Elections 2015 Baada ya Pinda kutangaza nia, Membe afunguka

Hivi Pinda si aliwahi tamka kwamba mafisadi wakishughulikiwa nchi itayumba?
 
Hakuna wa kumzuia lowasa akipita kwenye kugombea mtaisoma namba ni vumbi tuuuuu
 
Hawa marais ambao Membe anadai wamekuwa connected na dunia kutokana kuongoza wizara kwa mambo ya nje ndio wanaotuchafulia nchi, mfano mzuri ni JK ameshindwa kupunguza umaskini, uchumi wa Tz umezidi kuporomoka, saraf ya Tz ndo ivyo tena, ajira imekuwa kama ndoto lakini ukimtathmini JK na safari za nje tokea amekuwa rais utagundua ni rais wa kwanza ulimwenguni anayeongoza kupanda ndege kwenda huko duniani lakini wananchi wake njaa na umaskini umekithiri hata mlo 1 kwa siku ni shida kwa watanzania walio wengi.

Ni bora kabisa mara hii kupata rais asiye na harufu za mambo ya nje kama Membe ni yale yale tu. Na ukweli ni kwamba huyu Membe inavyoonekana tayari wanataka kurithishana urais na JK labda kuna makato huko watakuwa wanapeyana sasa hii pia haikubaliki.

Subiri mwezi ujao mkuu ndio utamjua Membe ni kiongozi wa aina gani.
 
Nukuu muhimu
1-
“Nilikuwa ni mjumbe pekee niliyepigwa vita na makundi yote. Mabilioni ya pesa yalichangwa na kuagiza wajumbe wasimchague Membe. Mlishuhudia jinsi kina (jina tunalihifadhi walivyonitukana, lakini kati ya wajumbe 2011, nilipata kura 1,455 na kushika nafasi ya sita.”


2- ("Hapa akimsema PM...")
“Chama chetu sasa kiwe na utaratibu utakaowabana watu fulani wasigombee kutokana na nyadhifa zao. Kama uko kwenye nafasi ya kufanya uamuzi, unawaadhibu hawa, halafu unajitokeza kugombea, kunakuwa hakuna objectivity (hali ya kutotenda haki)”

Uamuzi wa Kamati Kuu ya CCM wa kuwadhibiti kwa mwaka mmoja makada wake sita waliobainika kukiuka kanuni kwa kuanza mapema kampeni za urais, unaweza kuwa uliwakera wengi, lakini si Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Benard Membe, ambaye ni mmoja wa ‘waliofungwa kufuli’.

Membe anaona adhabu hiyo ilikuwa mwafaka na kwamba laiti uamuzi huo usingefanywa mapema, “ingekuwa vurugu tupu”.
“Sijui nchi hii ingekuwa wapi kama watu wangeachwa bila ya kuwekewa ‘gavana’,” alisema Waziri Membe kwenye mahojiano maalumu na gazeti hili yaliyofanyika kwenye ofisi za wizara hiyo jijini Dar es Salaam wiki iliyopita.

Membe pamoja na makada wengine, Frederick Sumaye, Edward Lowassa, William Ngeleja, Stephen Wasira na January Makamba walibainika kukiuka kanuni za uongozi na maadili za CCM kwa kuanza kampeni za kutafuta kuteuliwa na CCM kugombea urais.

Kwa mujibu wa taarifa ya CCM iliyotolewa baada ya kikao cha Kamati Kuu, makada hao walikiuka kanuni za uongozi na maadili za CCM kwa mujibu wa Toleo la Februari 2010 Ibara 6 (7) kwa baadhi yao kufanya vitendo vinavyokiuka maadili ndani ya jamii.

Bila ya kueleza ni jinsi gani vurugu hizo zingefanyika, Membe alisisitiza kuwa vurugu ingekuwa kubwa kama chama hicho kisingechukua hatua mapema.

