Baada ya Pesa Kuisha Kwenye Ulevi, Aila Maiti ya Mama Yake

Mbonea

JF-Expert Member
Jul 14, 2009
640
20






Mwanaume mmoja wa nchini Urusi ambaye alimuua mama yake alipokataa kumpa pesa za kwenda kwenye ulevi, amepunguziwa miaka ya kukaa jela kwa kula maiti ya mama yake baada ya kujitetea kuwa alikuwa na njaa sana na alikuwa hana chakula.

Sergey Gavrilov, 27, alihukumiwa kwenda jela miaka 14 na miezi mitatu baada ya kukiri kula nyama za mwili wa mama yake, limeripoti gazeti la Daily Mail.

"Sikuipenda kabisa nyama ya mwili wake.. ilikuwa na mafuta sana lakini kwasababu nilikuwa na njaa sana ilinibidi niile hivyo hivyo", Gavrilov alinukuliwa mahakamani akisema.

Gavrilov aliiambia mahakama kuwa alikuwa hana pesa za kununulia chakula baada ya kutumbua pesa zake zote kwenye pombe na kamari.

Wakati mama yake, Lyubov, 55, alipokataa kumkopesha pesa za kununulia pombe, alimpiga mama yake kichwani kwa kutumia tofali na kisha kumnyonga kwa kutumia waya wa umeme.

Gavrilov baada ya hapo aliuweka mwili wa mama yake kwenye korido ya nyumba yao na mwili huo uliganda kutokana na hali ya hewa ya baridi kali ya nchini Urusi.

Aliiba pesa za mama yake na kwenda kulewa kwa siku mbili na kurudi nyumbani akiwa amelewa chakari akiwa hana pesa yoyote.

Gavrilov alikuwa na njaa sana na kutokana na kwamba pesa alizomuibia mama yake alizitumbua kwenye ulevi, alikuwa hana pesa za kununulia chakula na hivyo kupelekea akate sehemu ya mwili wa mama yake na kutengeneza supu na pasta.

Gavrilov alikamatwa baada ya mwezi mmoja tangia alipoanza kula nyama za maiti ya mama yake wakati afisa wa polisi alipofika nyumbani kwake kufuatia taarifa kuwa amemuibia mtu simu.

Afisa huyo wa polisi aliukuta mwili wa mama yake ukiwa bado kwenye korido ya nyumba yao huku miguu yake yote miwili ikiwa imenyofolewa.

Katika mazingira ya kawaida ya sheria za Urusi, Gavrilov alikuwa afungwe miaka 15 jela kwa makosa yake aliyofanya lakini jaji wa kesi hiyo alionyesha huruma na kumpunguzia Gavrilov miezi saba kwenye hukumu yake kwa kile alichosema kwakuwa alikuwa na njaa... alihitaji kula ili asife njaa.



Source: News Agencies
 
Back
Top Bottom