Misri walikuwa na chama?mi nadhani hakuna haja ya kuwa na chama tuandamane kama watanzania wenye uchungu mpaka kieleweke,nnachokiona mimi hakuna CCM,Chadema wala CUF wote lao moja tu.Nachukia zaidi siasa ingawa viongozi wanatokana na hilo.
   
 9. Bakulutu

  Bakulutu JF-Expert Member

  #9
  Dec 1, 2011
  Joined: Nov 30, 2011
  Messages: 1,922
  Likes Received: 332
  Trophy Points: 180
  SIGNATURE NINI MAANA YAKE!
  Hiv mm na ww tukikubaliana ki2 na hili tufikie usahihi wa makubaliano ye2 zina hitajika sahihi zetu ww ukawa una pinga kuw mambo fulan hayakaa sawa,then later baaade nakumbia we sain tuu nitayarekebisha baadae! Nikija kataa kubadilisha utafuta sain yako!
  CHADEMA WALIPEWA JUICE WAKALEWA AU?!!
  HAPA TUMEZAMISHWA NUNGWI WALAI!
   
 10. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #10
  Dec 7, 2011
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,668
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Haya uliyoandika ni uchanga katika siasa.
  Nani alikwambia wakienda ikulu hawaruhusiwi kunywa juice au soda? Nani alikwambia kwa kuwa walikwenda ikulu kwa hiyo ikulu haiwezi kubadilika? na hasa ikulu hii ya Kikwete??
  Tuna ushahidi mwingi tu kwamba makubaliano mengine ukiukwa kwa makusudi na serikali.
  Ni serikali ya huyu huyu Kikwete ina rekodi ya kugeuza hata miswada ya bunge isomeke tofauti katika sheria kinyume na makubaliano.
  Tafakari sana kabla hujaandika.
   
 11. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #11
  Dec 7, 2011
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,668
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Wewe Made haya uliyoandika ni uchanga wako katika siasa za Tanzaia.
  Nani alikwambia wakienda ikulu hawaruhusiwi kunywa juice au soda? Nani alikwambia kwa kuwa walikwenda ikulu kwa hiyo ikulu haiwezi kubadilika? na hasa ikulu hii ya Kikwete??
  Tuna ushahidi mwingi tu kwamba makubaliano mengine ukiukwa kwa makusudi na serikali.
  Ni serikali ya huyu huyu Kikwete ina rekodi ya kugeuza hata miswada ya bunge isomeke tofauti katika sheria kinyume na makubaliano.
  Tafakari sana kabla hujaandika.
   
Loading...