“We angalia, kuna makundi mawili. Hili kundi letu (la walioanza kampeni mapema wakaadhibiwa) na hili jipya la hawa ambao wameanza kujitokeza sasa, ingawa najua nao watadhibitiwa tu. Hawa wasingedhibitiwa, ingekuwaje?” alihoji Membe.

Wakati CCM inawaita makada hao kwa ajili ya kuwahoji, tayari baadhi walishaanza kufanya sherehe na kualika wenyeviti wa mikoa ambao walieleza misimamo yao juu ya mgombea urais wanayemuunga mkono, wengine kuzunguka kwenye hafla mbalimbali kwa ajili ya harambee na wengine kuzigawa jumuiya za chama hicho, hasa Umoja wa Vijana (UVCCM), huku baadhi ya vikao vikiripotiwa kutawaliwa na malumbano yaliyosababishwa na misimamo tofauti kuhusu mgombea urais wa CCM.

Hata hivyo, Waziri Membe (61) hakusita kukosoa muundo wa vyombo vya uamuzi vya CCM ambao unawapa fursa baadhi kushiriki katika kuadhibu wanaotaka nafasi fulani na baadaye walioadhibu kujitokeza kuwania nafasi hiyo akisema utaratibu huo unawaonea wale ambao hawana fursa ya kuwadhibiti wengine.

“Chama chetu sasa kiwe na utaratibu unaowabana watu fulani kugombea kutokana na nyadhifa zao. Kwa mfano, uko kwenye nafasi ya kufanya uamuzi, unawaadhibu hawa halafu baadaye unajitokeza wewe. Huwezi kuchuja halafu ukajitokeza wewe (kugombea). Kutakuwa hakuna objectivity (haki),” alisema bila ya kuweka bayana watu waliohusika katika kuadhibu na baadaye wakajitokeza kuwania urais.

“Tuwe na utaratibu kwenye chama kwamba wanaowabana watu fulani, wasigombee na hasa wale walioshiriki uamuzi ule na wengine walioko kwenye nafasi za uamuzi… Kamati Kuu na hata (Halmashauri Kuu) Nec na Kamati ya Maadili, nao wasije kujitokeza baadaye na kutangaza nia. Vinginevyo hatutawaelewa,” alisema.

Pamoja na kusifu kitendo cha Kamati Kuu kudhibiti makada mapema, Membe anaona muda umefika kwa CCM kuruhusu wanachama wake wanaowania urais waanze harakati zao sasa.

“Huu ndiyo msimu wenyewe,” anasema Membe ambaye alizungukwa na wasaidizi wake wakati wa mahojiano hayo.
“Kinachotakiwa sasa ni chama kitoe guidelines (miongozo) kwa wagombea. Kiseme wanapaswa kufanya moja, mbili, tatu…. Chama kiruhusu, lakini wagombea wasivuke mipaka hiyo iliyowekwa.”

Kuhusu ndoto yake

Waziri Membe, ambaye alikuwa makini kutotamka waziwazi uamuzi wake wa kugombea urais mwakani, alisema amekuwa na ndoto siku nyingi na alianza kuipima ndoto yake hiyo katika uchaguzi wa wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM mwaka 2012 alipogombea nafasi hiyo kupitia kundi aliloliita “la kifo”.

“Ningeweza kuingia Nec kupitia nafasi ya wilaya ambako kwa vyovyote sikuwa na mpinzani. Lakini niliamua kwa makusudi kupima kukubalika kwangu ndani ya CCM. Katika kujipima huko, nikaamua kugombea nafasi hiyo katika ngazi ya taifa. Sasa kuna watu waliojua ndoto yangu na wakataka kunidhibiti. Wakatumia mabilioni kuniharibia ili kuhakikisha sipiti. Waliamini kwamba ningeangushwa, nisingeweza kurudi tena hapo kuomba nipitishwe,” alisema Membe.

