Mra Eliphas
JF-Expert Member
- Feb 16, 2017
- 264
- 234
Muda mfupi uliopita baada ya kuona post humu ndani kwamba Magufuli amewaagiza polisi wamwachie huru Ney wa Mitego, nilidhani ni propaganda tu maana sikuamini angeweza kufanya hivyo kutokana na anavyofahamika kwa msimamo wake hasi dhidi ya uhuru wa habari.
Punde nikaona video ya Dr. Mwakyembe akiwaambia wanahabari maamuzi hayo ya Magufuli na nikajiridhisha ni kweli.
Sasa basi kutokana maamuzi hayo ambayo ni dalili njema kwamba watawala wanaanza kujirekebisha kuondokana na tabia ya kubana uhuru wa habari, jambo ambalo litaanza kumpa sifa raisi Mugufuli , nigemshauri aagize pia yafuatayo:
1. Watu wote walikamatwa na polisi kwa tuhuma za uchochezi wafutiwe mashitaka yote na kuachiwa huru, kupita polisi.
2. Waziri wake wa habari akarudishe Bunge- Live
3. Polisi kuanzia sasa wasikamate mtu yeyote kwa kosa la uchochezi .
4. Waziri wake wa habari apeleke bungeni mswada wa kufuta sheria zote kandamizi kwa uhuru wa habari.
5. Rais amwajibishe Makonda kwa kitendo chake cha kuvamia Clouds ili kujenga uaminifa wa raisi na wanahabari.
Ikiwa Rais atafanya hayo atakuwa amejijengea sifa na kufungua ukurasa mpya wa habari Tanzania.