“Kwangu ilikuwa ni vita kuu... nilikuwa kwenye kundi la kifo. Sikufanya kampeni, sikutumia hela wala ushawishi wowote, lakini niliwashinda watu 26. Katika kundi lile (la watu 32), mimi ni mgombea pekee ambaye si mjumbe wa sekretarieti na wala sikuwa mjumbe wa Kamati Kuu. Sikwenda mikoani kutafuta kura wala sikutoa chochote.”

Membe anaongeza kusema: “Nilitaka kupima kama uadilifu wangu ungeweza kunipa nafasi ya uongozi ndani ya chama. Nilikuwa mjumbe pekee aliyepigwa vita kali na makundi yote. Mabilioni ya fedha yalichangwa na wajumbe kuagizwa wasimchague Membe. Mlishuhudia jinsi kina (jina tunahifadhi) walivyonitukana, lakini nikashika nafasi ya sita. Kati ya kura 2011, nilipata kura 1,455 sawa na asilimia 77.”

Alipoulizwa haoni kama mabilioni hayo ya fedha yaliyochangwa kwa ajili ya kuhonga wajumbe, yanadhihirisha kwamba chama hicho kimetawaliwa na rushwa, Membe alikuwa nadhifu katika kuisafisha CCM.

“Mkutano mkuu uliondokana na kashfa ya rushwa kwa ajili yangu. Ni fact (ukweli) kwamba wale watu waligawa rushwa, wajumbe walichukua wakatafuna, lakini hawaku - comply (hawakufuata masharti ya watoaji rushwa),” alisema.

Makundi ya urais

Kila wakati uchaguzi mkuu unapokaribia, CCM hugawanyika katika makundi kulingana na mtazamo wao kwa wagombea urais kwa tiketi ya chama hicho, kiasi cha kutishia kusambaratika. Hali hiyo huwafanya baadhi kuona kuwa ni bora mgombea asiye na makundi ndiye apitishwe kukinusuru chama kusambaratika. Lakini Membe ana mtazamo tofauti.

“Asiwadanganye mtu. Hakuna mgombea urais duniani asiyekuwa na makundi na akitokea mgombea huyo (asiye na makundi), basi ni dhaifu. Kuwa na makundi ni potision (msimamo). Makundi katika uchaguzi ni muhimu kwa kuwa yanamtofautisha mgombea mmoja na wengine. Kimsingi, makundi ndiyo msimamo wa mgombea.

“Mfano kama ni suala la ushoga, uko wapi; kama ni ufisadi, uko kwenye kundi gani. Huwezi kuwa katikati. Ukiwa katikati maana yake ni kwamba nusu unaunga mkono ushoga na nusu hauutaki. Utakuwa hueleweki.

“Kama kuna mambo huyataki, hayo ndiyo yanayo - define (yanayoelezea) kundi lako. Mfano kama (Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Joseph) Warioba anataka serikali tatu na mimi nataka serikali mbili, haya ndiyo makundi yetu. Wote ni CCM, lakini tuna makundi tofauti.”

Sifa za urais

Kuhusu mtazamo wake juu ya sifa za mgombea, Waziri Membe alisema urais ni taasisi nyeti mno watu kuigombea. “Mtu huwezi kusema nagombea urais ili nitekeleze ilani ya chama. Lazima uwe na mambo ya msingi kabisa ya kuwaambia watu kwa nini unataka urais. Huwezi kugombea urais eti kwa sababu una hela za kuwapa watu ili wakuchague,” alisema.

“Tunaweza kuweka sifa 100 au hata 300 za urais, lakini sifa za msingi kabisa za kiongozi huyo ni uchapakazi wake hapo alipo na siyo zamani. Pia tunaangalia uadilifu wake na anachotaka kutufanyia Watanzania. Mgombea urais lazima uende beyond (mbali na) ilani ya chama. Hata mbunge na diwani hutekeleza ilani ya chama! Sasa kwani ni lazima utekeleze ilani ya chama ukiwa Ikulu? Lazima ueleze utafanya nini.

Atagombea urais mwakani?

Membe amesema ana ndoto ambayo bado anaitafakari kuona maana yake. “Ndoto ziko za aina mbili; ile ya mtu kulala akaota na ikabainika kuwa ya kweli na ndoto ambayo ni people driven (inayotokana na maoni ya watu).

Akifafanua alisema, ndoto inayotokana na ushabiki wa watu ni ya kujipima na katika siasa mtu hawezi kujipima mwenyewe. Unahitaji timu kwa ajili ya utafiti wa uwezo wako na changamoto unazoweza kukumbana nazo katika hiyo ndoto, alisema.

“Hata wakati unapopata ushauri wa watu hao, bado haujaoteshwa. Ni process (mchakato). Hukurupuki tu. Huwezi kusema unataka, halafu uje uharibu nchi ya watu. Si suala la haki ya kikatiba. Mtu unaulizwa kwa nini unagombea, unajibu ‘ni haki yangu ya kikatiba’. Ah! Wewe mpuuzi? Ni lazima upate watu wa kukushabikia.

“Nchi ya watu milioni 45, ina watu wengi wenye akili sana, hivyo lazima ujiulize ‘why me? ( kwa nini mimi?)Wewe una nini zaidi mpaka uitake nafasi hiyo. Kusubiri kuoteshwa ni pale wenzako wa kweli wanaposema wamepima kukubalika kwako.”

Alipoulizwa kama tayari ameshaunda timu inayofuatilia na kuchunguza ndoto yake hiyo alijibu, “Ipo na nadhani mwezi ujao itaniletea majibu”.

Waziri Membe tayari ametangaza kutogombea tena ubunge katika Jimbo la Mtama mwaka 2015 na alipoulizwa anapanga kufanya nini baada ya hapo alijibu: “Tofauti na wengine, kwangu ubunge siyo kazi ya kudumu. Nilishawaambia kwamba sitagombea tena na nimewapa ruksa watu kuanza kujipitisha jimboni kwangu, sina tatizo nao.”

Waziri wa Mambo ya Nje na urais

Kwa miongo miwili, watu walioshika nafasi ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, ndiyo waliopitishwa kugombea urais kwa tiketi ya CCM na wakashinda. Benjamin Mkapa alishika wizara hiyo kabla ya mwaka 1995 kuwa Rais na baadaye mrithi wake, Jakaya Kikwete alishika wizara hiyo kwa miaka 10 na sasa ni Rais.

Hata hivyo, Membe hadhani kama kushika nafasi hiyo ni kujihakikishia urais... “Siyo ajabu Waziri wa Mambo ya Nje akashindwa urais, lakini marais wengi sana duniani wametokana na nafasi ya uwaziri wa mambo ya nje. Kama nilivyowaambia, mimi ni waziri wa 13 kushika wizara hii, lakini si wote wamekuwa marais.”

Hata hivyo, alisema waziri anayeshika wizara hiyo ana sifa za ziada kutokana na ukweli kuwa anakuwa na uzoefu katika masuala ya uongozi na itifaki katika ngazi ya kimataifa.

“Sifa ya kiongozi wa nchi ni kuwa connected to the world (kuwa umeunganishwa na dunia). Smart people (watu makini) hawachagui kiongozi ambaye hayuko connected,” alisema na kuongeza kuwa kutokana na kuongoza wizara hiyo anakutana na viongozi mbalimbali duniani, wawekezaji, wafanyabiashara na kufahamu kwa kina masuala ya ushirikiano.

“Rais huendi kujitambulisha kwa wenzako, lazima uwe unajua baadhi ya mambo. Haiwezekani wewe kila kitu unajifunzia Ikulu, kuapisha viongozi, kusoma hotuba, kukaribisha wageni ujifunze kwenye kipindi chako cha uongozi. Sasa hizo ndizo kazi za kila siku za waziri wa mambo ya nje,” alisema.

“Kazi zangu zote mimi (Wizara ya Mambo ya Nje) ni maagizo ya Rais na wizara hii ni idara ya Rais. Ni mkono wa Rais, hivyo ukiwa hapa una picha nzuri ya uongozi wa nchi. Lakini kama nilivyosema hata hivyo, siyo automatic (moja kwa moja), chama kinapaswa kukuchagua na watu wakukubali.”



cc: pasco
Mytake:
Huyu mtu ana uwezo mkubwa sana,
ingawa wapo wengi wenye sifa, lakini kiukweli simuoni mtu mwingine CCM anayemkaribia huyu mtu.

sosi: Kizitto Noya mwananchi.co.tz.


Hate him but the truth is, this is one of the best interviews to have ever been staged by those who are said to aspire for the high office. Kudos Membe for being candid and factual.
 
Kama mtaendelea kujidanganya kuwa raisi ni lazima atoke wizara ya mambo ya nje basi mtakuwa mmeshindwa kuelewa falsafa nzima ya uongozi. Sio kwamba kuwa wizara ya nje ndo utaweza kuendesha vema nchi hii.
Mambo mengi sana yanahitajika. Nadhani hili sihitaji kuliongelea sana kwa sababu rekodi ipo.
Utakuwa mtu wa ajabu kama na rekodi pia hauna
 
Nakuhakikishia Rais anayekuja hatakuwa na doa la ufisadi; uwe wa fedha za RICHMOND au fedha za kutoka kwa serikali ya Gaddaffi!!!

Wananchi Libya wanataseka, hivi hawajaanza kufuatilia hela zao zilizosambazwa na Gadafi maana zinatumika hovyo na bado watu wanajiita waadilifu, dah siasa unafiki sana.
 
Bado ni mapema sana kusema anafaa, rais ni mtu mwenye haiba ya juu, anayetakiwa kuchunguzwa sana, maana huyo ndie anaefanya kazi ya kufikiri na kuamua kwa niaba ya wengine woote anaowaongoza. Hivyo,ni vema tujue falsafa zake na hata misimamo yake popote pale alipowahi kutumikia watu au hata kufanya maamuzi. Siwapingi wanaompenda Membe ila ninatoa changamoto kwa wana jamvi ili kumpima kwa undani na umantiki wa hoja
 
Katika nchi za wenzetu walioendelea, mtu yeyote anayetaka kugombea uongozi wa nchi na hasa ofisi ya URAIS huwa wanaandika vitabu ambavyo huelezea maono yao ya jinsi watakavyokabiliana na matatizo ya nchi zao pindi watakapopata fursa ya kuchaguliwa na kuongoza nchi zao. Hapa kwetu wale wanaowania Urais wanabaki kuita tu waandishi wa habari na kutoa porojo zao zisizoeleweka kwanini wanasaka uongozi na jinsi gani watapambana na kutatua kero zinazowakabili wananchi; wanabakia kusimangana tu kuwa mwenzangu ni fisadi na mimi sio fisadi hivyo mimi ninafaa!!!

Kupitia JF mimi nilimshauri January Makamba kuwa he will have a head start to other aspiring candidates kama angeweka maono yake katika kitabu. Wazee wengi wanausaka URAIS kama njia ya kutaka kwenda kuiba tu na hawana vision wala uwezo wa kuandika kitabu; sioni hata mmoja kati ya hao wanaousaka urais ambaye ni competent kuainisha vision yake ambayo anaweza kuiuza kwa wananchi na ikakubalika!! Can someone envision Wassira, Sitta, Lowassa, Membe, Ngeleja writing a book that spells out what they want to do for the country to rid it of its cronic poverty,diseases and corruption? Nasikia Prof. Mwandosya nae yumo kwenye kinyang'anyoro hiki na anaandika kitabu; let us wait and see what he has to offer!!
 
Panya panya kwani huyo Membe katoka ukoo gani?Kama sio ukoo uleule wa panya?Tunataka fikra mpya kama angekua smart angekua mshauri mzuri kwa mwenyekiti wa mapanya!
 
Back
Top Bottom